Serikali iingilie kati watanzania wafanyakazi wanaofilisi makampuni sekta binafsi

Kuna jamaa alikuwa anaelezea uhusiano wa serikali na wafanyakazi wake.

Akasema serikali inadanganya kuwa inawalipa wafanyakazi wake mishahara, na wafanyakazi wanadanganya kwamba wanafanya kazi.
Kaka hii analog iwekwe notes board. Aloooo haki ni mbaya na ndicho kinachoendelea 🤣
 
Umelisoma vizuri jina la kampuni hiyo, jina tu linajieleza ni kampuni ya aina gani na akina nani, eti el chapo! Wacha wafunge, mwenye kampuni ameifilisi kampuni yake wewe unatska serikali ambayo inafilisiwa kampuni zake bila kuchukua hatua imkamate huyo chapo kwa kuifilisi kampuni yake! Utasubiri sana.
 
Ni kubwa mno na serikali isipoingilia kati investors wataacha kuja hii nchi tutabaki wenyewe na wataoinvest ni watu wanaoweza kubanana na sisi tu, wahindi wakenya wanigeria ambao wamezoea kufanya matukio ukiiba unapotezwa kwa ramani.
 
Tumia akili basi nenda kwa hiyo post ukasome comments utaelewa
 
Umelisoma vizuri jina la kampuni hiyo, jina tu linajieleza ni kampuni ya aina gani na akina nani, eti el chapo! Wacha wafunge, mwenye kampuni ameifilisi kampuni yake wewe unatska serikali ambayo inafilisiwa kampuni zake bila kuchukua hatua imkamate huyo chapo kwa kuifilisi kampuni yake! Utasubiri sana.
 
Wakiboresha maslahi ya wafanyakazi wao + mikataba mizuri + mazingira mazuri sehemu ya kazi = hawatoibiwa
Mtanzania ataiba tu, We anagalia serikarini watu wanavojichotea mipesa wakati wana mishahara minono na posho nzuri
 
Mtanzania hata umboreshee masirahi atakuibia tu
Huu ndio ukweli watu hawataki kuupokea, wizi hauhusiana na maslahi, wizi ni wizi. Tatixo la wizi ni kubwa mnoo! Yani kampuni inayodhamini ligi kuu inaibiwa mpaka wanafunga kabisa inatisha! Nani ataweka pesa hii nchi? Nchi zingine serikali inakumbembeleza usifunge Tanzania watu wanaona kawaida. Investor gani atakuja kuweka pesa hapa?
 
Reactions: Cyb
Ni kubwa mno na serikali isipoingilia kati investors wataacha kuja hii nchi tutabaki wenyewe na wataoinvest ni watu wanaoweza kubanana na sisi tu, wahindi wakenya wanigeria ambao wamezoea kufanya matukio ukiiba unapotezwa kwa ramani.
Watu wanaibia mpaka NGO za kusaidia wakulima.

Mwaka 2004 nilikuwa kazini New York. Nikawa napitia mitandao ya jamii ya Kitanzania. Nafikiri siku zile ilikuwa Young Africans.

Basi nikakutana na story kuna mchungaji mmoja wa Kimarekani analalamika kapigwa mizigo yake ya kwenda kusaidia wakulima huko Tanzania. Nikasikitika sana. Nikasema nitamsaidiaje huyu mtu? Mtu aliyeamua kusaidia wakulima wetu hatakiwi kupata matatizo hivi bila kusaidiwa. Nikasema mimi kwa kuwa nawajua wale ma top dog wazee wa bandari, nitamuunganisha huyu juu kabisa huku chini wasimzingue.

Nikam contact mshua mmoja top dog wa bandari. Akaniomba details za mzigo na contacts za huyo mchungaji wa Kimarekani. Nikampa contacts.

Baada ya muda nikaja kufuatilia yule mshua aliniambia amekutana na yule mchungaji, na mzigo wake ulipatikana kabla wajanja hawajaupoteza mazima.

Nikasema wabongo nuksi, wametaka kumpiga mpaka mchungaji wa watu anayesaidia wakulima.
 
Sasa aibu gani hii! Aise ulifanya kitu cha kizalendo masta !!!
 
Kila kitu serikali serikali ndio maana akili zinadumaa, Serikali ina mhimili wa mahakama, ambao kazi yake ndio ku deal na hizo issue hapo unataka serikali iafnye nini tena???
 
Na hizi taasisi za serikali ambazo wanalipwa mabilioni sbaabu ni nini kwajili ya wizi, usihalalishe wizi
Tuzungumzie sekta binafsi sababu ndio lengo la kuletwa hii mada
 
huzuni ni kuwa! wewe hujui na kibaya zaidi haujui kuwa hujui. hao wanakwepa KODI kwa kisingizio kuwa hakuna faida kwenye uwekezaji walioufanya, wanabaki kusingizia wafanyakazi. ndio hawa hawa kina BIG nyassh!(imechanganywa kwa mat*ko) na wenzao kadhaa wanaojifanya kuwa kampuni imepata hasara/kufilisika ama kufungwa/kuhama kabisa huku wakiwadhalilisha na kuwalipa UJIRA kidogo wafanyakazi wao.
 
Wanaiga kwa viongozi wao wanaonunua maV8 kila siku na kujenga maghorofa.

Mfumo wa nchi umeruhusu wizi kuwa sehemu ya maisha na sio kuset mfumo bora wa maisha unaoruhusu mtu kufanikiwa bila kuwa mwizi.
 
Na hizi taasisi za serikali ambazo wanalipwa mabilioni sbaabu ni nini kwajili ya wizi, usihalalishe wizi
Lakini mada yako si umeileta ukilenga sekta binafsi.? Tuishi humo, hao serikali kila siku wanajadiliwa na hakuna kipya
 
Mimi mfanyabiashara mkuu, gharama yaku declare bankrupt na kufunga kampuni haina manufaa kwako labda uuze kampuni kabla haijafilisika na hamna kitu kigumu kama kuuza kampuni yenye madeni. Haina mantiki mtu kuiacha kampuni ife aende soko lingine. Hukopesheki popote tena, mpaka mtu kafunga kampuni sio utani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…