Serikali imependekeza Sheria zinazolinda Maliasili na Kuikinga Nchi na Mikataba Mibovu zisitumike kwa DP World

Hizo pesa za kuwalipa zinatoka wapi mkataba ukivunjwa,huu ni ujinga labda tumuweke Tundu Lissu ikulu atusaidie kupiga mnada mali za ccm tuwalipe.
 
View attachment 2678469
Serikali ya Samia imepeleka muswada wa mabadiliko ya sheria kadhaa bungeni ili sheria zote za zamani zinazokinzana na mkataba na DP world zibadilishwe ili ziendane na hiyo IGA ya Dubai Ports World ‼️

Serikali imependekeza Sheria zinazolinda Maliasili na Kuikinga Nchi na Mikataba Mibovu zisitumike kwa DP World​


Serikali ya Samia imepeleka muswada wa mabadiliko ya sheria kadhaa bungeni ili sheria zote za zamani zinazokinzana na mkataba na DP world zibadilishwe ili ziendane na hiyo IGA ya Dubai Ports World.

Muswada wa "The Written Laws (Misc Amendment) No. 2 Bill, 2023" umesomwa kwa mara ya Kwanza tarehe 28 June 2023. Kamati ya Utawala Katiba na Sheria itauchambua kwenye vikao vya Kamati Mwezi wa Nane (Kuanzia 14 August).

Muswada huu unapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria Tano ikiwemo: (1) Sheria ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam, Sura ya 253; (2) Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Mali na Rasilimali Asilia, Sura ya 449; (3) Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusu Utajiri na Maliasilia za Nchi (Mapitio ya Mikataba na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi), Sura ya 450.

Muswada huo unapendekeza kutotumika kwa Sheria mbili zilizopitishwa na Bunge mwaka 2017 kwa madhumuni ya Kulinda Rasilimali zote za Tanzania katika Miradi ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Bandari endapo itakuwa imesharidhiwa na Baraza la Mawaziri.

Katika mapendekezo ya mabadiliko hayo, Muswada unataka Sheria hizi zisitumike ili kuwezesha Bandari za Tanzania zifanye kazi kwa Viwango vya Kimataifa zikipata Meli kubwa za Mizigo mikubwa. Vifungu vya wali na mabadiliko yanayopendekezwa ni kama ifuatavyo:

Jina la muswada wa marekebisho ya Sheria hili hapa:



Marekebisho ya kwanza yanayopendekezwa haya hapa:




Sheria mama ya 2017 inayotakiwa kubadilishwa inasea haya (katika aya ya 36, maneno "section 2" hapo juu yasomeke kamma "section 11"):




Marekebisho ya pili yanayopendekezwa haya hapa:




Sheria mama ya 2017 inayotakiwa kubadilishwa inasea haya (katika aya ya 38 hapo juu maneno "section 2" yasomeke "section 7"):



Hiyo ndiyo nguvu ya Waarabu wa Dubai!
 

Attachments

  • 1688511785655.png
    11.1 KB · Views: 2
  • 1688511812226.png
    12.5 KB · Views: 2
Hilo bunge linakaa nyumbani kwenu? Kuna bunge sahivi? Hivi huoni aibu kuleta uzushi wa kipuuzi km huu? Acheni rais afanye kazi yake, km we unaihitaji subiri 2025 uchukue fomu.
Unajua maana ya kusomwa mara ya Kwanza wewe mkurupuKaji? Umeambiwa sheria imesomwa bungeni Kwa mara ya kwanza kwenye Bunge la bajeti unatakaje zaidi?
 
Wacha kutulisha maneno yako, weka hayo mabadiliko yanayotakiwa yabadilishwe. Mbona umetaja vifungu ukaweka porojo zako badala ya hayo ya muswaa sasa hivi yako vipi na mapendekezo yatayobadilishwwa yako hivi. Sijaona..

DP World inahusiana nini na sheria zenu za ndani?

Wacha soinning.
 
Uchumi wa tanzania unachangiwa asilimia kubwa na mapato yatokana na revenue za bandari , approximate zaidi ya asilimia 40 , nazani ....


TICTS co. Walikuwepo for 26 years and they left ..sasa hii DP world inataka ipewe for indifinitely time pamoja na ku meet their contractual demands like TAX free , free to monitor all economic sector in the country ....

huku sisi tukipapaswa mikodi kama yote.....mpaka. Hela ya kula kesho inalipia kodi ili ku meet government expenses or public costs....


Sasa hii kiti kumpa mtu mmoja for indifinitely period .....afuu dahhh




Siku nikisikia Huyu mtu akitoka ofisini. Na kusema ""nimejiuzulu nafasi hii ya uraisi"" nchi italipuks kwa shangwe mnoooo
 
Mkataba wa DP WORLD na TPA uko wapi?
 
Bibi
Mkataba wa DP WORLD na TPA uko wapi?
shida sio mkataba (contract) bali. Yaliyomo ndani humo ndani ndani bibi elewa elewa elewaaaa ,,,, maneno yaliyo tumika ni kama tumefanywa double standards , kwamba ikitokea material breach hakuna kuvunja mkataba bali utaendelea tuuu , without any legal actions ????
 
Dah ama kweli Kuwa uyaone





Wazazi wetu walituambia kuwa uyaone....tunayaona sasa tumesoma , na tukasoma. Now tunatumia elimu kupambanua maisha. Dah
 
Hilo bunge linakaa nyumbani kwenu? Kuna bunge sahivi? Hivi huoni aibu kuleta uzushi wa kipuuzi km huu? Acheni rais afanye kazi yake, km we unaihitaji subiri 2025 uchukue fomu.
Kama hujui kusoma acha walioelewa wachangie umeambiwa bunge litakaa August. Usijitoe ufahamu kwa kutetea waarabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…