Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah huu ndio ukweli. Bora ukafie Dubai kuliko kufia Gongolamboto.Yote haya yanaanza na sera mbaya za kiuchumi nyumbani zinazofanya watu wakahangaike nje.
Huo ndiyo mzizi wa fitina.
Kama nyumbani kungekuwa na nafasi nzuri nyingi za watu kufanya kazi na kutumia vipaji vyao, sifikiri kama watu wangeondoka kwa mafungu hivyo.
Sasa hivi ukianzisha kibiashara kidogo tu, utapigwa kodi na TRA mpaka ujute, kabla hata biashara haijaanza.
Ukisema uanzishe ki Youtube channel uangalie mingo mtandaoni ndiyo kabisa, unaanza kutozwa hela kabla hata hujaingiza.
Ajira za sekta rasmi chache na zinaenda kwa kujuana.
Kwa nini watu wasione bora wakajaribu maisha nje huko. Nako wanakutana na dhahama hizi.
Hivi kuna wanaoondoka Tanzania kwa kujua kuwa wanakwenda kuwa makahaba?
suala la mabint kupenda kwenda Arabuni mm napendekeza serikali isijishughulishe nalo kabisa sababu wanajitakia, kila siku matatizo ni nchi za kiarabu dhidi ya wadada wa tz na yanaripotiwa lakini bado wanaendelea kwenda kwa wingi,,,, wapambane na hali zao.
Kama ni mfanyakazi wa shirika kubwa na amepangiwa apartment kampuni ndio inamlipia kila kitu je?🤔
Mimi ninaona tatizo moja kubwa ni kutegemea viongozi kutatua matatizo.Shida atujapata bado kiongozi sahihi atakaeshuka chini na kuishi maisha ya watz, Bado kuna fursa nyingi Sana hazijatumika kwenye raslimali zetu Kama zingetumika vizuri kimkakati zingemaliza tatizo la ajira nchini.
NAKAZIA.Mi siwalaumu hao Waarabu/Waturuki/Wahindi na Wazungu. Nawalaumu hao mnao waita dada zetu, kina wawasha nini kwenda huko? Kwanini wasitulize misambwanda yao huku huku tujenge nchi yetu?
Nimekuelewa mkuu dah!Tatizo sio kupangiwa, tatizo linaanzia wanawake wa kibongo wanapenda sana mteremko na Starehe. na ndio mana wengi wao wanagongwa kirahisi sana.
Anaweza kuwa accommodation anapata kwa kampuni, lakini watu wakawa wanasimamia gharama za starehe, night clubs, pombe, mavazi ambazo yeye kama yeye ni ngumu kuweza kujichia nazo. mana starehe gharama na Zaidi nchi za wenzetu.
Siku wananchi wakipewa uwezo wa kuamua vipaumbele na mambo yao juu mbona umasikini utapotea ndani ya miaka 10.Mimi ninaona tatizo moja kubwa ni kutegemea viongozi kutatua matatizo.
Utatuzi wa matatizo unatakiwa kuanzia kwa wananchi, viongozi wanatakiwa kupewa ajenda na wananchi, kwa sababu wale ni vijakazi wa wananchi tu.
Ukiwa na nchi ambayo wananchi, ama kwa kukosa elimu, ama kwa kukosa muamko ama kwa kukata tamaa, hawachukui ownership ya mambo, na wanategemea kiongozi Messiah type aje kutatua matatizo yao, uwezekano wa kutatua matatizo unakuwa mdogo.
Kwa sababu kiongozi, au viongozi ni wachache, hawawezi kuwa na uwezo wa kuona mengi kama wananchi wengi. We have to crowdsource problem solving, with inclusivity, diversity and complementarity.
Pia, viongozi wanachoka.There is such a thing as development fatigue.Mwishowe wanaamua kujiweka vizuri wao, familia zao na rafiki zao wachache, wakisema huu umasikini ulikuwepo, upo na utakuwepo tu, siwezi kuumaliza mimi.
Viongozi wanatakiwa kupewa ajenda na kushurutishwa kuifuata. Nguvu ya umma iwashurutishe.
Hongera wewe unalala nae, unaamka nae ugaibuni😭😭[emoji2958][emoji2958][emoji6][emoji854]