Serikali imetoa Tsh. Bil. 20 kulipa madeni ya wakulima, Wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho

Serikali imetoa Tsh. Bil. 20 kulipa madeni ya wakulima, Wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho

ndanda masasi

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2014
Posts
772
Reaction score
1,177
Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali imetoa Tsh. Bil 20 kulipa madeni ya wakulima, Wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho“JPM ametoa hizi fedha kwa ajili ya Tandahimba, Masasi, Mtwara & Kibiti kwa waliolipwa nusu, kiasi na wasiolipwa, zitaanza kulipwa kesho”

-----


Serikali imetoa shilling bilioni 20 za kulipa madeni ya wakulima, wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho. "Rais Magufuli ametoa fedha hizi kwa ajili ya Tandahimba, Masasi, Mtwara na Kibiti kwa ajili ya waliokuwa wamelipwa nusu, waliolipwa kiasi na wasiolipwa kabisa.

Fedha hizi zitaanza kulipwa kesho asubuhi," Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametoa kauli hii leo (Jumapili, Julai 19, 2020) wakati akizungumza na wanachama wa Chama cha Msingi (AMCOS) cha Matogoro na wakazi wa Tandahimba mkoani Mtwara alikoenda kuhamasisha maandalizi ya msimu wa ununuzi wa korosho.

Chanzo: Azam TV
 
Screenshot_20200719-181510_Chrome.jpg
 
Kampeni zimeanza kunoga.

Sijui wangeenda kuwaambia nini wakulima wa Korosho.
 
Kwa hiyo JPM katoa na siyo Serikali? Kama anafedha nyingi kiasi hiki kwanini aligombea kuwa Raisi,badala yake angeanzisha NGS ya kusaidia masikini?
 
Hela zimekuwa za mtu binafsi. Maana zinatoka kwa utashi wake.
Ya nini kuwa na Waziri wa Fedha. Rais atosha
 
Back
Top Bottom