Serikali iingilie kati au kuja na mbinu kuzuia kuvuja kwa pesa kwenye mzunguko wa uchumi

Serikali iingilie kati au kuja na mbinu kuzuia kuvuja kwa pesa kwenye mzunguko wa uchumi

ngebo

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2017
Posts
1,684
Reaction score
2,126
Angalizo ; huu uzi hauna maana mbaya wala kupangia watu namna ya kutumia pesa zao..!!!

Tanzania tumeingia kipindi ambacho tunaona magari mengi sana ya kifahari, ukiwa barabarani sasa hivi kupishana na gari za 500M or less ni kitu cha kawaida, waTanzania wengi sasa wakipata pesa tumeingia na kasumba ya kuona kuwa na ndinga kali ndio priority, ila naona hatuangalii kwenye long-run namna inavyogusa uchumi wetu kwa namna isiyo chanya. Kwa tuliosoma Uchumi, tunafahamu kitu kinaitwa (Leakages in the Economy Cycle) kwamba kwenye mzunguko wa fedha kuna vitu viwili, leakages yaani kuvuja na Injection yaani vitu vinavyo ongeza kipato ama pesa kwenye uchumi wetu mfano uwekezaji wa makampuni, kuuza mazao yetu nje ya nchi yani Exports nk..., sasa hili jambo la kuagiza sana hususan tugusie magari ni leakage kwenye uchumi wetu na limekua kwa kasi sana kwa hiki kipindi cha miaka mitatu hadi minne iliyopita. Serikali ni kweli kupitia vyombo vyake wameweka kodi ya juu kwenye importation ya hivi vitu ila bado haibalance pesa iliyotoka nje, mfano nikinunua gari ya million 200, kodi ya hiyo gari hata ikiwa million 100 bado hairejeshi ile million 200 iliyotoka kwenye mzunguko.. Tuweke akilini kuagiza magari inabidi utumie Dollar na tulikuwa mashahidi namna Dollar kipindi cha nyuma ilivyokua mtihani.. Tukilinganisha hali ya kimaisha kipindi cha JK pesa ilikua mkononi maana hata nagari ilikua nadra kuona watu wanasukuma gari za kifahari, yaani gari za namna hiyo ilikua ni shangingi ama Range na Benz or BMW chache, magari mengi sana yalikua Toyota za bei ya chini mfano balloon, corona, carina etc basi kwa maana hiyo pesa nyingi haikutoka nchini na pia magari hayakua mengi ila sasa spidi ipo juu sana, na sio jambo baya ni ishara watu wana vipato ila inabidi tutafute njia bora ya kuregulate hili jambo kwa kuwa linagusa uchumi wetu.

Nini cha kufanya ;
-Serikali ijaribu kufanya mchakato tupate viwanda hata vya kuassemble magari, mfano hai ni South Africa wana viwanda vya kuassemble magari toka mwaka 1924 mfano wana viwanda vya Volkswagen, BMW, Ford, Nissan, Toyota nk.. hivyo wanaepuka kutoa pesa yao kwenye mzunguko ndio maana magari kule bei ni rafiki, bei niliyonunulia IST kwa kule ningepata BMW safi kabisa, pia hivyo viwanda achilia mbali kuokoa gharama za importing magari pia zinatoa ajira hivyo itasaidia swala la ajira linalotesa sisi vijana nchini...

-Elimu itolewe ya namna nzuri ya matumizi, makazini kama mnavyofahamu kuna mikopo hutolewa kwa waajiriwa permanent, mimi ni shahidi nina watu nawafahamu walichukua mikopo ya hadi million 30 na wakaishia kununua ndinga ikiwa hata kiwanja cha million 10 hana wala savings ... mnafahamu pressure za mjini, gari kwanza kama tunavyosema vijana, ni sawa ni jambo jema ila gari ni liability vijana tupewe elimu juu ya hiyo mikopo, wazee wetu walianzisha biashara, kununua viwanja nk kwa hiyo mikopo tujitahidi kubakiza pesa kwenye mzunguko tukuze uchumi wetu

- Serikali iwekeze zaidi kwenye usafiri wa Umma (Public Transport) .. tunaona kwenye nchi developed usafiri wa umma upo level za juu sana mfano watu wana commute kutoka majumbani kwenda kazini na zile train zinafika hadi speed ya 70mph ama 112 kph, serikali ingekuja na hizi option mfano mtu kutoka bunju kwenda mjini ni kitu cha 20 mins max umefika, ingeokoa sana adha ya foleni mijini kwani kukiwa na usafiri mzuri spacious watu wengi wata opt hilo zaidi ama kwa watu wa maritime waangalie labda kuleta cruise ships ziwe zinapita maeneo yenye bahari jijini ingawa sio wote watatumia ila kama inawezekana pia itaokoa muda na kupunguza foleni na overload ya daladala nk...

-Pia serikali iendelee kuboost na kusupport wakulima na sector mfano ya madini na nishati ili exports ziongezeke tupate fedha ya kigeni..

Ni hayo tu members, kwa waliochukulia in a negative way hili andiko mniwie radhi
 
Umeongea vizuri, kwa sasa gari za bei mbaya kila kona vijana bado hatuna aidha elimu ya kuinvest mindset ni za kutumia tu.
 
Back
Top Bottom