Bunge kimekuwa butu kuisimamia na kumwajibisha serikali.limekuwa bunge la chochote Cha serikali ni ndiyooooooo.Ameharibuje?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bunge kimekuwa butu kuisimamia na kumwajibisha serikali.limekuwa bunge la chochote Cha serikali ni ndiyooooooo.Ameharibuje?
Betina anafikiri ataishi milele.Kuongeza ulinzi Kwa tulia mwansasua ambaye ameharibu bunge letu ni matumizi mabaya ya fedha za umma
EheeeeRais wetu Mpendwa aliagiza uchunguzi ufanyike.
Elezea kwa kina au unafikiri kila mtu ni chawa mkuu?Kama siyo CCM usingeweza kuingia hata hapa jukwaani
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Huna akili mbuzi wewe. Uchawa umekukaa hadi makalioni. Unawaza ujinga muda wote
Ulinzi WA Nini?Kuongeza ulinzi Kwa tulia mwansasua ambaye ameharibu bunge letu ni matumizi mabaya ya fedha za umma
Watu wazuri hawafiHalafu wanakufa wa imani moja tu!
Kwani wewe ndg Lucas huamini kwamba kuna kifo?Kwani wewe unajua kulichomuua? Uchunguzi si ndio utabaini kwa undani kulichomuua? Kwani wewe hofu yako ni nini uchunguzi ukifanyika?
Serekali ya kihalifu ichunguze kifo cha utata wakati wao wenyewe wameshawatanguliza kina Soka, Ali Kibao ahera?Ndugu zangu Watanzania,
Ifike mahali kama Taifa tusikubali kila kifo kipite hivi hivi au kuacha mambo yaende hivihivi kana kwamba hakuna kilichotokea vile au kusema ni Mapenzi ya Mungu au kuona ni kawaida.Mungu ametupatia akili kwa ajili ya kufikiri na kufanya tafakari kwa msaada wake Mungu Mwenyewe.
Ikumbukwe hii ni Dunia yenye vita vya kila aina ikiwepo kuhujumiana,kudhoofishana na kumalizana kwa kila mbinu .ambavyo vinakuwa vinafanywa kwa akili na maarifa ya hali ya juu sana na kufanywa na watu wenye akili za hali ya juu sana na ambao wapo kwa ajili ya kazi hiyo tu na wamefundishwa na kuivishwa kisawasawa.
Ifahamike kuwa wakati Mwingine kama Taifa linaweza kumalizwa na kutafunwa kama ugonjwa wa kansa kwa kumalizwa viongozi wake hasa wale wenye maono,akili kubwa,upeo,maarifa na ufahamu mkubwa wa masuala mbalimbali.watu wanaweza wakawa wanamaliza viongozi na watu wako muhimu pasipo wewe kujua .unapokuja kushituka ni wakati huna uwezo wa kusimama tena kukabiliana na hujuma hizo kwa sababu unakuwa tayari umepoteza watu wote wale wa muhimu.
Hivyo ni muhimu sana tuanze utaratibu wa kufanya uchunguzi wa vifo vya watu wa muhimu au viongozi pale inapotokea vifo vya ghafla na vyenye kutatanisha ili kuweza kujua ni vifo vya Mungu au vyenye mikono ya Binadamu. Kumbukeni hapa Majuzi tu tumepoteza kiongozi mashuhuri na muhimu sana hapa Nchi ambaye ni Mafuru.na sasa tumempoteza mwingine mtu wa muhimu sana kwa Taifa letu Dkt Faustine Ndugulile.
Lakini tujiulize huko India tumepeleka viongozi wetu wangapi katika kumbukumbu zetu na wangapi wamepoteza Maisha. Ni wakati wa kufumbua macho sasa kama Taifa kwa idara zetu za Ujasusi ndani na nje ya Nchi katika ulinzi wa viongozi wetu muhimu na watu muhimu.maana kuhujumiwa unaweza kuhujumiwa kwa njia mbalimbali ikiwepo hata wafanyabiashara wako wakubwa na wenye mitaji mikubwa na wenye mchango mkubwa kwa Taifa kupotezwa.
Lakini ni wakati pia wa kumuangalia Dkt Tulia kwa jicho la kijasusi zaidi kwa kujua kuwa anawakilisha Taifa letu huko Nje ya Nchi.hivyo ni Muhimu kumuongezea ulinzi zaidi awapo ndani na nje ya Nchi.Maana ikumbukwe ya kuwa hata katika kugombea hakugombea peke yake na hivyo siyo kila mmoja anapenda kuona Taifa fulani likiwa linang'ara katika nafasi za kimataifa kama ambavyo ilikuwa tumepata kwa Dkt Faustine Ndugulile kuongoza WHO kanda ya Afrika pamoja na kuwa na Dkt Tulia upande wa IPU.
Kwa hiyo kwa nafasi ambazo watanzania wanapata kuongoza taasisi za kimataifa tuhakikishe tunaongeza ulinzi ikiwepo kwa yule ambaye yupo kwenye masuala ya Fedha. Tukilala unaweza shangaa unafanyiwa hujuma na kupigwa mapigo makubwa makubwa mahali panapouma na kuacha majeraha,mapengo na alama zisizofutika wala kuzibika.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Kweli kabisa in kizimkaz's voiceUlinzi WA Nini?
Kifo ni kifo tu
Kifo kipo na kila kifo kina sababu yake.Kwani wewe ndg Lucas huamini kwamba kuna kifo?
Wewe nyumbani kwenu hujawahi kufiwa? Kama ulishawahi , je ulisha ita uchunguzi wowote ufanyike?Kifo kipo na kila kifo kina sababu yake.
Soma andiko langu uelewe na siyo kukurupukaWewe nyumbani kwenu hujawahi kufiwa? Kama ulishawahi , je ulisha ita uchunguzi wowote ufanyike?
Mimi ni mkulima na kilimo ndio kazi yangu.Aliyekurupuka ni wewe! Lakini bwana Lucas kwenye hii dunia ogopa sana kuwa mtumwa wa mtu mwingine kwa lengo la kujipatia kipato. Njia sahihi ya kujipatia kipato ni kufanya kazi kwa bidii, hata ukipata kidogo utaishi kwa amani na upendo kuliko maisha ya kujipendekeza kwa viongozi . Unajua kwa akili zako unaweza kumchomesha ndugu yako kwa lengo lakupata kipato??
Soma andiko uelewe ewe mkurupukajiKWa hiyo ndugu Popoma unataka kutuambia CCM mmeanza kushenyentana wenyewe kwa wenyewe siyo hadi muanze kupeana ulinzi maalum.
Wewe ndiye huna maana uliyejaa roho mbaya na mawazo ya kishetaniKwa tulia lolote litokee hana maana