mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,925
- 51,688
- Thread starter
- #21
Simba ni timu kubwa walitakuwa kuwa na uwanja wao kama ule au kuzidi ule.Pale Mwenge ni eneo zuri kuweka uwanja shida uwanja ni mdogo. Mimi mwenyewe natakaga sana kwenda kucheki mechi ili nikifikiria usumbufu wa kufika kwa Mkapa au Chamazi naghairi, ila pale Mwenge chap tu.
Wakati wa ujenzi au design, Manispaa kama haikuwa na pesa za kutosha ingetafuta wadau ikiwemo Simba ingeongeza eneo pale kabla ya ujenzi wa uwanja huu ili kupata majukwaa makubwa zaidi. Ona leo watu kibao wamesimama. Hii haipendezi. Ina maana unaweza kununua tiketi ukakosa pa kupaa ukizingatia uwanja hauna siti una mabenchi ya mbao kwa hiyo capacity yake ni ya kukadiria.
Pale mwenge ni prime area,kumfidia mtu kiwanja chake haipungui milioni 400.
Kwa size ya timu ya KMC ule uwanja unawatosha,hawana fanbase kubwa kihivyo