Serikali iboreshe sheria ya Ndoa za Kikristu ili ziruhusu talaka kuepusha mauaji na fumanizi

Serikali iboreshe sheria ya Ndoa za Kikristu ili ziruhusu talaka kuepusha mauaji na fumanizi

sasa mbona mahakamani wanatoa talaka freshi tu kwa ndoa za kikristo wewe ndo ulikua hujui
 
Serikali sio mwasisi wa ndoa za kikristo so haiwezi kuingiilia misingi yake,
Msingi na kanuni za ndoa kikristo ni Neno ambalo halibadiliki badiliki, so kazi ipo ni uvumilivu na kusameheana na kuombeana 😀
 
Kwanini inatoa cheti
 
Serikali ilitazame hili kwa jicho la dharula!

ndoa nyingi sana zimekuwa chanzo kikuu cha mauaji!

Ukipitia mafaili na report za kipolisi asilimia kubwa ya mauaji ya kimapenzi ni ndoa za kikristo!

Swali: Kwanini za Kikristo ndiyo zinaongoza!
Jibu: Ni kwasababu serikali haikutoa utaratibu rahisi wa kuachana (Talaka) kwenye ndoa za kikristo!

Hivyo imewafanya wakristo wanaofight divorce kuishi maisha hatarishi zaidi kutokana kwa wenza wao, mbali na migogoro mikubwa ya kupigana na kufumaniana pengine wengine hadi wanaletewa magonjwa kama ukimwi kwa kukosa namna ya kupata talaka

Mfano
Kuna scenario ya mama mmoja ambaye ameishi na Mme wake na kupata watoto watatu kwa kuvumilia, lakini uvumilivu umefika mwisho baada ya mmewake amekuwa ni wa kumpiga, matusi na kumdhalilisha, Mama huyo kariporti Mara kadhaa polisi lakini hajui afanyeje ili apate talaka kisheria!(divorce)

Pamoja na kipigo na masimango, malalamiko mengine ya yule mama ni mmewe kuwa na vimada wengi hadi na mabinti wa kazi ambayo yote kayavumilia lakini hili la kupigwa mme wake anaporudi kalewa limemshinda.

Hivyo kwa mateso ya mama yule, ni dhahiri yupo hatarini kufanya au kufanyiwa mauaji mda wowote!

Lakini kungekuwa na utaratibu mwepesi wa talaka wangeachana kwa Amani! Lakini hajui afanyeje!

Wahanga wa ndoa za kikristo ni wengi sana! Wanandoa wengi wa kikristo wametengana hadi makazi lakini huwa wanafuatiliana ili kufumaniana! (FUMANIZI kwa mgongo wa cheti cha ndoa)

Ndoa zenye migogoro mkewe/mme wanaotengana makazi miezi sita, au mwaka au miaka miwili kila mtu yuko kivyake, lakini kwasababu wanamiliki vyeti vya ndoa hufuatiliana kufumaniana kwasababu HAKUNA TALAKA! (Ili kuprove wrong kwa jamii mmoja amchafue mwenzake)

wahanga wakubwa zaidi wa hili ni wanawake kwasababu ya ushahidi wa tumbo wanapopata wenza wapya na pengine kupata mimba huko!

Nitoe rai kwa serikali Ione umhimu wa kuboresha sheria za ndoa za kikristo kupeana talaka isiwe jambo gumu la kutoana uhai kama kesi za ardhi!

Serikali itambue haina dini, hivyo itengue na mambo ya iman yabaki kiimani, kama vyeti vya ndoa inatoa serikali basi iruhusu pia kutoa talaka kuliko ilivyo ngumu sasa.

Ilivyo sasa inahitaji watalaam sana kufuatilia talaka kwa Wakristo hususani kwa wanandoa wasiona uwezo/ueleewa na sheria.
Labda hiyo kristu. Lakini Mkristo wa kweli hawezi kuifanya serikali wala mamlaka yoyote duniani kuwa Kristo!. Umepotea, nenda eneo lingine hii agenda si yako.
 
Tatizo upo ili kukashifu watu fulani, na huyo ni pepo. Umelelewa katika misingi ya kizinufi
Unauelewa mdogo sana wewe siyo level yangu! Sitakujibu tena! Nisamehe kwa kukwambia vyeti ni vya serikali ila wachungaji wanachokifanya ni uwakala wa kugawa hivyo vyeti!
 
Serikali haiwezi kuingilia mambo ya kidini zaidi na kikatiba wananchi wamepewa uhuru wa kuchagua dini wazitakazo ikiweno kufunga ndoa katika dini wazipendazo.

Kabisa, yaani serikali na ukiristu wapi na wapi. Serikali haina dini.
 
Ni uthibitisho kwa wanandoa!
Serikali inatambua cheti cha ndoa, ila haiusuki na utoaji wa vyeti vya ndoa. We ndoa ya wapi uliona unaenda kuchukulia cheti cha ndoa ofisi ya kijiji au kwa mkuu wa wilaya
 
Serikali inatumbua cheti cha ndoa, ila haiusuki na utoaji wa vyeti vya ndoa. We ndoa ya wapi uliona unaenda kuchukulia cheti cha ndoa ofisi ya kijiji au kwa mkuu wa wilaya
Serikali imeweka utaratibu wa kuwasajili/ kuwapa leseni wachungaji/mashekh ili wawe ni mawakala!
Hivyo watumishi wa Mungu hupewa vyeti na serikali halafu wao ndo huenda kuvigawa kwa waumini wao wanaofunga ndoa!
Ndiyo maana mchungaji asiye na leseni haruhusiwi kufungisha ndoa

Na nyongeza tu, ndoa haitakiwi ifungishwe usiku wa manane uchochori ni MARUFUKU
 
Serikali imeweka utaratibu wa kuwasajili/ kuwapa leseni wachungaji/mashekh ili wawe ni mawakala!
Hivyo watumishi wa Mungu hupewa vyeti na serikali halafu wao ndo huenda kuvigawa kwa waumini wao wanaofunga ndoa!
Ndiyo maana mchungaji asiye na leseni haruhusiwi kufungisha ndoa
Yesu ambaye ndo role model wa ukristo , alifundisha habari za MUNGU kwa kupitia mikutano/ makongamano Na hii ni baada ya kukataliwa na makuhani ambao walikuwa na uhusiano na serikali.
 
Ni uthibitisho kwa wanandoa!
Nabii aliyelala na kitoto cha miaka 9. Nabii aliyeoa mke wa mtoto wake. Nabii aliyemiliki mtumwa na hakuishia hapo akamtumikisha mtumwa huyo kingono. Atakufundisha nini kuhusu ndoa
 
Yesu ambaye ndo role model wa ukristo , alifundisha habari za MUNGU kwa kupitia mikutano/ makongamano Na hii ni baada ya kukataliwa na makuhani ambao walikuwa na uhusiano na serikali.
Usijifanye mcha Mungu kuliko Waroma!

Talaka ni suruhisho kwa watu wengi!

Kama ingekupasa kuwa mcha Mungu , unatakiwa Uoe bikira, na wewe usifanye kabla ya ndoa!
Hivi Leo unaoa mtu kashapigwa miti na kutoa mimba kama zote halafu unajiona kamirifu kwamba eti hutakiwi kuvunja ndoa yenye migogoro?

Kwa taarifa yako ndoa nyingi zimeshikiliwa na vyeti (hawana Mungu)
Na serikali ikiweka utaratibu rahisi wa talaka fasta wengi wataachana
 
Mbona kama unashinikiza? Alafu swala la mimi kumcha au kutomcha MUNGU ni la MUNGU(JEHOVAH na sio Allah ) mwenyewe
 
Back
Top Bottom