Serikali ifanye operesheni ya mashine bubu za kamari mitaani, Wachina wanahujumu uchumi

Serikali ifanye operesheni ya mashine bubu za kamari mitaani, Wachina wanahujumu uchumi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Jana nilipita maeneo ya Kigamboni, nikaingia uchochoroni sehemu moja karibu na msikiti wa Feri upande wa Kigamboni nikaona mashine moja ya Kamari uchochoroni kabisa, katika kibanda kisicho na hadhi hata kidogo, kimefichwa ndanindani.

Mchina mmoja akaifungua, akatoa machenji kibao ya shilingi mia mbili mia mbili akaweka kwenye kitu kama kikapu akapeleka kwenye mzani wa kupimia zile chenji (Inaelekea njia ya kuzihesabu kwa kuwa ni nyingi sana wanazipima kwa kilo wanajua kuwa kilo fulani ni shilingi fulani).

Palepale kuna sehemu kuna vijana wanachukua hayo machenji wanaenda kuyauza kama chenji kwa watu wa daladala—Yaani wanatakatisha hizo pesa kwa mtindo huo.

Kinachonisikitisha Wachina wanatoka huko kwao wanakuja maelfu ya Kilometa, wanafanya biashara haramu freely kabisa katika ardhi yetu na serikali ipo, haifanyi lolote, uchumi unahujumiwa lakini serikali inang'aang'aa macho tu.

Haya mambo ya wachina kufanya hizi kamari serikali yetu inajua na ni miaka michache huko Morogoro walikamatwa Wachina wamehodhi maelfu kwa maelfu ya coins.

Hizi coins wanazozihodhi inapeleka kupungua katika mzunguuko na matokeo yake kuleta shida katika uchumi wa nchi.

Nakueleza ukweli haya mambo ambayo Wachina wanayafanya, ya kuvamia vyanzo vya maji na kulima, kukata magogo hovyo, kufanya kamari na kudisturb uchumi wahusika wanayajua, wanakula rushwa kisha wanakaa kimya!

Nakueleza Ukweli, huu ujinga ambao wachina wanafanya, huwezi kwenda China ukafanya ujinga kama huo nchini mwao, ni kwa sababu wana akili.

Mbona sisi tunakuwa kama Mazuzu, tunauza nchi very cheap. Why?
 
Hatuwezi kuwazuia Wachina kufanya hizo biashara zako za kamari. Hizo mashine zenyewe zinalipiwa kodi ya maana pale bandarini.

Kipaumbele cha serikali ni kodi kwahiyo acha tukusanye kodi. Nawe kama una ganja unataka kuuza wewe tupe tu kodi yetu.
 
Tatizo la gambling ni uraibu kama wa pombe hakuna anae kulazimisha kwenda ku gamble cha msingi serekali itengeneze namna nzuri ya kupata kodi kwenye hizo mashine.

Soma kuhusu pathological gambling
 
Tatizo la gambling ni uraibu kama wa pombe hakuna anae kulazimisha kwenda ku gamble cha msingi serekali itengeneze namna nzuri ya kupata kodi kwenye hizo mashine.

Soma kuhusu pathological gambling
Kwa China gambling holela mitaani ni marufuku!, ni kosa la jinai huko kwao

Ila wao wanakuja kuchukua utajiri kilaini kwa Watanzania mbumbumbu.
 
Kama kweli wanafanya kinyemela, nakubaliana na wewe serikali ifanye hiyo operesheni, na kuwafungulia kesi ya uhujumu uchumi!

Hata hivyo, maelezo yako hayajitosheleza ku-conclude kwamba wanafanya biashara haramu! Na hata unaposema:-
Mchina mmoja akaifungua, akatoa machenji kibao ya shilingi mia mbili mia mbili akaweka kwenye kitu kama kikapu akapeleka kwenye mzani wa kupimia zile chenji (Inaelekea njia ya kuzihesabu kwa kuwa ni nyingi sana wanazipima kwa kilo wanajua kuwa kilo fulani ni shilingi fulani)

Palepale kuna sehemu kuna vijana wanachukua hayo machenji wanaenda kuyauza kama chenji kwa watu wa daladala—Yaani wanatakatisha hizo pesa kwa mtindo huo
Hakuna utakatishaji pesa wa aina hiyo... hapo wanachofanya ni kubadili coins kuwa notes lakini zote ni pesa!!

Unaposikia kutakatisha pesa, ni kuchukua dirty money na kuziingiza kwenye biashara halali ili hatimae akipeleka benki na akaulizwa mamilioni yote haya yanatoka wapi (Benki wana huo wajibu), basi atasema nafanya biashara ya Real Estates, na leo nimeuza nyumba 3, na unaonesha docs za kuuza nyumba tatu!

Kumbe alichofanyahapo kabla ni kuchukua pesa zake chafu, mathalani drugs money na kufungua Biashara ya Real Estate, na pesa atakayopata kupitia real estate ni CLEAN MONEY kwa sababu benki hawatakuuliza tena ulipata wapi mtaji wa kuanzisha real estate business... hiyo sio kazi yao! Ni kazi ya mamlaka nyingine siku akija kuwa suspect!
 
Karibu 20 ya pesa za nchi hii wanaziiba wachina kupitia haya madubu.
Unaweza usiamini hili lakini jitahidi tu niamini Mimi.
Uswahilini pato karibu lote linachukuliwa na Wachina kupitia haya madubwi
Halafu wajanja, wana mtandao mrefu hadi ndani ya jeshi la polisi, wanalindwa

Pia wanashirikiana na vijana wa Kitanzania wale wanaowaona ni wajanjawajanja na watemiwatemi ili kujilinda ndani ya jamii!

Kiufupi Wachina wanatorosha utajiri.

Wakishachukua hela mtaani kwa mtindo wa kamari, wanakwenda bureau de change, wananunua dola kisha wanaenda kwenye benki zao za wachina kudeposit hizo pesa kwenye account za benki zao za China

Yaani hii nchi itaendelea kuwa masikini kutokana na ujinga na ubinafsi wa wenye dhamana
 
Ukisikia Wachina wanaisifia nchi ndio kwa ishu kama hizi usidhani kuna cha maana.

Na viongozi wetu corrupt nao ukiwasikia wanavyowasifua Wachina ujue wamesha kaa mezani.

Kule kwao adhabu ya rushwa ni kali sana kwani wanajua madhara ya rushwa lakini huku wanazigawa kama njugu kwa baraka ya hiyo hiyo serikali yao...yaani ni kama unavyopigwa marufuku nyumbani kula makombo lakini unawapelekea Nguruwe.
 
Kama kweli wanafanya kinyemela, nakubaliana na wewe serikali ifanye hiyo operesheni, na kuwafungulia kesi ya uhujumu uchumi!

Hata hivyo, maelezo yako hayajitosheleza ku-conclude kwamba wanafanya biashara haramu! Na hata unaposema:-

Ha

za tena ulipata wapi mtaji wa kuanzisha real estate business... hiyo sio kazi yao! Ni kazi ya mamlaka nyingine siku akija kuwa suspect!
Inawezekana unajua sana kuhusu mambo ya money laundering kuliko mimi. But my point is angalia hii michezo ya kamari holela, kila kona ya nchi, hadi uswazi huko vichochori hizi machine zimekuwa installed.
Wachina nao wana vimashine vyao wanapiga hela za watanzania. Mamlaka zipo na zinaacha haya mambo kufanyika holela mitaani, hayako regulated.

Hebu weka input yako ili kusaidia nchi katika hili suala
 
Hizo biashara ni halali, siku hizi una bet hata kwa simu. Hakuna anae kulazimisha ku gamble
 
Jana nilipita maeneo ya Kigamboni, nikaingia uchochoroni sehemu moja karibu na msikiti wa Feri upande wa Kigamboni nikaona mashine moja ya Kamari...
Hisia zako kuhusu kamali umeamua ziwe hasi tu. Sioni ubaya wa tukio lote ulilolielezea. Tatatibu za leseni na mapato tu ndiyo Ziangaliwe

Kuhusu chenji; labda wewe mwenzetu ni tajiri unayemiliki usafiri binafsi. Lakini wauza chenji wamerahisisha sana maisha ya abiria kwa kuwa ile ya konda kusema nendeni watatu au wanne baada ya kuteremka mkagawane chenji imekwisha.

Hatua zozote zinazopunguza ajira kwa vijana lazima tuzipige vita
 
Wakishachukua hela mtaani kwa mtindo wa kamari, wanakwenda bureau de change, wananunua dola kisha wanaenda kwenye benki zao za wachina kudeposit hizo pesa kwenye account za benki zao za China

Yaani hii nchi itaendelea kuwa masikini kutokana na ujinga na ubinafsi wa wenye dhamana
Kuna sheria inayokataza kuchenji hela Bureaux de Change na kuweka kwenye Akaunti?

Yaani Tanzania iwe maskini kwa sababu hiyo?

Naona Missile of the Nation umepoteza FOCUS kwenye huu uzi
 
Wachina wanasaidia utekelezaji wa ilani ya chama [emoji4][emoji116]
1806634_37962591_1905218849557975_6157850605487390720_n.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom