Serikali ifanye operesheni ya mashine bubu za kamari mitaani, Wachina wanahujumu uchumi

Kwani wamelazimishwa au wameshikiwa bunduki kucheza hayo makamali si ujinga wao
Wananchi wana haki ya kulindwa dhidi ya adui ujinga- Ndiyo maana wewe ulipelekwa shule kwa kodi za wananchi si tu ili ujinufaishe wewe peke yako na familia yako bali unufaishe Taifa zima hasa pindi ukiwa na nafasi ya maamuzi serikalini
 
Nimekubali mkuu yaishe na nimekuelewa
 
Pamoja na idara husika kufanya kazi zao bado kuna nyufa nyingi katika kusimamia misingi na sheria za kazi. Kuna mahali tumekosea. Raia wa kigeni wako huru sana kufanya watakavyo. Wanakuja nchini kufanya shughuli za umachinga na unaweza kukuta bila leseni hata vibali vya kuishi nchini na hawaguswi. Sina hakika lakini nahisi tumerelax mno kiasi wageni wanafanya shughuli za ajabu lakini zikiwaingizia pesa bila kubugudhiwa!
 
Nchi yetu imezidi kuwa shamba la Bibi hayo madude ya mia 2 2 saizi wanawapa hata wenye maduka ya kimangi mangi.......muda mwingine unaichukia hadi serikali kwanini wanaruhusu huu upuuzi? Gambling inabidi iwe sehemu maalum......ila kwetu hapa kuanzia media matangazo ni kamari tu mwanzo mwisho.....sijui tunatengeneza kizazi Gani
 
Biashara hii ilipaswa kufanywa na Watanzania wenyewe sio wachina, Wachina walipaswa kusupply tu haya madubwana kwa wazawa then biashara ifanywe na wazawa...
 
Ujinga haufanywi na wachina, unafanywa na unao ogopa kuwataja. Mfumo wa utawala Tanzania upo kuanzia mitaani, na CCM wana mpaka mabalozi. Kuna kamati za ulinzi na usalama za Kata, zina wajumbe toka kila Mtaa. Machine ulio iona yaweza kuwa kwenye nyumba ya kiongozi, kazi iendelee.
 
Karibu 20 ya pesa za nchi hii wanaziiba wachina kupitia haya madubu.
Unaweza usiamini hili lakini jitahidi tu niamini Mimi.
Uswahilini pato karibu lote linachukuliwa na Wachina kupitia haya madubwi
Na usisahau na betting, ndio ndoto ya kutajirika kwa vijana wa leo. Serikali inaweza kuwa inapata mgao wake, vijana wanatumiwa. Wakifirisiwa na hiyo michezo wanaokwenda kuwakaba na kuwa yes wazazi.
 
Baadhi ya viongozi wahusika wakishafinyiwa fungu hawaangaiki tena.
 
Nakueleza Ukweli, huu ujinga ambao wachina wanafanya, huwezi kwenda China ukafanya ujinga kama huo nchini mwao, ni kwa sababu wana akili.

Mbona sisi tunakuwa kama Mazuzu, tunauza nchi very cheap. Why?
 
Wananchi wana haki ya kulindwa dhidi ya adui ujinga- Ndiyo maana wewe ulipelekwa shule kwa kodi za wananchi si tu ili ujinufaishe wewe peke yako na familia yako bali unufaishe Taifa zima hasa pindi ukiwa na nafasi ya maamuzi serikalini
Na mimi niliesoma private tangu kindergarten Nina Deni?!
 
Kule Moshi Wachina wamenyosha mikono juu na hizo machine zao, Wachagga washajua jinsi ya kudili nazo.
Sh.200 ikiikata na msumeno kidogo unaponda chuma nyembemba ndefu kama futi moja hivi unaibania pale ilipokata alafu unawekea ribiti na ile wire ya aluminiam(kama ile wanayowekea viraka masufuria) ukiienda pale kwenye mashine unaingiza hiyo 200 ila haidumbukii maana ule wire ndio unaishikilia ikigusa pale ndani kwenye ringi basi unacheza mpaka unazimaliza huko zote.[emoji13][emoji13][emoji13]
 
Hamna kitu kama icho njia ya kutoa ela kwenye bonanza ni kulivunja
 
Biashara hii ilipaswa kufanywa na Watanzania wenyewe sio wachina, Wachina walipaswa kusupply tu haya madubwana kwa wazawa then biashara ifanywe na wazawa...
Hicho ndio kinafanyika mchina haleti dubu bila utaratibu, mzawa unatafuta eneo, kuna gharama unalipa za dubu, mchina anakuletea kuna kiwango mchina cha kwake kila week anakuja kuchukua kikizidi ni pesa yako.
 
Nchi hii vijana wanataka pesa rahisi, wanataka kuvuna pesa bila kuumiza sana akili na mwili, wachina wameliona hilo na wanalifanyia kazi.

Vivyo hivyo kwa viongozi wetu, wazungu wamewajua viongozi wetu ni wala rushwa, wapenda madaraka na pesa nyingi, pia wananufaika na hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…