Serikali imesikiliza maoni ya wananchi inapoikubalia Kampuni ya MOFAT ombi LATRA kuziondoa Daladala Mbagala?

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
15,415
Reaction score
29,584
Mwezi January mwaka huu 2026, kampuni ya mabasi ya mwendokasi MOFAT ilituma ombi kwa LATRA kwamba walikuwa wakipata hasara ruti ya Mbagala kutokana na uwepo wa bajaji, bodaboda na daladala. Sisi wa zamani tunakumbuka wakati wa zoezi la ubinafsishaji sekta ya benki, benki binafsi za nje walitaka serikali iivunje NBC kwanza ndio waje. Nyerere alikataa Mkapa akakubali. Leo tunaona jambo kama hili tena.

Wadau wengi hawakukubaliana na maoni haya, wakitoa maelezo, kwamfano, kwamba uhitaji wa usafiri eneo la Mbagala ni mkubwa mno kwa mabasi ya mwendo kasi peke yake kukidhi mahitaji.

Leo tunasikia MOFAT wamekubaliwa maombi yao, kwamba daladala sasa zitapigwa marufuku huko Mbagala.

Kuna faida ya kuzuia daldala, kwa mfano kupunguza msongamano wa magari na hata uchafu katika ruti zinazotumika na daladala. Hata hivyo, tunajiuliza kama LATRA wamefanya upembuzi yakinifu hadi kufikia uamuzi huu, ikiwa ni pamoja na mambo yafuatayo
  1. Je LATRA wamesikiliza maoni ya wadau juu ya jambo hili?
  2. Je LATRA wamejihakikishia MOFAT watakidhi mahitaji ya usafiri Mbagala?
  3. Je LATRA watahakikisha monopoly ya MOFAT haisababishi wao kujipangia nauli wanavyotaka?
  4. Je MOFAT watahudumia katika muda ule daladala zinahudumia, kuanzia asubuhi hadi usiku?
  5. Je LATRA imefikiria kwamba kuruhusu MOFAT peke yake kunatengeneza "monopoly" ambayo inapingana na sheria za ushindani wa kibiashara?
  6. Je LATRA wamefikiria uwezekano wa kuwaruhusu daladala kuwa na mabasi ya kiwango cha mabasi ya mwendokasi ili waruhusiwe kutumia njia za BRT?
Ikiwa LATRA wamefikiria haya mambo yote na kupata majibu yanayoridhisha, basi wananchi hatuna neno. Ikiwa sivyo, LATRA mnatafuta vita huko Mbagala
 
1781685824576.png

Ndio haya tunayasema. Hivi hii serikali inawakilisha wananchi au baadhi ya viongozi mafisadi wa sasa na wa awamu za nyuma ambao tunajua wana hisa katika kampuni za Mwendokasi?
 
Mwezi January mwaka huu 2026, kampuni ya mabasi ya mwendokasi MOFAT ilituma ombi kwa LATRA kwamba walikuwa wakipata hasara ruti ya Mbagala kutokana na uwepo wa bajaji, bodaboda na daladala. Sisi wa zamani tunakumbuka wakati wa zoezi la ubinafsishaji sekta ya benki, benki binafsi za nje walitaka serikali iivunje NBC kwanza ndio waje. Nyerere alikataa Mkapa akakubali. Leo tunaona jambo kama hili tena.

Wadau wengi hawakukubaliana na maoni haya, wakitoa maelezo, kwamfano, kwamba uhitaji wa usafiri eneo la Mbagala ni mkubwa mno kwa mabasi ya mwendo kasi peke yake kukidhi mahitaji.

Leo tunasikia MOFAT wamekubaliwa maombi yao, kwamba daladala sasa zitapigwa marufuku huko Mbagala.

Kuna faida ya kuzuia daldala, kwa mfano kupunguza msongamano wa magari na hata uchafu katika ruti zinazotumika na daladala. Hata hivyo, tunajiuliza kama LATRA wamefanya upembuzi yakinifu hadi kufikia uamuzi huu, ikiwa ni pamoja na mambo yafuatayo
  1. Je LATRA wamesikiliza maoni ya wadau juu ya jambo hili?
  2. Je LATRA wamejihakikishia MOFAT watakidhi mahitaji ya usafiri Mbagala?
  3. Je LATRA watahakikisha monopoly ya MOFAT haisababishi wao kujipangia nauli wanavyotaka?
  4. Je MOFAT watahudumia katika muda ule daladala zinahudumia, kuanzia asubuhi hadi usiku?
  5. Je LATRA imefikiria kwamba kuruhusu MOFAT peke yake kunatengeneza "monopoly" ambayo inapingana na sheria za ushindani wa kibiashara?
  6. Je LATRA wamefikiria uwezekano wa kuwaruhusu daladala kuwa na mabasi ya kiwango cha mabasi ya mwendokasi ili waruhusiwe kutumia njia za BRT?
Ikiwa LATRA wamefikiria haya mambo yote na kupata majibu yanayoridhisha, basi wananchi hatuna neno. Ikiwa sivyo, LATRA mnatafuta vita huko Mbagala
Fr Kitima aliwaonya mkashupaza shingo na mfe kabisa
 
kwa ule wingi wa watu pale mbagala tutegemee kilio si muda mrefu.

juzi kati nilishuka mbagala pale saa tisa usiku , nilipata daladala mpaka mwenge.
sasa sijui ni mwendokasi gani watakuwa na gari muda huo .
 
Mwezi January mwaka huu 2026, kampuni ya mabasi ya mwendokasi MOFAT ilituma ombi kwa LATRA kwamba walikuwa wakipata hasara ruti ya Mbagala kutokana na uwepo wa bajaji, bodaboda na daladala.
What if Daladala nazo zikatuma maombi LATRA kwamba uwepo wa MOFAT unafanya na wao wanapata Hasara!

Hili Taifa mtu akiitwa MUWEKEZAJI, basi anapora haki zote za wazawa kwenye hilo eneo, na wanamtoa kabisa kwenye ushindani wa kibiashara?

Kama MOFAT anapata Hasara, kwanini asiangalie utaratibu mwingine(mbinu) wa kupata Faida, kwasababu kama unapata hasara maana yake kuna changamoto kwenye utoaji wako wa huduma (Nauli kubwa, upatikanaji wa magari, muda wa Safari n.k), Je MOFAT wamejaribu kurekebisha hayo?

MONOPOLY ni dalili ya kukosa Akili za kibiashara na kutumia Ubabe kwenye ushindani, matokeo yake watumiaji wa huduma ndio wataenda kuathirika zaidi.

Tanzania bila Rushwa, Haiwezekani!
 
Ni suala la kutambua nani wana maslahi ndani ya MOFAT! Hawajali kabisa wananchi ilimradi wanatengeneza hela zaidi
 
kwa ule wingi wa watu pale mbagala tutegemee kilio si muda mrefu.

juzi kati nilishuka mbagala pale saa tisa usiku , nilipata daladala mpaka mwenge.
sasa sijui ni mwendokasi gani watakuwa na gari muda huo .
Hilo ni jambo muhimu sana ambalo LATRA walipaswa kujiuliza. Wafanya biashara wanaamka saa 10 alfariji, hizo MOFAT zitakuwapo?
 
Lilikuwa ni suala la muda tu.... uwekezaji hauji bila maumivu.

Kuhusu ushirikishwaji wa wananchi wa eneo hilo, ilitakiwa ufanyike kabla ya uwekezaji kwa kufuata misingi ya bottom up approach...
 
Namuelewa yule mzee aliyesema kuishi Dsm ni kisababishi cha afya ya akili kwenda mrama.
Mmhh. Zamani nilisema askari wetu polisi ile harufu ya vituo vya polisi inawaathiri akili. Sasa hawa viongozi wetu sijui ni kitu gani kinaleta tatizo huko kichwani? NI harufu ya hela walizofungia nyumbani kwao wakiogopa kuziweka benki? Usikute hizo hela zinatoa fungus spores wanazovuta na zinaanza kuwaharibu akili
 
Lilikuwa ni suala la muda tu.... uwekezaji hauji bila maumivu.

Kuhusu ushirikishwaji wa wananchi wa eneo hilo, ilitakiwa ufanyike kabla ya uwekezaji kwa kufuata misingi ya bottom up approach...
Swali ni kwamba, kuzifungia daladala ilikuwa sehemu ya maamuzi ya mradi wa BRT au ni shinikizo la MOFAT baada ya kupewa mkataba? Hiki kipengele kipo kwenye mkataba wa MOFAT?

In fact, daladala wanaweza kuipeleka LATRA mahakamani kwa jambo hili. Mara nyingine mahakama inaweza kuwa fursa
 
Hapa ishu ni kwamba hatujui shughuli za umma kwenye nchi yetu ziendeshwe vipi...

Kama tumeamua ku-modernize usafiri wa umma kiasi cha kuweka BRT, basi lazima serikali iweke kanuni na utaratibu wa namna BRT zitaendeshwa...

Vitu kama uwepo wa mabasi ya kutosha, kiwango cha nauli, mabasi ku-operate masaa kadhaa kwa siku n.k...

Daladala zinaweza zikaondolewa zote na watu wakafurahia maisha ya usafiri wa umma fresh tu, lakini ni hadi tuwe tayari kusimamia huo mradi...

Nchi zote zenye BRT huwa hazina usafiri wa "daladala", huko wameweza kwa kuwa kila kitu wanakifanya wakiwa serious...
 
Swali ni kwamba, kuzifungia daladala ilikuwa sehemu ya maamuzi ya mradi wa BRT au ni shinikizo la MOFAT baada ya kupewa mkataba? Hiki kipengele kipo kwenye mkataba wa MOFAT?

In fact, daladala wanaweza kuipeleka LATRA mahakamani kwa jambo hili. Mara nyingine mahakama inaweza kuwa fursa
Kufungiwa kwa daladala katika sehemu zinazofanyakazi MOFAT, ni sehemu ya mkataba hivyo hili lingetokea tu.

Miradi kama hii imekuwa na changamoto sio tu kwa Tanzania hata huko nje mfano Brazil na Malaysia. Ambapo Daladala zilijikuta zikiondolewa barabarani kupisha aina mpya ya usafiri.

Nachoona hapakuwepo na ushikirishwaji wa wadau wote wa usafiri katika hatua zote za awali za kuanzisha mradi kama huu, na miradi mengine yoyote inayogusa maslahi ya wananchi.

Ndio maana nikasema kuwa tungetumia mfumo wa bottom up approach pasingekuwepo na kadhia hii.

Mfumo huu uliandaliwa baada ya mkutano wa mwaka 1992 huko Rio ukizitaka serikali kuu, serikali ya mtaa kusikiliza kwanza hoja za wadau juu ya maendeleo yao. Tanzania tulishiriki mkutano huu...
 
Mmhh. Zamani nilisema askari wetu polisi ile harufu ya vituo vya polisi inawaathiri akili. Sasa hawa viongozi wetu sijui ni kitu gani kinaleta tatizo huko kichwani? NI harufu ya hela walizofungia nyumbani kwao wakiogopa kuziweka benki? Usikute hizo hela zinatoa fungus spores wanazovuta na zinaanza kuwaharibu akili
Tuwaombee viongozi wetu.
 
Back
Top Bottom