Serikali imekuja na propaganda ya kuonyesha Mali zilizohalibika Wananchi na Nyie Endeleeni kuonyesha Maiti za Marehemu

Serikali imekuja na propaganda ya kuonyesha Mali zilizohalibika Wananchi na Nyie Endeleeni kuonyesha Maiti za Marehemu

Maiti si polisi wamezing'ang'ania watu wanapiga kelele wapewe maiti za ndugu zao wakazike kwa heshima lakini hazionekani. Mass graves. Mass cremation. Wataonyesha nini wakati hata miili haionekani?
 
Akili ya mama hiyo, mama kaimbwa weee kuelekea uchafuzi mkuu...mara bao la mama, madaktari wa mama, ushuzi wa mama, kalamu ya samuya nk nk nk ila vyooote havikumsaidia kitu, mwisho wa siku wananchi wakamkataa kwenda kumpigia kura!
Wananchi wa leo sio wa jana, propaganda hazitakusaidia kitu ewe rais haramu!
 
Kwamba serikali itapata hasara kurekebisha hizo mali ila kwenye upigaji wao serikali haipati hasara 😂
 
Propaganda ya kuonyesha mali ni nzuri wananchi nao waendelee kuonyesha Maiti za Marehemu tuone vitu vinarudishwa uhai wa watu Je?
Ni ujinga usio na mfano kulinganisha uharibifu wa mali na mauaji ya raia wasio na hatia. Kiongozi anayefanya hivyo anagongwa na wachawi.
 
Maiti si polisi wamezing'ang'ania watu wanapiga kelele wapewe maiti za ndugu zao wakazike kwa heshima lakini hazionekani. Mass graves. Mass cremation. Wataonyesha nini wakati hata miili haionekani?
Nikiangalia yanayofanywa na watawala wa Africa halafu nikikumbuka historia ya Africa ilivyosikitika siyo tu jinsi Patrice Lumumba alivyokufa ila pia jinsi ushahidi wa kifo chake na mwili wake kuchomwa na kuyeyushwa kwa acid ili kusiwe na kaburi lake, nachoka mimi.

Wale wanaowaita hawa watawala wetu kuwa ni wakoloni weusi na makaburu weusi wana hoja nzito sana maana wanayoyafanya ni hayo hayo na wakati mwingine yanazidi maradufu na yale yaliyofanywa zamani.
 
Kwamba serikali itapata hasara kurekebisha hizo mali ila kwenye upigaji wao serikali haipati hasara 😂
Hawachelewi kuzira hawa watawala wakasusa kurekebisha miundombinu iliyoharibika. Kwanza inabidi wafurahi maana wamepata fursa nyingine ya kupiga pesa za wananchi.
 
Hawachelewi kuzira hawa watawala wakasusa kurekebisha miundombinu iliyoharibika. Kwanza inabidi wafurahi maana wamepata fursa nyingine ya kupiga pesa za wananchi.
Tutaambiwa kurekebisha miundombinu ya mwendokasi ni 2T kumbe n 5B 😂
 
Ofisi ya ccm kinondoni mkwajuni motooo.
Iile gorofa walipambana sana kulijenga mpaka limeisha .ndo hvyo hakuna kulaumiana
 
Back
Top Bottom