Serikali ifanye operesheni ya mashine bubu za kamari mitaani, Wachina wanahujumu uchumi

Mtoa mada alikuwa akipita pita polini mara ghafla DUBU huyu hapa ah, ameliwa mtoa mada na dubu jamani nilisikia mayowe tu mamaaaasss
 
Nakueleza Ukweli, huu ujinga ambao wachina wanafanya, huwezi kwenda China ukafanya ujinga kama huo nchini mwao, ni kwa sababu wana akili.

Mbona sisi tunakuwa kama Mazuzu, tunauza nchi very cheap. Why?
Mshana Jr, kilichonisikitisha zaidi ni nilichokisoma katika comments za watu katika uzi huu. Yaani people are so naive, hawajali, wanaona eti wachina wanachofanya ni sawa. Wanadai eti kama kuna sheria inaruhusu hilo basi eti ni sawa tu, Badala wapige kelele haya mambo yawe regulated ikibidi sheria ibadilishwe na uwepo uthibiti zaidi, wao wameridhika na hali eti kwa kuwa hali iko hivi ilivyo basi tuwaache wachine wawapune waswahili huko uswazi!. Tuna tatizo la IQ, IQ zetu ni ndogo sana
 
Pamoja na idara husika kufanya kazi zao bado kuna nyufa nyingi katika kusimamia misingi na sheria za kazi. Kuna mahali tumekosea. Raia wa kigeni wako huru sana kufanya watakavyo. Wanakuja nchini kufanya shughuli za umachinga na unaweza kukuta bila leseni hata vibali vya kuishi nchini na hawaguswi. Sina hakika lakini nahisi tumerelax mno kiasi wageni wanafanya shughuli za ajabu lakini zikiwaingizia pesa bila kubugudhiwa!
IQ zetu ndogo
 
Jana nilipita maeneo ya Kigamboni, nikaingia uchochoroni sehemu moja karibu na msikiti wa Feri upande wa Kigamboni nikaona mashine moja ya Kamari uchochoroni kabisa, katika kibanda kisicho na hadhi hata kidogo, kimefichwa ndanindani.

Mchina mmoja akaifungua, akatoa machenji kibao ya shilingi mia mbili mia mbili akaweka kwenye kitu kama kikapu akapeleka kwenye mzani wa kupimia zile chenji (Inaelekea njia ya kuzihesabu kwa kuwa ni nyingi sana wanazipima kwa kilo wanajua kuwa kilo fulani ni shilingi fulani).

Palepale kuna sehemu kuna vijana wanachukua hayo machenji wanaenda kuyauza kama chenji kwa watu wa daladala—Yaani wanatakatisha hizo pesa kwa mtindo huo.

Kinachonisikitisha Wachina wanatoka huko kwao wanakuja maelfu ya Kilometa, wanafanya biashara haramu freely kabisa katika ardhi yetu na serikali ipo, haifanyi lolote, uchumi unahujumiwa lakini serikali inang'aang'aa macho tu.

Haya mambo ya wachina kufanya hizi kamari serikali yetu inajua na ni miaka michache huko Morogoro walikamatwa Wachina wamehodhi maelfu kwa maelfu ya coins.

Hizi coins wanazozihodhi inapeleka kupungua katika mzunguuko na matokeo yake kuleta shida katika uchumi wa nchi.

Nakueleza ukweli haya mambo ambayo Wachina wanayafanya, ya kuvamia vyanzo vya maji na kulima, kukata magogo hovyo, kufanya kamari na kudisturb uchumi wahusika wanayajua, wanakula rushwa kisha wanakaa kimya!

Nakueleza Ukweli, huu ujinga ambao wachina wanafanya, huwezi kwenda China ukafanya ujinga kama huo nchini mwao, ni kwa sababu wana akili.

Mbona sisi tunakuwa kama Mazuzu, tunauza nchi very cheap. Why?

Nilienda Bagamoyo Kidomole kuangalia shamba langu. Wakati nasubiri wafanyakazi wangu waje njia panda nikaona gari lina park na wachina wawili wakashuka wakaenda kwenye kibanda na kurudi na mfuko.

Nilishangaa kuona wachina wako huko. Nilivyo uliza watu wa pale wakasema ni wamiliki wa machine za kamari na pesa nyingi za bodaboda zinaishia huko. Cha ajabu ni kwamba wachina wanapita kukusanya pesa sio kuweka pesa!.

Hii ni biashara ambayo haina faida yoyote na hiyo kodi wanayopata serikali ni ndogo ukilinganisha na pesa zinazotoka kwenye hizi jamii masikini.
 
Jana nilipita maeneo ya Kigamboni, nikaingia uchochoroni sehemu moja karibu na msikiti wa Feri upande wa Kigamboni nikaona mashine moja ya Kamari uchochoroni kabisa, katika kibanda kisicho na hadhi hata kidogo, kimefichwa ndanindani.

Mchina mmoja akaifungua, akatoa machenji kibao ya shilingi mia mbili mia mbili akaweka kwenye kitu kama kikapu akapeleka kwenye mzani wa kupimia zile chenji (Inaelekea njia ya kuzihesabu kwa kuwa ni nyingi sana wanazipima kwa kilo wanajua kuwa kilo fulani ni shilingi fulani).

Palepale kuna sehemu kuna vijana wanachukua hayo machenji wanaenda kuyauza kama chenji kwa watu wa daladala—Yaani wanatakatisha hizo pesa kwa mtindo huo.

Kinachonisikitisha Wachina wanatoka huko kwao wanakuja maelfu ya Kilometa, wanafanya biashara haramu freely kabisa katika ardhi yetu na serikali ipo, haifanyi lolote, uchumi unahujumiwa lakini serikali inang'aang'aa macho tu.

Haya mambo ya wachina kufanya hizi kamari serikali yetu inajua na ni miaka michache huko Morogoro walikamatwa Wachina wamehodhi maelfu kwa maelfu ya coins.

Hizi coins wanazozihodhi inapeleka kupungua katika mzunguuko na matokeo yake kuleta shida katika uchumi wa nchi.

Nakueleza ukweli haya mambo ambayo Wachina wanayafanya, ya kuvamia vyanzo vya maji na kulima, kukata magogo hovyo, kufanya kamari na kudisturb uchumi wahusika wanayajua, wanakula rushwa kisha wanakaa kimya!

Nakueleza Ukweli, huu ujinga ambao wachina wanafanya, huwezi kwenda China ukafanya ujinga kama huo nchini mwao, ni kwa sababu wana akili.

Mbona sisi tunakuwa kama Mazuzu, tunauza nchi very cheap. Why?
Ukiona hivyo ujue hiyo ni miradi ya CCM ndiyo wenye uswahiba na hao wachina wanawakusanyia hela za uchaguzi mkuu 2025
 
[emoji23] umenikumbusha siku moja mchina alimpeleka jamaa polisi ambaye aliweka mashine ya kamari.kila anapokuja kuangalia imeingiza sh ngapi inasoma 0 .sijui iliishia wapi hiyo kesi
 
Back
Top Bottom