Serikali imepandisha sana gharama za kutuma na kupokea hela kwa simu, ole wake mtu aniambie tuma na ya kutolea

Serikali imepandisha sana gharama za kutuma na kupokea hela kwa simu, ole wake mtu aniambie tuma na ya kutolea

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
IMG-20210714-WA0204.jpg

Pongezi kwa bunge la kijani la Mwendazake kwa kuyafanya maisha ya Mtanzania yawe magumu kila kukicha.
 
Mkome!

Wakati Mwigulu anasoma bajeti ya kupandisha kodi kule bungeni mambo yalikuwa hivi hapa jf[emoji116]

Uzi wa bajeti ulikuwa na replays 90

Uzi wa Sabaya ulikuwa na replays elfu 1 na zaidi

Uzi wa kusaini petition ya kumtoa Diamond kwenye tuzo za bet ulikuwa na replays 800 na zaidi.


Kuleni upumbavu wenu. Najua na hili mtapiga kelele siku 2 hizi alafu mtarudi kwenye ujinga wenu.
 
Si tulikubaliana mama afungue nchi na sifa kedekede tulimpa na tathmini ya siku zake mia tulizipamba!,tuvute pumzi ndo kwanza safari inaanza.
Msoga oyee.
 
Mradi wa SGR, Bwawa la Nyerere, Kuhamia Dodoma ndio sababu kuu ya haya makodi mapya
 
Mkome!

Wakati Mwigulu anasoma bajeti ya kupandisha kodi kule bungeni mambo yalikuwa hivi hapa jf...
Dah,nakumbuka mkuu adi tulijibishana kwenye uzi wa sadala na bet!kumbe ndo mwigulu alikua anapitisha haya?nimejuta jamani😪😪😪
Ya msingi tuliacha,tukabaki kumsalandia sadala!
 
Mzunguuko mkubwa wa pesa upo kwenye miamala na wala sio benki kama ilivyokuwa awali. Kwa hiyo serikali inakwenda kutafuta pesa where the money is.

There is no such a thing as free lunch, miradi mingi ya maendeleo inahitaji pesa nyingi. Na hiyo ndio gharama ya maendeleo.
 
Back
Top Bottom