Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 15,415
- 29,584
Fr Kitima aliwaonya mkashupaza shingo na mfe kabisaMwezi January mwaka huu 2026, kampuni ya mabasi ya mwendokasi MOFAT ilituma ombi kwa LATRA kwamba walikuwa wakipata hasara ruti ya Mbagala kutokana na uwepo wa bajaji, bodaboda na daladala. Sisi wa zamani tunakumbuka wakati wa zoezi la ubinafsishaji sekta ya benki, benki binafsi za nje walitaka serikali iivunje NBC kwanza ndio waje. Nyerere alikataa Mkapa akakubali. Leo tunaona jambo kama hili tena.
Wadau wengi hawakukubaliana na maoni haya, wakitoa maelezo, kwamfano, kwamba uhitaji wa usafiri eneo la Mbagala ni mkubwa mno kwa mabasi ya mwendo kasi peke yake kukidhi mahitaji.
Leo tunasikia MOFAT wamekubaliwa maombi yao, kwamba daladala sasa zitapigwa marufuku huko Mbagala.
Kuna faida ya kuzuia daldala, kwa mfano kupunguza msongamano wa magari na hata uchafu katika ruti zinazotumika na daladala. Hata hivyo, tunajiuliza kama LATRA wamefanya upembuzi yakinifu hadi kufikia uamuzi huu, ikiwa ni pamoja na mambo yafuatayo
Ikiwa LATRA wamefikiria haya mambo yote na kupata majibu yanayoridhisha, basi wananchi hatuna neno. Ikiwa sivyo, LATRA mnatafuta vita huko Mbagala
- Je LATRA wamesikiliza maoni ya wadau juu ya jambo hili?
- Je LATRA wamejihakikishia MOFAT watakidhi mahitaji ya usafiri Mbagala?
- Je LATRA watahakikisha monopoly ya MOFAT haisababishi wao kujipangia nauli wanavyotaka?
- Je MOFAT watahudumia katika muda ule daladala zinahudumia, kuanzia asubuhi hadi usiku?
- Je LATRA imefikiria kwamba kuruhusu MOFAT peke yake kunatengeneza "monopoly" ambayo inapingana na sheria za ushindani wa kibiashara?
- Je LATRA wamefikiria uwezekano wa kuwaruhusu daladala kuwa na mabasi ya kiwango cha mabasi ya mwendokasi ili waruhusiwe kutumia njia za BRT?
What if Daladala nazo zikatuma maombi LATRA kwamba uwepo wa MOFAT unafanya na wao wanapata Hasara!Mwezi January mwaka huu 2026, kampuni ya mabasi ya mwendokasi MOFAT ilituma ombi kwa LATRA kwamba walikuwa wakipata hasara ruti ya Mbagala kutokana na uwepo wa bajaji, bodaboda na daladala.
Ni suala la kutambua nani wana maslahi ndani ya MOFAT! Hawajali kabisa wananchi ilimradi wanatengeneza hela zaidiWhat if Daladala nazo zikatuma maombi LATRA kwamba uwepo wa MOFAT unafanya na wao wanapata Hasara!
Hili Taifa mtu akiitwa MUWEKEZAJI, basi anapora haki zote za wazawa kwenye hilo eneo, na wanamtoa kabisa kwenye ushindani wa kibiashara?
Kama MOFAT anapata Hasara, kwanini asiangalie utaratibu mwingine(mbinu) wa kupata Faida, kwasababu kama unapata hasara maana yake kuna changamoto kwenye utoaji wako wa huduma (Nauli kubwa, upatikanaji wa magari, muda wa Safari n.k), Je MOFAT wamejaribu kurekebisha hayo?
MONOPOLY ni dalili ya kukosa Akili za kibiashara na kutumia Ubabe kwenye ushindani, matokeo yake watumiaji wa huduma ndio wataenda kuathirika zaidi.
Tanzania bila Rushwa, Haiwezekani!
Hilo ni jambo muhimu sana ambalo LATRA walipaswa kujiuliza. Wafanya biashara wanaamka saa 10 alfariji, hizo MOFAT zitakuwapo?kwa ule wingi wa watu pale mbagala tutegemee kilio si muda mrefu.
juzi kati nilishuka mbagala pale saa tisa usiku , nilipata daladala mpaka mwenge.
sasa sijui ni mwendokasi gani watakuwa na gari muda huo .
Namuelewa yule mzee aliyesema kuishi Dsm ni kisababishi cha afya ya akili kwenda mrama.View attachment 3609720
Ndio haya tunayasema. Hivi hii serikali inawakilisha wananchi au baadhi ya viongozi mafisadi wa sasa na wa awamu za nyuma ambao tunajua wana hisa katika kampuni za Mwendokasi?
Mmhh. Zamani nilisema askari wetu polisi ile harufu ya vituo vya polisi inawaathiri akili. Sasa hawa viongozi wetu sijui ni kitu gani kinaleta tatizo huko kichwani? NI harufu ya hela walizofungia nyumbani kwao wakiogopa kuziweka benki? Usikute hizo hela zinatoa fungus spores wanazovuta na zinaanza kuwaharibu akiliNamuelewa yule mzee aliyesema kuishi Dsm ni kisababishi cha afya ya akili kwenda mrama.
Swali ni kwamba, kuzifungia daladala ilikuwa sehemu ya maamuzi ya mradi wa BRT au ni shinikizo la MOFAT baada ya kupewa mkataba? Hiki kipengele kipo kwenye mkataba wa MOFAT?Lilikuwa ni suala la muda tu.... uwekezaji hauji bila maumivu.
Kuhusu ushirikishwaji wa wananchi wa eneo hilo, ilitakiwa ufanyike kabla ya uwekezaji kwa kufuata misingi ya bottom up approach...
Kufungiwa kwa daladala katika sehemu zinazofanyakazi MOFAT, ni sehemu ya mkataba hivyo hili lingetokea tu.Swali ni kwamba, kuzifungia daladala ilikuwa sehemu ya maamuzi ya mradi wa BRT au ni shinikizo la MOFAT baada ya kupewa mkataba? Hiki kipengele kipo kwenye mkataba wa MOFAT?
In fact, daladala wanaweza kuipeleka LATRA mahakamani kwa jambo hili. Mara nyingine mahakama inaweza kuwa fursa
Tuwaombee viongozi wetu.Mmhh. Zamani nilisema askari wetu polisi ile harufu ya vituo vya polisi inawaathiri akili. Sasa hawa viongozi wetu sijui ni kitu gani kinaleta tatizo huko kichwani? NI harufu ya hela walizofungia nyumbani kwao wakiogopa kuziweka benki? Usikute hizo hela zinatoa fungus spores wanazovuta na zinaanza kuwaharibu akili