A
Anonymous
Guest
Baada ya kukamilisha mambo yangu nikakaa kijiweni na Vijana wa eneo hilo kujua mbili tatu za eneo hilo.
Katika storI za hapa na pale akapita kijana mmoja ambaye alionekana kumfokea mzee mmoja, nikauliza kulikoni mbona 'dogo' anakosa adabu.
Nikaambiwa bwana huyo ni Mwalimu flani (akamtaja kwa jina la kwanza - Frank) huyo bwana hachezewi hakuna anayemgusa. Ilibid nidadisi zaidi kwani ana ishu gani. Ndipo wakanipa kisanga kizima.
Soma Pia: Mwalimu huyu wa Shule ya Msingi Mungu Maji aangaliwe, ananyanyasa Wanafunzi
Watoto wanashika nondo juu kwenye dirisha ndio wanachapwa, kutandikwa huko sio kwenye makalio tu. Fimbo zinachapwa mgongoni miguuni hadi kichwani, sio fimbo tu anatumia hadi mateke na ngumi. Vipigo hivi ni wasichana na wavulana.
Nikaelezwa kuwa Watoto wengi wameacha shule kwa kuhofia kipigo cha kinyama cha mwalimu huyo pindi wanapokosea. Baadhi ya Wazazi hawana budi kukubali watoto kubaki nyumbani kwani wanahofia pia wanaweza kuumizwa vibaya kwasababu ilishawahi kutokea mtoto mmoja ambaye angemaliza la saba mwaka huu (2024) alichapwa na Mwalimu huyo baadaye akaanza kulalamika maumivu ya tumbo na wiki moja baadaye alipoteza maisha, so haikujulikana wazi kama chanzo ni mwalimu au alikuwa na changamoto zake nyingine.
Wakazidi kunieleza kuwa kuna Wazazi wawili walikwenda kumhoji kwa nini anawatesa watoto wao nasikia yalitokea mabishano na mama huyo wakashikana na mwalimu kupigana. Mama mwingine yeye aliwashwa kibao hakuthubutu tena kuuliza chochote.
Naiomba Serikali imchukulie hatua mwalimu huyu kwani anawakatili watoto sio kwa kipigo cha kinyama bali pia kukosa haki yao.ya msingi ya kupata.elimu. Pili anawanyanyasa wanakijiji hiko yy amekuwa mungumtu.
Tanzania yetu ni nchi ya Amani mtu mmoja anawezaj3 kunyanyasa watoto na wazazi wao kwnye ardhi yao?
NAOMBA SERIKALI IMSHUGHULIKIE MTU HUYU HARAKA.
Tamko la Serikali ~ DC wa Ikungi: Tunachunguza tuhuma za Mwalimu wa Shule ya Mandimu (Singida) anayedaiwa kudhalilisha Wanafunzi