Tumwesige senior
JF-Expert Member
- Jan 28, 2013
- 3,506
- 6,305
Huyo mwalimu kama akampiga mwanangu kwa staili hiyo,ndo mjue vita ya nne ya dunia imeanza rasmi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inaonekana hujawasoma vizuri watanzania wa miaka hii, hawana muda wa kufuatilia kabisa mambo ya msingi kwenye jamii wanazoishi Wako bize na mambo ya kipuuzi tuu kama mipira, kubeti/mabonanza, ulabu, mademu etc...unaweza kukuta ulivyoambiwa ni kweli kabisa but they don't have time,pamoja na kuwa na kamati ya shule.Siamini kama ulimwengu wa leo kuna Mwalimu anaweza kuwa jeuri kiasi hiki na akaendelea na maisha kama kawaida.
Yaani hicho kijiji hakuna hata mwanaume mmoja wa kumshughulikia ipasavyo ili ajifunze kwamba ualimu wake sio chochote kwenye jamii ya watu waliostarabika.
Binafsi hakuna kitu ninachochukizwa kama ukatili dhidi ya mtoto aise suala hilo huwa nalibeba mwenyewe kwenye vyombo vya sheria.
Sheria ya mtoto inamlinda mtoto vizuri sana tena ushahidi wa mtoto hauhitaji uwe mzito bali akithibitisha tu anafanyiwa ukatili basi mtuhumiwa atakumbana na adhabu kali sana.
Kazi nzuri, lakini Kwa nini usitumie pia taaluma yako kupambana na wabadhirifu wa mali za umma ambao wamekuwa wakibainishwa na CAG kwenye ripoti zake za kila mwaka?Mkuu kwenye utetezi wa haki za watoto huwa sina mzaha kuna walimu kadhaa wa sekondari na msingi wametema bungo baada ya kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Nilipomaliza masomo ya sheria nilianza rasmi kazi hii na huwa natumia gharama zangu za nauli kusafiri kutoka mkoa mmoja hadi mwingine kwa ajili ya kazi hii.
Ndiyo maana nimemwambia mleta mada kama bado yupo hapo kijijini afanye mpango wa mawasiliano ya huyo mwalimu hamnazo nianze kushughulika naye kisheria.
Ni Stress sijui baadhi ya walimu wanayo..Kwanini umpe mtoto wa mtu mwingine kipigo kikali ??Ukiona ni mkorofi ameshindikana achana nayeMwalimu Frank jela inakubeep.
Kimbia fasta.
Na wewe ulivyo mjinga Jambo la kijiweni kwenye kahawa unaleta hukuu? Shamba umepata kwanza wewe...kenge jike weweWanakijiji wamekujaza majungu na fitina na wewe umeyachukua kama yalivyo na kwanini umeconclude bila kusikiliza upande mwingine kwa kumuuliza muhusika.
Wazazi wamewaachia malezi yote walimu. Shida inaanzia hapo.HIvi karibuni katika hekaheka za kutafuta mashamba kwa ajili ya msimu ujao wa kilimo nilifika katika kijiji kimoja kinaitwa Mandimu kilichopo Kata ya Mungaa, Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.
Baada ya kukamilisha mambo yangu nikakaa kijiweni na Vijana wa eneo hilo kujua mbili tatu za eneo hilo.
Katika storI za hapa na pale akapita kijana mmoja ambaye alionekana kumfokea mzee mmoja, nikauliza kulikoni mbona 'dogo' anakosa adabu.
Nikaambiwa bwana huyo ni Mwalimu flani (akamtaja kwa jina la kwanza - Frank) huyo bwana hachezewi hakuna anayemgusa. Ilibid nidadisi zaidi kwani ana ishu gani. Ndipo wakanipa kisanga kizima.
Soma Pia: Mwalimu huyu wa Shule ya Msingi Mungu Maji aangaliwe, ananyanyasa Wanafunzi
Wakasema tangu Mwalimu Frank afike kijijini hapo kabla ya kuwa Mwalimu Mkuu amekuwa akitandika watoto wetu kinyama sana.
Watoto wanashika nondo juu kwenye dirisha ndio wanachapwa, kutandikwa huko sio kwenye makalio tu. Fimbo zinachapwa mgongoni miguuni hadi kichwani, sio fimbo tu anatumia hadi mateke na ngumi. Vipigo hivi ni wasichana na wavulana.
Nikaelezwa kuwa Watoto wengi wameacha shule kwa kuhofia kipigo cha kinyama cha mwalimu huyo pindi wanapokosea. Baadhi ya Wazazi hawana budi kukubali watoto kubaki nyumbani kwani wanahofia pia wanaweza kuumizwa vibaya kwasababu ilishawahi kutokea mtoto mmoja ambaye angemaliza la saba mwaka huu (2024) alichapwa na Mwalimu huyo baadaye akaanza kulalamika maumivu ya tumbo na wiki moja baadaye alipoteza maisha, so haikujulikana wazi kama chanzo ni mwalimu au alikuwa na changamoto zake nyingine.
Wakazidi kunieleza kuwa kuna Wazazi wawili walikwenda kumhoji kwa nini anawatesa watoto wao nasikia yalitokea mabishano na mama huyo wakashikana na mwalimu kupigana. Mama mwingine yeye aliwashwa kibao hakuthubutu tena kuuliza chochote.
Naiomba Serikali imchukulie hatua mwalimu huyu kwani anawakatili watoto sio kwa kipigo cha kinyama bali pia kukosa haki yao.ya msingi ya kupata.elimu. Pili anawanyanyasa wanakijiji hiko yy amekuwa mungumtu.
Tanzania yetu ni nchi ya Amani mtu mmoja anawezaj3 kunyanyasa watoto na wazazi wao kwnye ardhi yao?
NAOMBA SERIKALI IMSHUGHULIKIE MTU HUYU HARAKA.
Tutafika huko ili mradi tu kuhakikisha usawa wa kijamii unafikiwa maana ukishakuwa kwenye field ya sheria hutakiwi kuogopa chochote as long as unachopambania is for public interest mkuu.Kazi nzuri, lakini Kwa nini usitumie pia taaluma yako kupambana na wabadhirifu wa mali za umma ambao wamekuwa wakibainishwa na CAG kwenye ripoti zake za kila mwaka?
Nakutakia kila la heri na Mungu wa Tanganyika awe pamoja nawe.Tutafika huko ili mradi tu kuhakikisha usawa wa kijamii unafikiwa maana ukishakuwa kwenye field ya sheria hutakiwi kuogopa chochote as long as unachopambania is for public interest mkuu.
🙏.Nakutakia kila la heri na Mungu wa Tanganyika awe pamoja nawe.
Kama umepita shule utakua unajua adhabu za jumuia kama za upiga kelele darasani wote mfiche uso kwenye dawati bila kujali kama ulipiga kelele au laa, hapo malezi ya mzazi yanaingiaje?Wazazi wamewaachia malezi yote walimu. Shida inaanzia hapo.
Wazazi wawalee watoto wao vema waache visingizio.
Mtoto akiwa vizuri kwenye malezi ya nyumbani kamwe hawezi kuadhibiwa ovyo shuleni.
Sasa hivi wazazi wanawapelekea walimu mitoto mijambazi!
Mitoto iliyoshindikana. Mitoto mila bangi. Mitoto.....
Poleni sana walimu kazi yenu ni ngumu sanaaa lakini mwenyezi Mungu atawalipieni. Msikate tamaa. Hakuna aliyemo humu JF hakupita kwa mwalimu. MMEGEUKWA!
Maelezo yako kwa kiasi kikubwa yameunga mkono hoja yangu.Kama umepita shule utakua unajua adhabu za jumuia kama za upiga kelele darasani wote mfiche uso kwenye dawati bila kujali kama ulipiga kelele au laa, hapo malezi ya mzazi yanaingiaje?
Mtoto kakulia kwenye gas na umeme au mkaa, anakuta shule wanapasua kuni hajui shoka wanashikaje na hana nguvu kivile, asipopasua kuni ni fimbo sana na kutokula hapa unakuta mzazi hajui au ni shule gani wanaandika kweny fom kua "tunapikia kuni na mtazipasua"? Malez ya mzaz yanahusika?
Kuna shule mtoto anapigwa sana kisa hajamaliza ada (kama hukupitia haya huwez kunielewa).
Mtoto hajafikia wastani wa alama kwenye tests za week)mwez atakula fimbo kulingana na masomo atakayo kua amefeli, wewe kama mzaz hapo unahusikaje?
Kwa kifupi makosa yasiyo husiana na malez ya wazaz ni mengi sana na adhabu zake hua n mbaya.