Serikali iangalie uwezekano wa kutoa mikopo kupitia halmashauri kwa mtu hata mmoja mmoja badala ya kulazimishwa kuwa katika kikundi

Serikali iangalie uwezekano wa kutoa mikopo kupitia halmashauri kwa mtu hata mmoja mmoja badala ya kulazimishwa kuwa katika kikundi

njia pekee ya serikali kusaidia vijana ni kutunga sheria ambayo italazimisha kila after ten yrs, Rais anaemaliza muda wake anatoka na watu wake wote ambao alihudumu nao

anatoka na wabunge, mawaziri, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, wakurugenzi yan wote ili na vijana wapate hizo nafasi

kijana mwenye mastars ya kilimo au mathematics kumpa mkopo wa milion 2 tena kwenye vikundi na mlolongo mrefu hapana

vijana wanata nafasi hizo hizo zao coz kama elimu viongozi wengi wanazidiwa na hawa vijana wa mtaani
Sasa mkuu wakitoka wote tutajikuta kila baada ya muda huo tunaanza upya kwa kila kitu,na kila kitu kilichokuwa kimeanza na kuanzisha linaweza kisiendelezwe na wapya.

Nachoona Ni lazima kila awamu owe na Sera endelevu katika utengenezaji wa fursa za ajira kwa vijana,ikiwa Ni pamoja na kushirikiana na secta binafsi ili ikue vizuri na kuzalisha ajira za kutosha kwa kuiweka mazingira mazuri ya kisera na kisheria, kusudi wawekezaji wengi wawekeze mitaji yao hapa nchini.

Sanjari na Hilo vijana wasaidiwe na serikali pale wanapoanza biashara zao kwa kuwalea na kuwakuza,ikiwezekana Kodi na mapato waanze kulipa baada ya mwaka mmoja kupita kusudi waweze kusimama imara kibiashara na kuingia katika soko la ushindani
 
viongozi wetu wanaamini ajira kwa vijana ni mambo ufundi, vikundi vya saccos, mjikusanye mfuge bata 10 yan mambo kama hayo

hakuna kiongozi anawaza kukupa ww shamba la hekari 50, na matrecta, mbegu na mbolea ili ulime uje kuwa mfanyabiasha mkubwa au mkulima mkubwa

wao wanataka mambo kama hayo muende kwa mkurugenzi mkalielie pale mpate milion 2 kwa watu kumi, wakati kwao hiyo ni posho ya kikao tu
 
Ndugu zangu watanzania,

Mfumo uliopo kwa Sasa juu ya pesa za halmashauri zinazotolewa Kama mkopo kwa vijana kutokana na makusanyo na mapato ya ndani unataka vijana au akina mama au watu wenye ulemavu kuweza kujiunga au kuunda kikundi cha kijasiriamali ili kuweza kupatiwa mkopo, ambapo hapa kuna taratibu za kufuata ili kukidhi vigezo Kama vile kutengeneza katiba, kuwa na akaunti ya kikundi, viongozi wa kikundi, mradi au wazo la mradi au biashara na mengineyo.

Ndugu zangu katika utolewaji wa pesa hizi hazitoi fursa kwa mtu mmoja mmoja kupatiwa mkopo, ukiwa kijana pekee huwezi ukapata mikopo hii hata Kama Ni muaminifu,una wazo zuri la biashara au mradi au una mradi au biashara ambayo ungependa uongeze na kukuza mtaji wako.

Hali hii inawanyima fursa vijana wengine ambao wanaona katika vikundi Kuna kuwa na baadhi ya changamoto Kama vile uaminifu mdogo kwa baadhi ya wanakikundi,kutofautiana kwa malengo, matumizi mabaya ya Fedha, uzembe wa baadhi ya wanakikundi, wengine kuchukua hela na kuishia kugawana pasipo kutumia katika malengo husika.

Kutokuwa na Elimu ya kutosha juu ya mradi au biashara tarajiwa na hivyo kuishia kupoteza mtaji wote kabla hata ya kurejesha, Haraka ya baadhi ya Wana kikundi au vijana kutaka utajiri wa haraka haraka na hivyo kuwekeza katika maeneo hatari wasio na uzoefu nayo au ujuzi nao zaidi ya habari za kusikia tu juu ya faida kubwa watakayoipata.

Hivyo nilikuwa naona Ni wakati wa serikali ya Rais wetu mpendwa mama Samia kuangalia uwezekano wa kutoa fursa ya mkopo kwa mtu hata mmoja mwenye kuhitaji mkopo huu huku wenye kuungana na kuwa kikundi nao waendelee kupewa Kama kawaida,hii itarahisisha na kusaidia vijana wengi Sana kuweza kupata mikopo na kuwasaidia vijana wengine hata kimawazo na kiushauri.

Vigezo vinavyoweza kutumika ni Kama vile uwepo wa Taarifa za kutosha juu ya mwenendo wa kiuadilifu, kiweledi, kimaadili, kiutendaji, kiuaminifu na kitabia kutoka katika uongozi wa serikali za mitaa.

Uwepo wa mdhamini anayeaminika na mwenye makazi ya kudumu katika eneo analotokea na kuishi kijana anayehitaji mkopo, mdhamini akubali kuwajibika endapo mhusika au kijana ataamua kukimbia au kutoroka kabla ya kurejesha pesa halmashauri.

Mdhamini asaiini fomu maalumu mbele ya mwanasheria wa serikali na kula kiapo cha kuwajibika juu ya Deni la anaye mdhamini na kopi ya fomu hiyo ibaki halmashauri ,nyingine kwa mwanasheria,nyingine kwa serikali ya mtaa ,nyingine kwa anayechukua mkopo na nyingine abaki nayo mdhamini.

Mdhamini awe na Mali zisizo hamishika na zenye hati inayotambulika kisheria,mdhamini awe Ni mzazi wa mhusika au mtu mwingine yeyote mwenye Mali zisizo hamishika na makazi ya kudumu eneo husika,Mdhamini akitaka kumdhamini mtu zaidi ya mmoja aruhusiwe mpaka pale tu itakapothibitika kuwa Mali za mdhamini Zina thamani kubwa ukilinganisha na mikopo au fedha inayotaka kuchukuliwa.

Hili Jambo litasaidia halmashauri kupata marejesho ya mikopo yote inayotolewa kwa vijana lakini pia itawasaidia vijana wengi kupata mikopo kwa urahisi bila mlolongo wa kutafutana na hata kuwalazimisha wengine ili wajiunge kwenye vikundi kusudi kutimiza lengo la kupata mkopo ambapo mwisho wa siku Hawa walio lazimishwa au kupachikwa kwenye kikundi kuweza kusaidia kupata mkopo wanakuwa hawana ule moyo au ufanisi mzuri na uwajibikaji mzuri na wanakuwa hawana mchango wowote ule katika kukuza ,kulinda na kuendeleza mtaji.

Naiomba Sana serikali iliangalie hili kwa jicho la kipekee kabisa, maana unakuta mtu unalima lakini unakosa hela ya pembejeo hasa mbolea kwa kuwa unawaza ukitaka mkopo wa kupanua kilimo chako inahitaji uende kwenye kikundi ambacho unajikuta nacho kina malengo mengine kabisa Kama vile ufugaji wa kuku wa mayai au ng'ombe wa maziwa ambapo unaona wewe huwezi ukapata hata nafasi ya kwenda kukatia ng'ombe majani au kuwawekea maji kuku kwa kuwa wewe shughuli zako Ni shambani muda mwingi na ndio Jambo unalolipenda kuliko ufugaji wa kuku wa mayai au nyama au ng'ombe wa maziwa.

Unakuta kikundi kimeundwa na kuomba mkopo wa Jambo fulani lakini Wana kikundi kila mmoja ana malengo yake kichwani juu ya hela ikiwa mkononi mwao, hivyo kupelekea mradi uliolengwa kukosa nguvu ya pamoja ya wanakikundi.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627
Wazo lako ni zuri sana! Maana unawapatia watu milioni kumi hawana misingi ya biashara, hawajui biashara,wananjaa lazima kwenye makusanyo mtafutane kwa tochi!
Ni vema watafute vijana wajasiliamali walio simama vizuri ndio wawape ili kuongezeea mitaji ili kukuza biashara zao! Kuliko kupambana na mtu anayetapataba hata changamoto za biashara hazijui!
 
Ndio maana wengi wanaishia kupoteza mtaji wote waliopewa Kama mkopo na halmashauri,maana wanakuwa hawana uzoefu wa Biashara Wala kujuwa changamoto za biashara,wanapokuja kupata Elimu na uzoefu inakuwa haina msaada maana wanakuwa wameshapoteza kila kitu Hadi matumaini
 
viongozi wetu wanaamini ajira kwa vijana ni mambo ufundi, vikundi vya saccos, mjikusanye mfuge bata 10 yan mambo kama hayo

hakuna kiongozi anawaza kukupa ww shamba la hekari 50, na matrecta, mbegu na mbolea ili ulime uje kuwa mfanyabiasha mkubwa au mkulima mkubwa

wao wanataka mambo kama hayo muende kwa mkurugenzi mkalielie pale mpate milion 2 kwa watu kumi, wakati kwao hiyo ni posho ya kikao tu
Ndio maana napenda wapewe vijana kwa mmoja mmoja ambao tayari wamesimama na kuwa na msingi wa kibiashara na wanakuwa wanahitaji kukuza mitaji yao na kupanua biashara zao au miradi yao
 
Ndio maana napenda wapewe vijana kwa mmoja mmoja ambao tayari wamesimama na kuwa na msingi wa kibiashara na wanakuwa wanahitaji kukuza mitaji yao na kupanua biashara zao au miradi yao
Kweli kiongozi japo wewe japo ni chawa ila kwa thread hii nakupa 100%
 
Baada ya kukopesha wazalishaji ambao wata create ajira ila tunakopesha washuuzi na tunakopesha vikundi ambavyo hata elimu ya biashara hawana.
 
Ndio maana napenda wapewe vijana kwa mmoja mmoja ambao tayari wamesimama na kuwa na msingi wa kibiashara na wanakuwa wanahitaji kukuza mitaji yao na kupanua biashara zao au miradi yao

Hilo serikali hawawez kufanya, hapo ni Sawa na kumwambia mkurugenzi asitembee na V8

Wao wanataka kutoa milion 2 Kwa watu kumi, mkaanzishe mtaji wa kufuga bata na kuku
 
Juzi nilienda kupata ABCD kama kijana nikaambiwa hayo hayo ya kikundi nilimchallenge yule dada Afisa Maendelo kuhusu kuruhusu mkopo wa mmoja mmoja akasema hilo suala limejadiliwa na sio muda Wizara itatoa tamko lakini hadi sasa kuna matumaini ya kuja kwa mikopo ya mtu mmoja mmoja,
Endelea kua karibu na Halmashauri yako utakuja kupokea habari njema.
Na katika hayo makundi alikuambia kama kuna uorodheshwaji wa mali unazomiliki zisimame kama dhamana?
 
Hilo serikali hawawez kufanya, hapo ni Sawa na kumwambia mkurugenzi asitembee na V8

Wao wanataka kutoa milion 2 Kwa watu kumi, mkaanzishe mtaji wa kufuga bata na kuku
Nina Imani na serikali yangu na naamini Jambo Hili litafanyiwa kazi ili kutoa fursa kwa vijana wengi kunufaika na mpango huu nilioupendekeza
 
Nina Imani na serikali yangu na naamini Jambo Hili litafanyiwa kazi ili kutoa fursa kwa vijana wengi kunufaika na mpango huu nilioupendekeza

Imani yako ni kubwa Sana,

Waache kujilipa ela za posho wampe kijana?

Never in earth, sio tanzania hii labda tanzania ya awamu ya 500
 
Imani yako ni kubwa Sana,

Waache kujilipa ela za posho wampe kijana?

Never in earth, sio tanzania hii labda tanzania ya awamu ya 500
Rais wetu mpendwa mama samia Ni msikivu Sana na mwenye upendo na watanzania,Atasikiliza ombi hili na serikali itarekebisha kanuni
 
N
Ha ha ha ha me Niko hapa always, wazo lako ni zuri Sana na lingesaidia Sana vijana
NAshukuru Sana lakini katika ahadi yako ingekuwa Bora ungetanguliza advansi maana Nina imani kubwa Sana na serikali ya mh Rais mama Samia kufanyia kazi suala hili
 
N

NAshukuru Sana lakini katika ahadi yako ingekuwa Bora ungetanguliza advansi maana Nina imani kubwa Sana na serikali ya mh Rais mama Samia kufanyia kazi suala hili

Ah wapi, wao wanataka mpange folen ya kwa mkurugenzi kusubiria milion 2 Kwa watu 15
 
Back
Top Bottom