Sintofahamu yaibuka siku moja baada ya mazishi, ndugu wadai mali za marehemu

Sintofahamu yaibuka siku moja baada ya mazishi, ndugu wadai mali za marehemu

Kuna familia moja hivi, wamasai baba yao amefariki hata mwili haujapoa ndani ya masaa machache, watoto wamepata ru taarifa kitu cha kwanza wanaanza kugombania kadi za magari na hati za nyumba na mama yao. Sema mama yao alikua strong akawaambia msinichezee nyie vifaranga.
Kaskazini na Mali wanatoana Roho, ndio kisa cha wasiojulikana kuenea
 
Kichekesho kikubwa kwenye huu uzi ni hao ndugu kuanza kudai eti marehemu alikuwa na matatizo ya uzazi, mara mtoto si wake. Seriously? Hizi dharau kwa wajane zinatakiwa zikome. Kama wana wasiwasi na damu ya ndugu yao, waache porojo za mtaani na waweke mezani hela ya vipimo, mtoto apelekwe kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, ukweli ni kuwa hawana uchungu na mtoto hapo, wanataka tu kumchafua Flora ili wapate sababu ya kumfukuza na kubeba hizo mali, science will humble them, wakipewa majibu ya DNA wataficha wapi nyuso zao hao?
 
Huyo mjane haudhuriagi vikao vya wanawake!
Mume akifa hutakiwi kuanza kulia sijui kuzimia. Unakusanya documents muhimu unazihamisha halafu ndo unaanza kulia kwa kwikwi😂
Mme na mke sio ndugu wa damu. Na ndio maana mme akifariki siku hiyohiyo mke anachukuliwa na mwanamme mwingine na kuanza kutumia pesa za mme wake wa zamani na huyo mchepuko. Na mke akifariki mme pia anaanza kutafuna pesa na mchepuko wake. Kwasabababu Mke na mme sio ndugu wanatakiwa kuandaa document za kurithisha mali zao watoto wao ambao ndio ndugu zao. Watoto ni ndugu wa damu wa mama. Watoto pia ni ndugu wa damu ya baba. Mali asirithishwe mke au mme bali watoto. Na document itamke wazi watoto hawaruhusiwi kuziuza isipokua kuziendeleza tu na kile watakacho kipata kwenye kuziendeleza watamgawia ndugu yao wa damu yaani mama au baba yao. Au hata kama mama au baba yao aliyebaki ataziendeleza ataziendeleza hizo mali zikiwa katika umiliki wawatoto ambao ni ndugu zao.
 
Kama ndugu wana tamaa hata ukiandika wosia, bado tu watasumbua, mahakamani n.k. Pia wosia unaweza pingwa mahakamani.
Wao kuwa na tamaa hakutabadilisha matakwa yako, kama wosia utakua umekidhi vigezo hata upingwe mpaka Mahakama ya Rufani, hautabatilishwa. Onana na wakili akuandalieni vyema wosia, ndio suluhu ya vurugu mechi kama hizi.
 
Shehe, tamaa ni uchawi.
Unadhani mali zinapatikana kirahisi basi. Kuna mali zingine nimemwandikisha wife,akija kuhonga nikifa atajijuaga mwenyewe.
Hahahaha!
Uko radhi agongewe ndani ya nyumba uliyomuachia?😃
 
Wao kuwa na tamaa hakutabadilisha matakwa yako, kama wosia utakua umekidhi vigezo hata upingwe mpaka Mahakama ya Rufani, hautabatilishwa. Onana na wakili akuandalieni vyema wosia, ndio suluhu ya vurugu mechi kama hizi.
Hakuna kesi ya mirathi ambayo ni rahisi, hata kama uliacha wosia. Wakienda tu mahakamani, hata kama mwishoni wosia utafuatwa, ila miaka hapo sio chini ya mitano itapotea kukimbizana na kujibishana mahakamani.
Tamaa ni mbaya sana.
 
Sintofahamu imeibuka katika Mtaa wa Longdong, Kata ya Sokon One jijini Arusha, siku moja baada ya mazishi ya Gervas Jackson, baada ya ndugu wa marehemu kuanza kuhoji kuhusu mali na fedha alizoacha.

Gervas Jackson alifariki dunia kutokana na ajali na kuzikwa jana katika Makaburi ya Njiro jijini Arusha. Baada ya mazishi, ndugu wa marehemu walifanya kikao kilichomhusisha mjane wake, Flora Stanley, wakitaka kufahamu mali alizoacha pamoja na kiasi cha fedha alichokuwa nacho.

Flora amesema yeye na Gervas walifunga ndoa rasmi Oktoba 16, 2021, na waliishi pamoja hadi kifo cha mume wake.

Kwa mujibu wa Flora, baadhi ya ndugu katika kikao hicho walidai kuwa marehemu hakuwa na uwezo wa kupata mtoto, hivyo wakaibua pia mashaka kuhusu mtoto aliyemzaa na marehemu, wakidai si mtoto wa ndugu yao.

Hali hiyo imezua hisia miongoni mwa wananchi, hasa baada ya Flora kueleza kuwa mmoja wa mawifi yake amechukua hati ya nyumba pamoja na hati ya kiwanja, mali ambazo anasema zilinunuliwa na yeye pamoja na marehemu wakati wa uhai wao.

Baada ya wananchi kufahamu kuhusu kuchukuliwa kwa hati hizo, waliandamana hadi nyumbani kwa mmoja wa mawifi hao na kumtaka azikabidhi ili zimrudie mjane, wakieleza kuwa suala la umiliki wa mali linapaswa kushughulikiwa kwa haki na kwa kufuata sheria.

Mvutano huo ulimfanya Diwani wa Kata ya Sokon One, Muksin, kufika katika eneo hilo kwa ajili ya kuhakikisha hali ya amani na utulivu inaendelea.

Nyumbani hapo pia anaishi mama wa marehemu, ambaye ni mama mkwe wa Flora. Mama huyo anaelezwa kuwa anaumwa na hawezi kuzungumza, hali iliyowafanya baadhi ya wananchi kutaka ndugu wa marehemu wachukue jukumu la kumhudumia.

Hata hivyo, tukio hilo limeibua mjadala mpana kuhusu changamoto zinazowakabili baadhi ya wajane jijini Arusha, ambapo kumekuwa na malalamiko ya ndugu au watu wengine kujaribu kudai au kuchukua mali zilizoachwa na waume zao mara tu wanapofariki.

Wananchi wameitaka serikali kuangalia namna bora ya kudhibiti vitendo hivyo na kuweka mifumo madhubuti ya kuwalinda wajane dhidi ya kupoteza mali zao baada ya vifo vya waume zao.
Video:
View attachment 3646821
Hiyo kaskazini ndio kanda inayosifika kuwa na watu wenye hali nzuri kiuchumi na angalau elimu nzuri lakini ndio kila siku tunasikia wanafanya matukio ya kipumbavu na kimaskini. Sasa huko ambako hawajaelimika kiasi cha kutosha hali itakuwaje?
 
Hiyo kaskazini ndio kanda inayosifika kuwa na watu wenye hali nzuri kiuchumi na angalau elimu nzuri lakini ndio kila siku tunasikia wanafanya matukio ya kipumbavu na kimaskini. Sasa huko ambako hawajaelimika kiasi cha kutosha hali itakuwaje?
Shida ni tamaa😂
 
Back
Top Bottom