Serikali iboreshe sheria ya Ndoa za Kikristu ili ziruhusu talaka kuepusha mauaji na fumanizi

Mbona talaka zinatoka tangu kitambo kupitia serikalin, na unaposema wakristo wanaongoza kuuwana kisa mapenzi au ndoa ni uongo mtupu yapo matukio kibao ya kiislam sema wanamaliza kimya kimya ninaushahidi nimeshuhudia kabisa acha hizo wewe
 
Mkuu ndoa ya kikristo haina talaka.hilo lipo wazi.

Kama mmeoana kanisani kwa baraka za paroko.

Serikalini unafata nn?

Kule ni madai ya kugawana mali na mengine..
 
Naingoja hio ndoa ambayo mnasema hakuna kuachana!😅 Yani mwanamke anifanyie vimbwanga kisa tu tulifunga ndoa kanisani niendelee kumvungia?

Sijui itakuwaje ila kwa akili zangu nafikiri tutaachana bila hata makaratasi...

Wanawake hawa wote waliojaa mitaani nikose mtu wa kutulizana nae hata kwa sogea tuishi kisha nikahalalisha kimila!
 
Kiongozi wa dini ndio anatoa .Ndio maana ufumbuzi wa hiyo ndoa kukiweko mgogoro huanzia kwenye dini Kwanza sio serikalini
Cheti Cha ndoa kinatolewa na serikali. Yule kiongozi wa dini anayekukabidhi anakuwa ni wakala tu. Na ukitaka kutafuta talaka unakwenda mahakamani, ukifuata taratibu zote mahakama itatoa talaka (itawatenganisha kwa amani kisheria, Kila mmoja awe huru) bila kujali ni ndoa ya kikristo,au dini nyingine.
 
Kabisa
 
Ninavyojua mimi ,serikali haijazuia talaka kwa ndoa za kikristo. Hata ukristo haujazuia talaka bali unadiscourage kitendo cha talaka.
Andiko lako lina walakini.
Pengine ungeshauri wakristo wasidiscourage tendo la talaka na pengine walipigie debe.
Lakini kuna kifungu kwenye Bible kinasema ,,Ninachukia kuachana' sasa sijui mkristo gani atadiriki kufanya machukizo kwa makusudi.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Unasema? Kwani kile cheti huwa ni cha dini fulani au huwa ni vya serikali? Dini hazina vyeti bali wao wamekasimishwa madaraka ya kutoa hivyo vyeti kwa niaba ya serikali! Vikiisha huwa wanaenda kuchukua serikalini!
Ni kweli, vyeti ni vya serikali.
 
Nahisi Kwa mbali kama umeandika kitu usichokijua, sababu ni kwamba hakuna mahali serikali inahusika kuruhusu au kuzuia ndoa kuvunjika. Unapofunga ndoa ya kikristu unatumia nyaraka ya serikali ambayo iko wazi na inaeleza endapo ndoa ni ya mke na Mme mmoja, wake wengi, kimila nk.

Hakuna mahali umezuia kuvunja ndoa mpaka uuwe MTU, haya biblia umeandika Mme na asimwache mke wake isipokuwa Kwa uzinzi, manake imeruhusu ndoa kuvunjika sasa unataka serikali iingilie Kati kufanya nini.

Usiingie kwenye ndoa Kwa sababu umekatiwa Sana viouno, siku ukikutana na anayenyonya Sana utaona viono si kitu, ukikutana na ajiliza saana utaona kote ulikuwa umepotea, ingia kwenye ndoa ukitambua kuna kipindi kitafika airtime ya kugongana itapungua Kwa sababu za kimajukumu.

Usiyumbishwe na Yule unayekutana naye nyote mkiwa mnawaza ngono na ukadhani ni Bora Sana, ukikaa naye miezi miwili utagundua siyo Bora,
 
Alichounganisha MUNGU mwanadamu hawezi tengua. MUNGU anachukia kuachana. Ukitaka ndoa zakuachana baadae nenda kwingine na serikalini. Kwa wakristo talaka no !!!
 
Kuachana ni makubaliano,meridhiano, nafsi zenu wote zikubali
Kwenye ndoa/mahusiano kuna mmoja anaweza
Akawa anadai talaka na mwingine hataki....
Figisu ndiyo inaanzia hapo mpaka kuumizana

Ova
 
Kuachana ni makubaliano,meridhiano, nafsi zenu wote zikubali
Kwenye ndoa/mahusiano kuna mmoja anaweza
Akawa anadai talaka na mwingine hataki....
Figisu ndiyo inaanzia hapo mpaka kuumizana

Ova
Ndipo hapo serikali inatakiwa iwe na suruhisho
 

Mkristu aliyefunga ndoa kwa baba Paroko hakuna kuachana ndomaana maandiko yanasema kwa waliyojaaliwa tu sasa kama ujajaliwa unaenda kufunga ndoa kwa baba paroko ya nini
Siku hizi hata kama mlifunga ndoa ya kikristu kama mmojawapo kaenda kudai talaka mahakamani ,mahakama inatengua kabisa ndoa yenu
 
Boss. Kwani Kuna mtu anakukataza kumuacha mke wako ukimfumania hata Kama umemfumania na waziri.
 
Kwanini serikali iboreshe na sio wakristu wenyewe, je serikali ndio mungu wa wakristu, seriikali ndio ilipanga ndoa ya kikristu,huoni kuwa serikali itakuwa inaingilia mambo ya dini(uhuru wa kuabudu)) nijuavyo mimii ndoa ni ibada.
 
Mkuu ndoa ya kikristo haina talaka.hilo lipo wazi.

Kama mmeoana kanisani kwa baraka za paroko.

Serikalini unafata nn?

Kule ni mudai madai ya kugawana mali na mengine..
Sasa namuelewa mtoa mada anayeomba serikali iingilie kati talaka iruhusiwe kwenye ndoa za kikristo. Mkuu hata nilichokiandika hapo ina maana hujakielewa? Soma tena, kama bado hujaelewa unijulishe nitafute namna rahisi ya kukuelewesha.

Mkuu kwani wewe ulisikia wapi kuwa ndoa ya kikeisto haina talaka?
 
Weka hapa taratibu za kufuata ili watu wapate mwongozo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…