Serikali ilitazame hili kwa jicho la dharula!
ndoa nyingi sana zimekuwa chanzo kikuu cha mauaji!
Ukipitia mafaili na report za kipolisi asilimia kubwa ya mauaji ya kimapenzi ni ndoa za kikristo!
Swali: Kwanini za Kikristo ndiyo zinaongoza!
Jibu: Ni kwasababu serikali haikutoa utaratibu rahisi wa kuachana (Talaka) kwenye ndoa za kikristo!
Hivyo imewafanya wakristo wanaofight divorce kuishi maisha hatarishi zaidi kutokana kwa wenza wao, mbali na migogoro mikubwa ya kupigana na kufumaniana pengine wengine hadi wanaletewa magonjwa kama ukimwi kwa kukosa namna ya kupata talaka
Mfano
Kuna scenario ya mama mmoja ambaye ameishi na Mme wake na kupata watoto watatu kwa kuvumilia, lakini uvumilivu umefika mwisho baada ya mmewake amekuwa ni wa kumpiga, matusi na kumdhalilisha, Mama huyo kariporti Mara kadhaa polisi lakini hajui afanyeje ili apate talaka kisheria!(divorce)
Pamoja na kipigo na masimango, malalamiko mengine ya yule mama ni mmewe kuwa na vimada wengi hadi na mabinti wa kazi ambayo yote kayavumilia lakini hili la kupigwa mme wake anaporudi kalewa limemshinda.
Hivyo kwa mateso ya mama yule, ni dhahiri yupo hatarini kufanya au kufanyiwa mauaji mda wowote!
Lakini kungekuwa na utaratibu mwepesi wa talaka wangeachana kwa Amani! Lakini hajui afanyeje!
Wahanga wa ndoa za kikristo ni wengi sana! Wanandoa wengi wa kikristo wametengana hadi makazi lakini huwa wanafuatiliana ili kufumaniana! (FUMANIZI kwa mgongo wa cheti cha ndoa)
Ndoa zenye migogoro mkewe/mme wanaotengana makazi miezi sita, au mwaka au miaka miwili kila mtu yuko kivyake, lakini kwasababu wanamiliki vyeti vya ndoa hufuatiliana kufumaniana kwasababu HAKUNA TALAKA! (Ili kuprove wrong kwa jamii mmoja amchafue mwenzake)
wahanga wakubwa zaidi wa hili ni wanawake kwasababu ya ushahidi wa tumbo wanapopata wenza wapya na pengine kupata mimba huko!
Nitoe rai kwa serikali Ione umhimu wa kuboresha sheria za ndoa za kikristo kupeana talaka isiwe jambo gumu la kutoana uhai kama kesi za ardhi!
Serikali itambue haina dini, hivyo itengue na mambo ya iman yabaki kiimani, kama vyeti vya ndoa inatoa serikali basi iruhusu pia kutoa talaka kuliko ilivyo ngumu sasa.
Ilivyo sasa inahitaji watalaam sana kufuatilia talaka kwa Wakristo hususani kwa wanandoa wasiona uwezo/ueleewa na sheria.
-Kiufupi Mkuu,bado una uelewa mdogo wa masuala ya sheria hasa sheria ya ndoa (Tanzania Marriage Act 1971) pamoja na mawazo hafifu kuhusiana na katiba ya nchi.Kuna a lot of limitations zilizowekwa na katiba juu ya serikali kuingilia mambo haya ya kidini na ndoa ikiwemo kama ulivyoainisha hapo juu.
-Katiba inatoa uhuru kwa raia wa Tanzania wa kuabudu wanachokiamini,na sheria ya ndoa ambayo iliundwa na ambayo ni consistent na katiba inatambua hilo-Na hata mashauri ya talaka mahakamani yanazingatia sana miongozo ya ulipofungia ndoa (kanisani,msikitini nk.) katika kuamua mashauri yake.
Role ya Wafunga ndoa.
-Wafunga ndoa wamepewa choices kwa mujibu wa sheria ya Tanzania,na kila choices huambatana na wajibu wake pamoja na consequences zake.Mfano-Choice ya kuamua kufunga ndoa ya kiserikali ambayo haifungwi na mambo ya imani.Choice ya kufunga ndoa ya kidini,choice ya kufunga ndoa ya kimila and so on.
-Kila choice unayoifanya inafungwa na taratibu zake,sheria zake,wajibu,tamaduni zake etc.Hivyo ni wajibu wa mwanandoa mtarajiwa kuelewa taratibu za dini husika au dhehebu kiundani kabla ya kufunga ndoa.Tendo hili ni la hiari
-Ukiangalia kiundani utaona sheria imekupa kila aina ya choices (uhuru wa kuamua) kwendana na matakwa ya kikatiba.
- Wanandoa wanatia saini kwenye vyeti vya ndoa kuonesha kukubaliana na yaliyomo kwenye mkataba huo-Unakuwa mkataba Rasmi unaotambulika kisheria pale unapotia sahihi na pande husika ikiwemo mashahidi nk. na kuzingatia taratibu zote halali kwa mujibu wa sheria.
-Tendo la kufungisha ndoa limekaa kiimani zaid kuliko kiserikali hvyo utaona serikali ina role ndogo sana.
*Changamoto nyingi katika maswala haya hujitokeza hasa pale wahusika wanapokuwa wanaongozwa zaid kihisia kuliko kufikiria sawasawa juu ya wajibu mzito uliopo mbele yao (kutokupevuka).Wahusika wanaotarajia kufunga ndoa kutokuelewa sheria na Taratibu za nchi na kiimani kwa ufasaha nk.Mfano- haiwezekani wahusika kufunga ndoa kikristo halafu kutaka kuishi kwendana taratibu za ndoa za kiislam nk.
*Tafiti yako ina base kwenye upande mmoja tu-Unazungumziaje trend inayoongezeka ya wachumba ambao wanauana kabla ya ndoa katika jamii yetu? Unazungumziaje trend ya michepuko kushiriki kuua baadhi ya wanandoa? nk.The problem is very very wider
Who to blame.
-Wanaopaswa kulaumiwa kwa changamoto hz ni wanandoa wenyewe husika kwa kutokufanya machaguo sahihi ya nn wanafanya na wajibu wao ni nn,na consequences ni zipi hasa nk.