Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Sera zinazosimamia masuala ya usalama barabarani zimeweka Sheria na kanuni za kufuatwa.
Uendeshaji magari ya abiria una Sheria na kanuni zake. Mojawapo ni dereva wa Magari ya abiria anatakiwa awe na utimamu wa mwili na akili wakati wote aendeshapo magari.
Nilikuwa naongea na dereva mmoja wa mabasi, akaniambia jambo la kushangaza sana.
Akasema madereva wengi wanaoendesha magari yanayokwenda safari za chini ya kilomita 600, hulazimishwa kufanya safari za kwenda na kurudi.
Akasema kwa mfano dereva anaondoka Dar es salaam saa nne asubuhi, akifika Iringa kuanzia saa 12 jioni au Moja jioni, hutakiwa kugeuza kurudi Dar es salaam saa 2.30 au 3.00 usiku.
Dereva huyo akaniambia kuwa matokeo yake madereva wengi wa mabasi hutumia mirungi ili iwafanye wasilale wakati wa usiku.
Kuna wakati baadhi yao wakikamatwa wamiliki wa mabasi hupiga simu ili mabasi hayo yaendelee na safari.
Halijatokea tatizo kubwa la ajali. Lakini Serikali isije kusema kuwa hatujawaambia.