Serikali ifanye operesheni ya mashine bubu za kamari mitaani, Wachina wanahujumu uchumi

Wewe ndiyo tatizo, Wala siyo betting. Pengine vijana wako wanacheza na wameliwa jana
Ile siyo betting unayoijua wewe, kwamba unaenda sehemu, unakuta ofisi, unaomba karatasi unajaza

Nilichokiona mimi ni vivending machine uchwara vimewekwa ndanindani kwenye mabanda karibu na mama ntilie wanapouzia chakula chao.. Wanakuja vijana na mia mbili mia mbili zao wanadumbukiza mle, wanaliwa, wanarudi tena. Kuna vijana wa Kibongo ndo wapo pale kama kusimamia mashine hizo, halafu Bosi mchina anakuja baadae kukusanya mihela yake aliyowakamua waswahili!

Ninaposema vimashine bubu ni mashine bubu kweli na location zinapowekwa ni chimbo kwenye mikusanyiko ya watu
 
Hizo mashine zipo ila sasa ni maamuzi yako mi huwaga naziangalia na kupita pembeni. Kwa sababu utashinda elfu ishirini halafu utarudi tena una liwa elfu hamsini. Sijawahi muona mchina ana lazimisha mtu acheze ilo dude
 
Mkuu mbina kama una chuki nao?kumchukua tajiri hakukupi unafuu wewe!!ninavyojua mimi hao wanaendesha biashara hiyo kwa kufuata sheria ziluzowekwa na bodi ya michezo ya kubahatisha nchini na kila machine ina namba ili kuzitambua idadi yake, na huwa zina kaguliwa na wao, ili kulipa kodi.eti kuuza change kwa watu wa daladala ni kutakatisha pesa?!!kwani hizo coins wanazotumia kwenye mashine hizo huwa wakifungua wana zila hadi useme kuwa zinapungua mtaani?mbona zinarudi tena mtaani?mbona zile milioni 200, zilizokamatwa kipindi kile huko morogoro warirudishiwa?!!
Na kwa taarifa yako sio wachins tu hata wazungu wanabiashara hiyo.wala usiwasingizie wachina eti ndio wanao disturb uchumi wetu,umeme wa kuunga unga, sera za kibabe na vitisho, uchumi utakuwaje imala hapo? Yule aliyelima kando ya mto nenda hata sasa kama humkuti akilima bado, vibali muwape nyie kosa liwe lake?
 
Acha kupotosha mkuu, hii biashara wana kila documents zinazotakiwa , na bodi ya michezo ya kubahatisha wana zikagua kila wakati!!kwani hao wafanya biashara wengine wa kigeni wanapopata pesa zao kama faida huwa wanazifanyia nini?!!
 
Hizo mashine zipo ila sasa ni maamuzi yako mi huwaga naziangalia na kupita pembeni. Kwa sababu utashinda elfu ishirini halafu utarudi tena una liwa elfu hamsini. Sijawahi muona mchina ana lazimisha mtu acheze ilo dude
Si watanzania wote wana uelewa kama wako.

Ni kama viroba, yalifanyika maamuzi ya busara ya kuvipiga marufuku licha ya kwamba unywaji wa viroba si kwamba watu walikuwa wanalazimishwa ila uamuzi wa kuvipiga marufuku tunaangalia faida pana kwa jamii
 
Acha kupotosha mkuu, hii biashara wana kila documents zinazotakiwa , na bodi ya michezo ya kubahatisha wana zikagua kila wakati!!kwani hao wafanya biashara wengine wa kigeni wanapopata pesa zao kama faida huwa wanazifanyia nini?!!
Yaani vimashine vile uchwara vya kuwaibia walalahoi pesa zao wewe unawaona ni wawekezaji? —Ndiyo maana hii nchi itaendelea kuwa shamba la bibi kwa sbabu ya watu wenye mentality ya aina hii

Kama hiyo biashara ni halali na haina tatizo kwa nini serikali za nchi zao zimezipiga marufuku hizo biashara kufanyika katika vichochoro vya mitaa yao?
 
Si watanzania wote wana uelewa kama wako.

Ni kama viroba, yalifanyika maamuzi ya busara ya kuvipiga marufuku licha ya kwamba unywaji wa viroba si kwamba watu walikuwa wanalazimishwa ila uamuzi wa kuvipiga marufuku tunaangalia faida pana kwa jamii
Zipo za kupima tena double kiki, ita rudi pale pale kila siku ni maamuzi binafsi. Serikali itakacho fanya ni kutoa elimu kukusanya kodi basi
 
Hapo BOLD na suala zima la michezo ya kamari holela sina tatizo, na wala sikubishii coz we all know hawa Wachina na ndo maana nimesema wazi kama kweli hilo jambo lina-exist, lazima serikali iingie front kwa sababu huo ni uhujumu wa uchumi!

Nilipotofautiana na wewe ni hicho kipengele cha kubadili change, hiyo haiwezi kuwa ground.
 
Kama msimamizi wa hayo maswala anakula per diem na mshahara mzuri kuna haja gani ya kujihangaisha na vitu vya kipuuzi
 
Je wajua?,
CHUKI HUUA AU HUWEZA KUSABABISHA KIFO?
 
Kama wewe ni concerned citizen ungechukua hatua ya kuripoti kwenye mamlaka husika ndiyo wange confirm legality ya hiyo biashara. Otherwise kuileta humu ni nginjera tu
 
Labda utupe nini maana ya uwekezaji kwanza?hapa kwetu kilimo cha mirungi ni halamu lakini nchi ngapi ni biashara nzuri tu na ni halali?uhalamu wa kitu ni wewe unavyouchukulia na sio kiwe halamu kwa kila mtu!!kamali karibu dunia nzima ipo, huo mtizamo ni wako eti vimashine uchwara, wakati serikali yako ndio inakopatia kodi, na kukufanya uvimbe!!ninachofahamu wale wako kisheria hapa nchini, na ndio maana ziko wazi kila sehemu zinaonekana.watanzania wananufaika na uwepo wake, mmoja mmoja na taifa zima.kwani hapa kwetu mbona karibia kila biashara inafanyika uchochoroni kwani masikini ndiko wanaishi na ndio wengi, na ndiko kwenye biashara nzuri!!!sasa masaki, ostabey kuna vichochoro, kule nenda kwenye makasino, ma bar utazikuta tu, za kiwango chao, sio dubu, ila bado ni kamali tu.
 
Inasikitisha sana...

Ukizingatia hao wachina kule kwao wametoka kama wafungwa...
 
Huu uzi umenifundisha kuwa Watanzania wa leo ni naive sana na ni don't care

Akija mchina, mhindi, mzungu au mgeni yeyote akaigeuza nchi na wananchi shamba la bibi wanaona sawa tu as long as kuna vibenefit vichache vichache

Kule China hakuna mgeni anayeweza kuinstall vimashine hivi uchwara mtaani akawa unakomba hela za wachina kisha akaachwa salama. Ila ujinga huu unafanyika Tanzania na raia wanaona it is OK
 
Nchi ambayo Twiga wanapanda ndege kuna kinachoshindikana??
 
Naunga mkono hoja for 100%, wanapiga Sana pesa na kuwafilisi wazawa ,viko vingi vimashine vyao ,itungwe SHERIA , serikali inakosa mapato
 
Unajua selikali inawakamua kodi kiasi gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…