Yimakatso
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 7,060
- 9,468
Kiukweli walimu wanahitaji ushauri wa kisaikolojia maana inaonekana wana shida kubwa vichwani mwao hivyo wanaamini kumalizia stress zao kwa watoto kutapunguza changamoto walizonazo.Kila siku humu tunaambiwa wanaume wa vijijini ni mashababi ukilinganisha na Dar kumbe Huwa tunalishwa matongo pori.
Baadhi ya Walimu hasa wa kiume wakiwa huko vijijini Huwa wanajiona kama watawala kwenye hilo eneo ovyo kabisa hao watu.
Niliendaga Namanyere Rukwa kumsalimia kaka yangu ambaye ni mwalimu, siku tukaamua kutembea tembea kujionea mji Kila tunakopita mwalimu anajulikana vibaya mno na wanakijiji basi tukapita mtaa mmoja tunasikia kelele watoto kama miaka 12-16 wamefungiwa ndani wanachapwa kufika tu mwalimu hata hajauliza akaomba fimbo na yeye akaingia ndani kuanzia kuwatandika wale madogo wakati zinaondoka nikamwambia sasa wewe jamaa unawachapa watoto wa watu kiasi hiko ikitokea mtu akakata moto ghafra hujui kama ni kesi ?
Wapo baadhi ya walimu wanaojitambua walishaapa hawatahangaika kuchapa mtoto wa mtu maana ikitokea bahati mbaya mtoto akadhurika basi kibarua chake kinaishia hapo hapo na jela inamchungulia.
Hivi walimu hawawezi kufanya kazi yao ya ualimu ambayo jukumu la kwanza ni kufundisha wakaachana na stress za kuadhibu watoto hovyo?
Sema walimu ni sikio la kufa kila siku wanapatwa na majanga kutokana na adhabu kwa watoto lakini hawajifunzi tu.