Naona watu wapo busy kutaka file la namna JPM alivyokufa lifutwe. Sasa litafutwaje kwa mfano.
Rais kututangazia kwamba kilichomuua JPM ni tatizo la mfumo wa moyo lilomsumbua kwa zaidi ya miaka 10, haiondoi nadharia kwamba inawezekana kuna mkono wa mtu/watu waliotumia hilo tatizo la moyo kuharakisha kifo chake. Yote katika yote ni kwamba lazima udadisi ufanyike, za kuambiwa changanya na za kwetu.
Huyu hakuwa tu JPM, huyu alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyeifanyia makubwa nchi yetu. Kuzika tu na kusahau ni hatari kwa usalama wa viongozi wetu wajao, iwapo kifo cha JPM kitaachwa juu juu tu.