Serikali ichunguzeni kampuni ya Mysol, inatesa wananchi

Mkataba uko pale pale lazima ulipie
 
Kwani mkataba wenu ulisema ukipata umeme wa Tanesco usilipie!!??
 
Makubaliano ambayo mlifanya wakati mnaandikishana ndiyo yataamua ubaki na Sola milele ama ulipe hela za watu, Binafsi naona hapo mleta mada ndiyo hajui kwamba hajui. Anakazania kusema kampuni linanyanyasa wanainchi.
Hapa mkuu ..mteja ndio ana nyanyasa kampuni....
 
Ww unatakiwa, aidha malizia deni/ wakabidhi mali yao. Ninyi waha/wahaya huwa ni wasumbufu sana kwenye mikataba.
 
Mm nimewahi kuhuduma ktk ofc hyo zamani ijulikana kama mobisol nimewai kuwa afsa wa juu sna ktk kampuni hyo yenye makao yake makuu mjini Arusha 88 hapo njiro hill

Kwa kifupi Sana wew ndio tatizo mkp hapo hvyo unaweza kufikishwa mahakamani na kutakiwa kulipa na Deni lote pmj na fine juu
Haiwezekani utumiee mtambo wa watu muda wote na hujamaliza Deni lao alfu Leo hi unakuja huku kulialia tukuonee huruma
Eti kissa umeunganishwa umeme wa grid ,takatkaa gani unaaongea kiongozi

laiti ningekuwa Bado Niko myso Kama afsa wwake alfu ukute mm ndio area manager au zonal manager ningekukata makof manne mazito kwa kuaribu Sola yetu nakuchapa mbele ya mkeo na watoto wako
 
Mkataba unasemaje maana umelipa 1 na point m kati ya 2 na point m, so lazima ulipe maana ndo maana ya mkataba,

Leo waliita lisora lakini wakati unaingia mkataba uliita solar ,acha hujua heshim mkataba, ukileta ubishi watakushitaki na utalipwa nyingi kuliko iliyobaki
 
Wewe ndiye tatizo!😁.

NB:Hao siyo TALA wala BRANCH,utautapika tu huo mtambo wao.
 
Yaani bila kuuna uma maneno....ukweli ni kwamb wewe nyapinyapileo

Ndie uliyekiuka masharti ya mkataba.
Ulipoingia makubaliano nao,na ukakubali kulipa kwa awamu.
Ni lazima ukamilishe malipo yako na wao ili wakuachie hiyo solar,lazima ukamilishe malipo yao.

Vinginevyo utakuja kuburuzwa mahakamani na utajikuta ukilipa mara mbili zaidi,pamoja na gharama zao za kuendesha kesi pamoja na Riba na pia Usumbufu uliowasababishia.

Acha ubishi wa kiha!
 
Mkataba uko pale pale lazima ulipie
Ndugu yangu,watz wenzangu hii mikataba hata ile mingi ya serikali huwa wanakimbilia kusaini tu kwa mihemko, bila kusoma vizuri T&C's na matokeo yake ndio kama huyu jamaa wa solar! Yaani yeye ni kutekelezaj mkataba unavyosema, na hakuna longolongo za kwamba sasa amepata umeme wa TANESCO hapo.....
 
Watu wanaoingia solar za mikataba nawashangaa sana, mbona mitambo ipo mingi tu sokoni ni wewe tu kwenda kuchukua unaoumudu
 
Rejea kwenye mkataba wenu.Kama unasema ukiingiza umeme deni litakoma sawa.Lakini kama mlikubaliana ulipe hadi kumaliza unalo hilo.
 
Mtoa mada utalipishwa mara tano ya bei ya mtambo ukipelekwa mahakamani. Bora ulipe hilo deni maana hata wakichukua mtambo wao pia wanaweza kukushitaki kwa kuvunja mkataba na usumbufu tena hapo kama huo mtambo ndio dhamana. Wanauchukia na kukugeuzia kibao

Mchawi ni huo mkataba ulioingia

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Mysol wanastahili pongezi, wakachukue mitambo yao hizi Kampuni za zinazowekeza kwenye nishati ya umeme zilistahili zipunguziwe kodi ili nao washushe bei zao zaidi.
 
Tukiachana na huyu muha kuacha kulipa deni,hii kampuni ni ya kitapeli,mitambo yao ina tabia ya kujizima yani hata kama kuna jua unatumia masaa matatu tu usiku inazima licha ya kwamba hukutumia during daytime

Ukiwapigia wanakuja mafundi wao wanakushauri ununue battery na wanataka uwalipe pia, simshauri mtu kununua hizo solar,ukimaliza tu kuwalipa deni mtambo unakufa
 
Wewe ndo tatizo na siyo hiyo kampuni!! Makubaliano yalikuwa kuwalipa na wewe kubakia na solar yako!!

Huwezi kungangania kubakia na vifaa vyao vya solar wakati hujakamilisha mkataba wako!!

Kupata kwako umeme wa Tanesco siyo kigezo cha kutowalipa!!

Ni haki ya kabisa ya msingi kukunyanganya hivyo vifaa maana wewe ndo umevunja mkataba na si wao!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…