Harusi ni sherehe,
Sherehe ni STAREHE.
SERIKALI haiwezi kuingilia Sherehe au STAREHE za watu.
Serikali inaweza ingalia ndoa lakini sio harusi.
Serikali haipangagi masuala ya ANASA au STAREHE za watu wake.
Ndio maana huwezi sikia serikali ikiingilia bei ya pombe au sigara Kwa maana ni STAREHE hizo ambazo mtu anaweza kuifanya au asifanye.
Ila serikali inaweza ingilia vitu basic na lazima Kama vile maji, Mafuta, umeme, vocha(bando) Kwa maana hizo ni muhimu na basic.
Kuiingiza serikali kwenye STAREHE zako ni ukosefu wa Akili.
Ni Sawa na masuala ya Hoteli, au Lodge, au Guesthouse,
Au masuala ya kwenda Disco au kuangalia Wasanii.
Msanii anauwezo WA kukuambia kiingilio milioni moja l. Sasa wewe utajipima Kama unauwezo huo au laa, pia utaangalia huyo msanii anatoa Huduma ya viwango hivyo au ni geresha tuu.
Usitake kila kitu serikali ikufanyie hasa mambo ya ANASA.
Harusi sio lazima.
Ndoa ndio lazima.