A
Anonymous
Guest
Naomba kuwasilisha kilio cha wananchi kuhusu ujenzi wa barabara ya Bonyokwa, hususan eneo la Kimara Mwisho.
Zaidi ya mwaka mmoja uliopita, mkandarasi alichimba upande mmoja wa barabara lakini akaiacha bila kuendelea na ujenzi. Hali hiyo imeendelea kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara. Magari, pikipiki na bajaji hupata ajali mara kwa mara kutokana na ubovu wa eneo hilo, jambo linalosababisha majeraha kwa wananchi na uharibifu wa vyombo vya usafiri.
Kinachoshangaza ni kwa nini mkandarasi aliruhusiwa kuchimba barabara ikiwa maandalizi ya kuendelea na ujenzi hayakuwa yamekamilika. Wananchi tunaendelea kuumia kila siku huku tukikosa majibu ya lini mradi huu utakamilika. Barabara ya Bonyokwa imekuwa ahadi inayorudiwa kwa muda mrefu bila kuona utekelezaji unaoonekana.
Tunaiomba Serikali, kupitia TANROADS na Wizara ya Ujenzi, kuchukua hatua za haraka kurejesha usalama wa barabara hii na kuharakisha utekelezaji wa mradi. Maisha ya wananchi yanapaswa kupewa kipaumbele kuliko ahadi zisizo na utekelezaji.