TheCrocodile
JF-Expert Member
- May 31, 2021
- 1,864
- 5,254
Sintofahamu imeibuka katika Mtaa wa Longdong, Kata ya Sokon One jijini Arusha, siku moja baada ya mazishi ya Gervas Jackson, baada ya ndugu wa marehemu kuanza kuhoji kuhusu mali na fedha alizoacha.
Gervas Jackson alifariki dunia kutokana na ajali na kuzikwa jana katika Makaburi ya Njiro jijini Arusha. Baada ya mazishi, ndugu wa marehemu walifanya kikao kilichomhusisha mjane wake, Flora Stanley, wakitaka kufahamu mali alizoacha pamoja na kiasi cha fedha alichokuwa nacho.
Flora amesema yeye na Gervas walifunga ndoa rasmi Oktoba 16, 2021, na waliishi pamoja hadi kifo cha mume wake.
Kwa mujibu wa Flora, baadhi ya ndugu katika kikao hicho walidai kuwa marehemu hakuwa na uwezo wa kupata mtoto, hivyo wakaibua pia mashaka kuhusu mtoto aliyemzaa na marehemu, wakidai si mtoto wa ndugu yao.
Hali hiyo imezua hisia miongoni mwa wananchi, hasa baada ya Flora kueleza kuwa mmoja wa mawifi yake amechukua hati ya nyumba pamoja na hati ya kiwanja, mali ambazo anasema zilinunuliwa na yeye pamoja na marehemu wakati wa uhai wao.
Baada ya wananchi kufahamu kuhusu kuchukuliwa kwa hati hizo, waliandamana hadi nyumbani kwa mmoja wa mawifi hao na kumtaka azikabidhi ili zimrudie mjane, wakieleza kuwa suala la umiliki wa mali linapaswa kushughulikiwa kwa haki na kwa kufuata sheria.
Mvutano huo ulimfanya Diwani wa Kata ya Sokon One, Muksin, kufika katika eneo hilo kwa ajili ya kuhakikisha hali ya amani na utulivu inaendelea.
Nyumbani hapo pia anaishi mama wa marehemu, ambaye ni mama mkwe wa Flora. Mama huyo anaelezwa kuwa anaumwa na hawezi kuzungumza, hali iliyowafanya baadhi ya wananchi kutaka ndugu wa marehemu wachukue jukumu la kumhudumia.
Hata hivyo, tukio hilo limeibua mjadala mpana kuhusu changamoto zinazowakabili baadhi ya wajane jijini Arusha, ambapo kumekuwa na malalamiko ya ndugu au watu wengine kujaribu kudai au kuchukua mali zilizoachwa na waume zao mara tu wanapofariki.
Wananchi wameitaka serikali kuangalia namna bora ya kudhibiti vitendo hivyo na kuweka mifumo madhubuti ya kuwalinda wajane dhidi ya kupoteza mali zao baada ya vifo vya waume zao.
Video: