Serikali iangalie uwezekano wa kutoa mikopo kupitia halmashauri kwa mtu hata mmoja mmoja badala ya kulazimishwa kuwa katika kikundi

Huu ndio utakuwa mwanzo wa kufa kwa hiyo project.

Risk ya pesa kupotea kwa mtu mmoja ni kubwa kuliko kikundi.

Mtu mmoja anaweza kopa na kutokomea nazo ila kikundi ambacho members wote wapo verified atapatikana tu mmoja au baadhi yao kubeba mzigo in case of default.

Hili jambo lisifanyike.
 
Nimetoa masharti na taratibu za kutoa mkopo kwa mtu mmoja,Soma Tena utaelewa namna ambavyo itakuwa ngumu kwa pesa kupotea bila kulipwa
 
hata mabenki na taasisi zingine za kifedha zimeweka masharti hayo lkn bado watu hawalipi mikopo.watz bado tunadhani mikopo ni zawadi.la msingi ni kweli mikopo ya vikundi inasumbua sana na mfumo huo hauna tija kabisa.aangaliwe mtu mmoja mmoja ambaye yuko serious na biashara akopeshwe.pia kuna mapungufu makubwa kwenye utoaji wa fedha hizo kwa halmashauri.fedha nyingi hutolewa kwa watu ambao si sahihi.hutolewa kwa watu au vikundi ambavyo vina mahusiano na watendaji wa halmashauri.
 
Naamini serikali yetu itafanyia kazi mawazo haya
 
Na katika hayo makundi alikuambia kama kuna uorodheshwaji wa mali unazomiliki zisimame kama dhamana?
Hapana,
Mkishakua kikundi ina maana hapo tayari mmedhaminiana hakutahitajika mali ya mmoja mmoja iwe kama dhamana.
 
Hapana,
Mkishakua kikundi ina maana hapo tayari mmedhaminiana hakutahitajika mali ya mmoja mmoja iwe kama dhamana.
Basi kwenu huko mna neemeka, huku mpaka muorodheshe mali zenu na baada ya hapo mnatakiwa mumtafute mdhamini mwingine mwenye mali zisizo hamishika asimame kama mdhamini

Mi niliwaambia watu kuwa mpo kwenye mkopo mwingine maana hayo masharti hayapo kwenye kanuni za mikopo ya halmashauri
 
Serikali ya tanzania hainaga haraka hiyo kuambiwa kuna uweza wa kuja kwa mikopo ya mtu mmoja mmoja inaweza kuchukua miaka 5 mbele..hapo ni hadi sera ifanyiwe marekebisho.
 
Halmashauri gani hiyo inaujinga hivyo..itaje tuifuatilie.
 
Ndugu Lucas hongera kwa uzi huu.
Nna maswali machache kwako kutokana na uzoefu wako au ulivyo shauri;

1.Serikali za mitaa huwa zinatunza taarifa za kila kijana hapo mtaani kama ulivyosema hapa "Vigezo vinavyoweza kutumika ni Kama vile uwepo wa Taarifa za kutosha juu ya mwenendo wa kiuadilifu, kiweledi, kimaadili, kiutendaji, kiuaminifu na kitabia kutoka katika uongozi wa serikali za mitaa"

2. Kama ndivyo kwy swali la kwanza, unaweza ukanipa majina ya hizo taarifa zinaitwaje na custodian wa hizo taarifa.

3. Umewahi kusikia watu wanaogopa mikopo ya benki kisa watauziwa mali zao hasa nyumba? Huoni hii itakua changamoto kwa watu kukubali kuwadhaminj hao vijana hofu ikiwa mali zao zinaweza taifishwa??

Nimependa ulivyozungumzia mfano wa mahitaji ya mbolea. Kuna namna wazo linaweza boreshwa na naona hili ni la maingi sana na halihitaji dhamana ya mtu mwingine kama likiboreshwa, shamba laweza kuwa dhamana.
 
Katika swali la kwanza ningependaa kukujibu kuwa is huku mikoani tuna vijiji na vitongoji ,Ambapo Kuna kuwa na Mwenyekiti wa Kijiji na kitongoji,kijana anaweza asifahamike vizuri kwa hao viongozi wawili lakini Kuna kiongozi chini Yao anayeitwa Balozi au mjumbe,huyu kwa kiasi kikubwa anawafahamu vizuri Sana watu wake,hata ukitaka kupata taarifa za ndani juu ya mtu fulani Ni Rahisi Sana kupata kupitia watu Hawa.

Pia swala la kwamba watu wataogopa kuuziwa Mali zao hapo ndipo usalama wa fedha za halmashauri utakapokuwepo maana atakayechukua na kukubalika kudhaminika maana take Ni yule anayeaminika vizuri Sana na mdhamini,Hivyo Jambo hili litasaidia halmashauri kupata marejesho ya mkopo wake bila wasiwasi na kusaidia vijana wengine wengi kunufaika,
.
Pia mikopo hii itatolewa kwa vijana waaminifu tu maana ili mdhamini akudhamini Ni lazima awe amejihakikishia na kujiridhisha juu ya weledi uaminifu na umakini wa kijana husika na uwezo wa kuisimamia kuilinda na kuiendeleza pesa atakayopatiwa Kama mkopo
 
Khee!
Kweli hao wapo kwenye mkopo mwingine, mikopo ya Halmashauri haina mambo mengi kubwa ni hilo la kikundi kusajiliwa hapo mtajidhamini wenyewe, katiba, akaunti na utambulisho wa serikali ya Mtaa.
 
Asante kwa majibu nimekuelewa vyema.
 
Khee!
Kweli hao wapo kwenye mkopo mwingine, mikopo ya Halmashauri haina mambo mengi kubwa ni hilo la kikundi kusajiliwa hapo mtajidhamini wenyewe, katiba, akaunti na utambulisho wa serikali ya Mtaa.
Naskia hiyo fomu ipo kabisa imeandika vigezo hivyo na wao wakopaji wanaambiwa na Afisa maendeleo jazeni tu haina shida yeyote na watu wana tii

Ngoja nikiipata hiyo fomu ntaiweka hapa muione
 
Naskia hiyo fomu ipo kabisa imeandika vigezo hivyo na wao wakopaji wanaambiwa na Afisa maendeleo jazeni tu haina shida yeyote na watu wana tii

Ngoja nikiipata hiyo fomu ntaiweka hapa muione
Sawa ukiipata iweke, maana hata mie nimeshangaa
 
Haya mashart Kwa kikundi cha watu 20 wanapewa milion 200 au
Kwanza naskia waliokuwa na mipango ya kukopa M50 walivyoitwa kwenye semina wakashushwa hadi 20M na bado hizo ni ahadi yani hawajapewa

Wametumia pesa nyingi wengine wanadai wametumia zaidi ya 500K na bado hakuna dalili za wao kupata mkopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…