Serikali ifanye operesheni ya mashine bubu za kamari mitaani, Wachina wanahujumu uchumi

Mimi msimamo wangu ni kutokana na mafundisho ya dini kucheza kamari ni haramu...kamari zote hazipo kumtajirisha mtu
Usiseme kupitia hizo mashine watu wanaliwa pesa zao ,pia tunaona watu wakipoteza pesa zao kupitia betting za mipira japokuwa unasema zinaendeshwa vizuri...kamari ni haramu...kama umeamua kuacha mafundisho ya dini Acha kamari ikufilisi
 
Mbona walikamatwa Morogoro hao Wachina?
Kwa sababu walikuwa wanaendesha biashara ya kamali bila kufuata sheria!! Hata hao anaowasema Misile of The Nation ikithibitika wanaendesha isivyo halali, nao WANAPASWA KUKAMATWA!

Hawatakamatwa kwa sababu wanaendesha michezo ya kamali bali kuendesha michezo ya kamali bila kufuata sheria!
 
Sidhani kama mmemuelewa mtoa mada ama mnachangia kishabikii

Mtoa mada hapingi kamari, anapinga kamari za uchochoroni na swali lake hasa ni are they controlled?

Pia kuna conspiracy ya MONEY LAUNDRY yaani utakatishaji wa fedha

Kamari inaruhusiwa na ndo maana kuna hadi Bodi ya michezo hii ya kubahatisha lakini shida iko kwenye hizo za uchochoroni, je usimamizi ukoje?
Je uchunguzi unafanyika kujua machine hazijatekenywa kupunguza zaidi Odds za kushinda?
Je kuna namna ya kucontrol kipato wanachopata hawa jamaa ili kujua kodi sahihi ya kulipa?

Je wanatambulika kisheria?Kiserikali?

Ikiwa mtu anamalalamiko kuhusu mashine hizo anamuona nani?

Hayo yote ni maswali muhimu sana ambayo tukiwa na majibu yake tutajua picha halisi ya hiki kinachoendelea
 
Hizo mashine zipo ila sasa ni maamuzi yako mi huwaga naziangalia na kupita pembeni. Kwa sababu utashinda elfu ishirini halafu utarudi tena una liwa elfu hamsini. Sijawahi muona mchina ana lazimisha mtu acheze ilo dude

Ndugu unaongelea uchumi wa mchezaji, kijana mtanzania anaeliwa hela kutokana na hulka ama uraibu wake wa kucheza kamari

Mtoa mada anazungumzia uchumi wa taifa, athari kwa taifa kwa kuwepo kwa kamari hizi za mchongo mchongo.

Vitu viwili tofauti. Japo kimoja ni sababu ya moja kwa moja ya nyingine.
 
Mbona pombe zina uzwa tu, cha m
Huu uzi umenifundisha kuwa Watanzania wa leo ni naive sana na ni don't care

Akija mchina, mhindi, mzungu au mgeni yeyote akaigeuza nchi na wananchi shamba la bibi wanaona sawa tu as long as kuna vibenefit vichache vichache

Kule China hakuna mgeni anayeweza kuinstall vimashine hivi uchwara mtaani akawa unakomba hela za wachina kisha akaachwa salama. Ila ujinga huu unafanyika Tanzania na raia wanaona it is OK

Ndugu unaongelea uchumi wa mchezaji, kijana mtanzania anaeliwa hela kutokana na hulka ama uraibu wake wa kucheza kamari

Mtoa mada anazungumzia uchumi wa taifa, athari kwa taifa kwa kuwepo kwa kamari hizi za mchongo mchongo.

Vitu viwili tofauti. Japo kimoja ni sababu ya moja kwa moja ya nyingine.
Biashara ya gambling ipo duniani kote sasa serikali ichukue vipi kodi ndio liwe swali, unalo jaribu kusema ni kwamba serikali ukusaidie kumlea mtoto wako.

Kucheza kamari ni maamuzi binafsi ni kama kunywa pombe. Serikqli iweke kodi kubwa labda ili watu wasi wekeze kwenye iyo biashara. Ila hata wewe ukiamua kula usiku ni ume gamble kwa sababu huna uhakika uta amka asubuhi. Gambling is part of life
 
Jana nilipita maeneo ya Kigamboni, nikaingia uchochoroni sehemu moja karibu na msikiti wa Feri upande wa Kigamboni nikaona mashine moja ya Kamari uchochoroni kabisa, katika kibanda kisicho na hadhi hata kidogo, kimefichwa ndanindani.

Mchina mmoja akaifungua, akatoa machenji kibao ya shilingi mia mbili mia mbili akaweka kwenye kitu kama kikapu akapeleka kwenye mzani wa kupimia zile chenji (Inaelekea njia ya kuzihesabu kwa kuwa ni nyingi sana wanazipima kwa kilo wanajua kuwa kilo fulani ni shilingi fulani).

Palepale kuna sehemu kuna vijana wanachukua hayo machenji wanaenda kuyauza kama chenji kwa watu wa daladala—Yaani wanatakatisha hizo pesa kwa mtindo huo.

Kinachonisikitisha Wachina wanatoka huko kwao wanakuja maelfu ya Kilometa, wanafanya biashara haramu freely kabisa katika ardhi yetu na serikali ipo, haifanyi lolote, uchumi unahujumiwa lakini serikali inang'aang'aa macho tu.

Haya mambo ya wachina kufanya hizi kamari serikali yetu inajua na ni miaka michache huko Morogoro walikamatwa Wachina wamehodhi maelfu kwa maelfu ya coins.

Hizi coins wanazozihodhi inapeleka kupungua katika mzunguuko na matokeo yake kuleta shida katika uchumi wa nchi.

Nakueleza ukweli haya mambo ambayo Wachina wanayafanya, ya kuvamia vyanzo vya maji na kulima, kukata magogo hovyo, kufanya kamari na kudisturb uchumi wahusika wanayajua, wanakula rushwa kisha wanakaa kimya!

Nakueleza Ukweli, huu ujinga ambao wachina wanafanya, huwezi kwenda China ukafanya ujinga kama huo nchini mwao, ni kwa sababu wana akili.

Mbona sisi tunakuwa kama Mazuzu, tunauza nchi very cheap. Why?

5273295F-2616-420A-BE86-5F11E6CCF3A6.jpeg
 
Kwa sababu walikuwa wanaendesha biashara ya kamali bila kufuata sheria!! Hata hao anaowasema Misile of The Nation ikithibitika wanaendesha isivyo halali, nao WANAPASWA KUKAMATWA!

Hawatakamatwa kwa sababu wanaendesha michezo ya kamali bali kuendesha michezo ya kamali bila kufuata sheria!
na hii kamari ya Kigamboni imefuata sheria ?
 
Kosa ni la wachina au ni wananchi wenu wenye iq ..... Ngoja niishie hapo.

Ila jaribu kuangalia TV au kusikiliza redio siku nzima,alafu hesabu matangazo au vipindi vya kubet/kamari ni vingapi kwa siku. Alafu niambie kwa mtu asiyekua na kazi rasmi,si anakua programmed kucheza hio michezo.?na bahati mbaya sisi wengi huwa tunazurura zurura mitaani na nyumbani,Lazima nitacheza tu...waChina hawana kosa Bali wametumia fursa,,akili zetu zingekuwa zinachaji kama za kwao tungekua mbali
 
Hatuwezi kuwazuia Wachina kufanya hizo biashara zako za kamari. Hizo mashine zenyewe zinalipiwa kodi ya maana pale bandarini.

Kipaumbele cha serikali ni kodi kwahiyo acha tukusanye kodi. Nawe kama una ganja unataka kuuza wewe tupe tu kodi yetu.

Kwenye sport betting ukishinda au kishindwa panakatwa kodi. Haya mamashine kodi inakatwa wapi?
 
Nimekwambia kodi ya haya mamashine ipo bandari ushuru wa kuingiza hizo mashine ni mkubwa sana.

Umeelewa?
 
Ukiwa na jamii ya watu wajinga, werevu watawatumia kujinufaisha.
Kama vijana wetu wasingekua wanacheza hii kamari, sidhani kama hii midude ingekuwepo.
 
Jana nilipita maeneo ya Kigamboni, nikaingia uchochoroni sehemu moja karibu na msikiti wa Feri upande wa Kigamboni nikaona mashine moja ya Kamari uchochoroni kabisa, katika kibanda kisicho na hadhi hata kidogo, kimefichwa ndanindani.

Mchina mmoja akaifungua, akatoa machenji kibao ya shilingi mia mbili mia mbili akaweka kwenye kitu kama kikapu akapeleka kwenye mzani wa kupimia zile chenji (Inaelekea njia ya kuzihesabu kwa kuwa ni nyingi sana wanazipima kwa kilo wanajua kuwa kilo fulani ni shilingi fulani).

Palepale kuna sehemu kuna vijana wanachukua hayo machenji wanaenda kuyauza kama chenji kwa watu wa daladala—Yaani wanatakatisha hizo pesa kwa mtindo huo.

Kinachonisikitisha Wachina wanatoka huko kwao wanakuja maelfu ya Kilometa, wanafanya biashara haramu freely kabisa katika ardhi yetu na serikali ipo, haifanyi lolote, uchumi unahujumiwa lakini serikali inang'aang'aa macho tu.

Haya mambo ya wachina kufanya hizi kamari serikali yetu inajua na ni miaka michache huko Morogoro walikamatwa Wachina wamehodhi maelfu kwa maelfu ya coins.

Hizi coins wanazozihodhi inapeleka kupungua katika mzunguuko na matokeo yake kuleta shida katika uchumi wa nchi.

Nakueleza ukweli haya mambo ambayo Wachina wanayafanya, ya kuvamia vyanzo vya maji na kulima, kukata magogo hovyo, kufanya kamari na kudisturb uchumi wahusika wanayajua, wanakula rushwa kisha wanakaa kimya!

Nakueleza Ukweli, huu ujinga ambao wachina wanafanya, huwezi kwenda China ukafanya ujinga kama huo nchini mwao, ni kwa sababu wana akili.

Mbona sisi tunakuwa kama Mazuzu, tunauza nchi very cheap. Why?
Pale Dodoma soko la ndugai yamejaa kibao utadhani nayo ni bidhaa. Yaani haya madude sasa hivi ni kila kona.
 
Toka zamani nchini Kamari ipo na ilikuwa controlled, ila siku hizi watu wanasimika vimashine vyao vya kamari uchochoroni kabisa mitaani wanawapiga walalahoi hela
Haya matendo ni disaster, sijui kwa nini watu wanachukulia easy
 
Yani bottom line is hakuna anae kupeleka pale ku gamble
 
Back
Top Bottom