Serikali ifanye 'due diligence' mkataba TANESCO kukodisha software kwa Dola 30m toka kampuni ya India

Serikali ifanye 'due diligence' mkataba TANESCO kukodisha software kwa Dola 30m toka kampuni ya India

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Chini ya dr Menard Kalemani tuliambiwa tanesco tayari ilikua inajiendesha yenyewe na taarifa ya mwisho ya hesabu shirika lilianza kupata faida.

Asili ya tanesco kua mzigo ni kugeuzwa shamba la bibi na wapigaji. Mikataba ya uzalishaji ya kinyonyaji na makampuni binafsi na ubadhilifu wa vigogo ndio ilikua kawaida.

Baada ya Rais kumuondoa Kalemani na kumuweka Januari Makamba watu wameshituka. Huo ndio ukweli mtupu. Wananchi hawamuamini Januari kutokana na kauli zake na kundi lao kukejeli na kudharau juhudi za Magufuli alipokuwa Rais.

Makamba ameanza kuweka watu wake kwenye bodi wakiwepo wafanyabiashara wakubwa halafu mara shirika linaingia mkataba wa kukodi software eti ya management kwa dola za kimarekani milioni 30.

Kama Serikali imefanya uchunguzi wa nani anataka kupewa kandarasi za kujenga meli za shirika la meli 'due diligence' na kukuta madudu ya kutisha tungependa wafanye pia uchunguzi kama ilikua lazima kukodi software ya management na kwa bei hiyo kubwa ya kushangaza. Na pia kama utaratibu wa manunuzi wa serikali haujakiukwa.

Kuna watu nchini wanasifiwa tu wakati ujuzi wao ni kutoa kandarasi za kipigaji tu. Inavyofahamika nchini kuna wajuzi wazuri wa tehama na wameweza kutengeneza software nzuri zinatumika na serikali. Hawa kina Januari na timu yake ameweka tanesco ni sawa na wale walitaka kupeleka ndege ya air tanzania afrika ya kusini kuweka nembo na maandishi ya kampuni kwa dola millioni kadha.

Ikiwa tunataka kuendelea lazima tusimamishe upigaji.

Kwa hivyo tunataka uchunguzi wa ukodishaji hiyo software vinginevyo hayo ya bandari tutaona ni 'selective' action kufanya show tu. Ni mambo yale ya awamu ya nne yaani usanii tu.
 
Serikali Mtandao (e-Government Authority (eGA)) wanasemaje juu ya hili? Miongozo yao imefuatwa? Hivi kukodisha ndio kwa kiingereza ni subscription?
 
Za chini ya kapeti ni kuwa hizi ni dili za kuwarudishia hela zao waliominywa na JPM, na kwa minajili hii msishangae kusikia kuwa kampuni nyingine zimepewa zabuni ya kusambaza vitu fulanifulani. Yaani ni Upigaji mtupu kwenye awamu hii ya Samia.
Ukichunguza hili dili utakuta watu wana 10% zao humo.

Hili ni dili linalonuka ufisadi wa kufa mtu, Samia hawezi kukwepa Lawama kwa vitu vyenye harufu ya UPIGAJI kama hivi
 
Za chini ya kapeti ni kuwa hizi ni dili za kuwarudishia hela zao waliominywa na JPM, na msishangae kusikia kuwa kampuni nyingine zimepewa zabuni ya kusambaza vitu fulanifulani
Ukichunguza hili dili utakuta watu wana 10% zao humo
Hili ni dili linalonuka ufisadi wa kufa mtu, Samia hawezi kukwepa Lawama kwa vitu vyenye harufu ya UPIGAJI kama hivi
Ya sirini yataletwa wazi
 
Yaani TANESCO na Bandari zimegeuka Taasisi za Kupigia hela za Watanzania.

IPTL, Escrow, Symbion, Richmond na Leo Mkataba wenye viashiria vyote vya kifisadj uliosainiwa na TANESCO juzi hapa kwa hiyo kampuni ya kihindi vyote hivyo ni sehemu ya ufisadi uliotokea TANESCO.

Wizi mtupu
 
Sidhani kama atakubali kufanya "due diligence" na kama asipokubali ifanyike, basi ndio itadhihirika wapigaji wa awamu ya nne sasa wameshika hatamu.

Nina wasiwasi sana na wale wazito wa awamu ya nne waliokwapuliwa mali zao walizopata kwa wizi wakati ule, zile furaha zao twitter baada ya msiba wa JPM lazima watakuwa na mipango ya kuzirudisha kwa kumtumia "mama"
 
hivi hawa kamaa kweli wako == kichwani yaani wananunua software ya php kwa billion of money wakati smart codes ama Magilla tech wangeweza kuwauzia kwa shilingi million 30
 
Ndo hivyo yaani nimeshangaa unakodisha software yaani sio hata kununua kwa 30m usd
 
Sidhani kama atakubali kufanya "due diligence" na kama asipokubali ifanyike, basi ndio itadhihirika wapigaji wa awamu ya nne sasa wameshika hatamu.

Nina wasiwasi sana na wale wazito wa awamu ya nne waliokwapuliwa mali zao walizopata kwa wizi wakati ule, zile furaha zao twitter baada ya msiba wa JPM lazima watakuwa na mipango ya kuzirudisha kwa kumtumia "mama"
Huku tunakamuliwa tozo na huku watu wanagawana tozo zetu kirahisi hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ERP COST.png
 
Kuna watu wengi wameshalipia kuunganishiwa umeme, wanapigwa danadana, hizo pesa si bora zingeenda kununua meter na vifaa ili watu wengi wapate umeme TANESCO waendelee kukusanya pesa za mauzo ya umeme?

Kwani tatizo la ufanisi wa TANESCO ni kukosekana kwa ERP au mfumo mbovu?
 
Eti "naangushiwa gari bovu" wakati umepanda gari bovu ulilonunua kwa pesa yako ya urithi! Shame!
 
Za chini ya kapeti ni kuwa hizi ni dili za kuwarudishia hela zao waliominywa na JPM, na kwa minajili hii msishangae kusikia kuwa kampuni nyingine zimepewa zabuni ya kusambaza vitu fulanifulani. Yaani ni Upigaji mtupu kwenye awamu hii ya Samia.
Ukichunguza hili dili utakuta watu wana 10% zao humo.

Hili ni dili linalonuka ufisadi wa kufa mtu, Samia hawezi kukwepa Lawama kwa vitu vyenye harufu ya UPIGAJI kama hivi
Ndiyo maana walimdanganya Mama na slogan ya “Kazi iendelee” yaani wao akina Makamba walimaanisha kazi ile ya enzi za Dkt Jakaya ya uzembe, wizi na ufisadi iendelee. Siyo ajabu kuona wanatafuta hela kwa nguvu ili pia 2025 waweze kumpiku Mama. Yaani tunamhurumia Mama, angewajua walivyo walafi ni bora hata angetumia ushauri wa kitengo kuendesha serikali yake lasivyo hawa mchwa mpaka 2025 watambakiza Mama akiwa ana kashfa kuzidi za Dkt Jakaya.
 
Chini ya dr Menard Kalemani tuliambiwa tanesco tayari ilikua inajiendesha yenyewe na taarifa ya mwisho ya hesabu shirika lilianza kupata faida.

Asili ya tanesco kua mzigo ni kugeuzwa shamba la bibi na wapigaji. Mikataba ya uzalishaji ya kinyonyaji na makampuni binafsi na ubadhilifu wa vigogo ndio ilikua kawaida.

Baada ya Rais kumuondoa Kalemani na kumuweka Januari Makamba wa tu wameshituka. Huo ndio ukweli mtupu. Wananchi hawamuamini Januari kutokana na kauli zake na kundi lao kukejeli na kudharau juhudi za Magufuli alipokuwa Rais.

Makamba ameanza kuweka watu wake kwenye bodi wakiwepo wafanyabiashara wakubwa halafu mara shirika linaingia mkataba wa kukodi software eti ya managrment kwa dola za kimarekani milioni 30.

Kama Serikali imefanya uchunguzi wa nani anataka kupewa kandarasi za kujenga meli za shirika la meli 'due diligence' na kukuta madudu ya kutisha tungependa wafanye pia uchunguzi kama ilikua lazima kukodi software ya management na kwa bei hiyo kubwa ya kushangaza. Na pia kama utaratibu wa manunuzi wa serikali haujakiukwa.

Kuna watu nchini wanasifiwa tu wakati ujuzi wao ni kutoa kandarasi za kipigaji tu. Inavyofahamika nchini kuna wajuzi wazuri wa tehama na wameweza kutengeneza software nzuri zinatumika na serikali. Hawa kina Januati na timu yake ameweka tanesco ni sawa na wale walitaka kupeleka ndege ya air tanzania afrika ya kusini kuweka nembo na maandishi ya kampuni kwa dola millioni kadha.

Ikiwa tunataka kuendelea lazima tusimamishe upigaji.

Kwa hivyo tunataka uchunguzi wa ukodishaji hiyo software vinginevyo hayo ya bandari tutaona ni 'selective' action kufanya show tu. Ni mambo yale ya awamu ya nne yaani usanii tu.
Usiwe na wasiwasi. Tuko kazini. Soon or later.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Yaani TANESCO na Bandari zimegeuka Taasisi za Kupigia hela za Watanzania.

IPTL, Escrow, Symbion, Richmond na Leo Mkataba wenye viashiria vyote vya kifisadj uliosainiwa na TANESCO juzi hapa kwa hiyo kampuni ya kihindi vyote hivyo ni sehemu ya ufisadi uliotokea TANESCO.

Wizi mtupu
Yaani Mtanzania ama mwafrika kwa ujumla mwanasiasa anaona raha kujiibia.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Tulipaza sauti ba kusema wizara ya nishati ni woszara nyeti.. aliitaji bla bla nyingi inaitaji strong management, critical minds..
Sasa wanaleta mwanasiasa kui- manages this department ni haibu kwa Taifa.
 
Mama hawezi kumkagua makamba ambae ni waziri wake wa mchongo, CCM ni ukoo wa panya, ukiona uchunguzi umefanyika ujue ni kwa wale wasohitajika ili kuwaharibia, katiba mpya ni muhimu sana kwa taifa letu kuliko kitu chochote kile kwa sasa.
 
Back
Top Bottom