Serikali imetoa Tsh. Bil. 20 kulipa madeni ya wakulima, Wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho

Serikali imetoa Tsh. Bil. 20 kulipa madeni ya wakulima, Wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho

Kutoka maktaba online :

8 October 2019

SERIKALI IPO TAYARI KULIPA DENI LA SHILINGI BILIONI 13 KWA WAKULIMA WA KOROSHO


"Msema kweli mpenzi wa Mungu,tulishindwa kuendelea kuwalipa kwakuwa fedha ilituishia,lakini Sasa tumeshapata fedha baada ya kuuza korosho zetu zote tan220,000 kwa hiyo fedha tunayo tunauhakika wa kuwalipa wakulima,"alisema Mh. Omari Mgumbo

Picha : Naibu Waziri wa Kilimo Omari Mgumbo na Mkuu wa Wilaya Sebastian Waryuba akipata maelezo kutoka kwa mkulima Ahmad Ulenje
Soma zaidi :
source : SERIKALI IPO TAYARI KULIPA DENI LA SHILINGI BILIONI 13 KWA WAKULIMA WA KOROSHO
 
Mali Kauli

WAKULIMA TANDAHIMBA WADAIWA BILIONI 1.4, MKUU WA WILAYA ATOA AGIZO HILI.
22 Jan 2020
Wakulima wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara wakaliwa kooni na Bodi ya korosho baada ya kukopeshwa mifuko ya pembejeo yenye thamani ya bilioni 1.4 ambapo wengi wao hawajalipa hivyo mkuu wa wilaya hiyo Sebastian Waryuba amewataka walipe fedha hiyo ili msimu wa 2020/21 wakulima wengine waweze kukopa tena.

Source : HTv Tanzania
 
14 Julai 2020
Mtwara, Tanzania

SHIDA YA MAJI KIJIJI CHA DING`WIDA MTWARA, KUVUNJA NDOA ZA WATU,'WANAUME ZETU WANADHANI TUNALALA KONA'

Kampeni ya serikali ya kumtua ndoo mwana mama imeshindwa Kusini, wanakwenda mwendo mrefu na kulala huko huko kuwahi foleni. Wananchi wamechoka na ahadi za viongozi


Source : HTv Tanzania
 
19 Jul 2020
Mtwara, Tanzania


Serikali imetoa shilling bilioni 20 za kulipa madeni ya wakulima, wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho. "Rais Magufuli ametoa fedha hizi kwa ajili ya Tandahimba, Masasi, Mtwara na Kibiti kwa ajili ya waliokuwa wamelipwa nusu, waliolipwa kiasi na wasiolipwa kabisa. Fedha hizi zitaanza kulipwa kesho asubuhi," Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametoa kauli hii leo (Jumapili, Julai 19, 2020) wakati akizungumza na wanachama wa Chama cha Msingi (AMCOS) cha Matogoro na wakazi wa Tandahimba mkoani Mtwara alikoenda kuhamasisha maandalizi ya msimu wa ununuzi wa korosho.

Source : Azam TV

Daaah! Huyu kweli ni rais wa wanyonge,yaaani rais katoa bilion 20 kwenye mshahara wake!!!!!!!!????? Kama thread inavyojieleza,au Mimi sijaelewa? Amezitoa wakati muafaka karibia Oct 2020. Korosho zilinunuliwa msimu uliopita mwaka Jana zinalipwa ndani ya muda mwezi mmoja kabla ya msimu mwingine wa ununuzi wa korosho!!!!! Hongera rais wetu mwenye moyo mzuri kwa wanyonge
 
16 Julai 2020
Mtwara vijijini
Tanzania

''TUNAPANDA KWENYE MIKOROSHO KUTAFUTA MAWASILIANO''.

Shida kubwa ya mawasiliano ya simu, barabara, shule ya sekondari , zahanati , hakuna maji safi yalito salama kwa wananchi sehemu ya Moma pia Afisa Mtendaji wa Kata athibitisha kero hizo.

Source : HTv Tanzania
 
20th, July 2020
dodomamc.go.tz › event › maadhim...
Maadhimisho ya miaka 10 ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote


Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote nchini ( UCSAF)

VIWANJA vya Nyerere (Nyerere Square)

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote nchini (UCSAF) unatarajia kufanya maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwake. Maadhimisho hayo ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mfuko ni sehemu ya Utekelezaji wa Kauli Mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Kuufikia Uchumi wa Kati. Kauli mbiu katika maadhimisho haya ni Mawasiliano kwa Wote ni Kichocheo cha Kuufikia Uchumi wa Kati.

Maadhimisho haya yatafanyika hapa Dodoma kuanzia tarehe 27 Aprili hadi kilele chake tarehe 30 Aprili, 2019 ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mbunge).

Katika maadhimisho haya, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote umeandaa shughuli mbalimbali katika kipindi cha muda wa maadhimisho, yakiwemo maonesho ya watoa huduma mbalimbali za mawasiliano nchini ambayo yatafanyika kuanzia tarehe 27 Aprili hadi siku ya kilele tarehe 30 Aprili 2019. Mfuko unachukua fursa hii kuualika umma wa wananchi wa Jiji la Dodoma pamoja nanyi waandishi wa habari kuhudhuria maonesho hayo yatakayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Nyerere Square) jijini Dodoma.

Sambamba na maonesho hayo, Mfuko utazindua Klabu za TEHAMA katika Shule za Sekondari za Dodoma pamoja na Msalato zilizoko Dodoma siku ya tarehe 28 April 2019. Aidha Mfuko utagawa Kompyuta kwa Wilaya ya Gairo pamoja na kuzindua mnara wa mawasiliano uliopo wilaya ya Bahi siku ya tarehe 29 Aprili 2019, ikiwa ni kielelezo cha miradi ambayo inatekelezwa maeneo mengi nchini Tanzania Bara na Visiwani.

Soma zaidi : Maadhimisho ya miaka 10 ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)

Mfuko wa Mawasiliano kwa wote upo kisheria ili kuhakikisha hata sehemu za vijijini mawasiliano kupitia minara iwafikie wananchi.


Lakini wananchi wengi bado hawajafaidika na mfuko huo kuwasogezea mawasiliano ya simu vijijini
 
16 Julai 2020
Mtwara vijijini
Tanzania

''TUNAPANDA KWENYE MIKOROSHO KUTAFUTA MAWASILIANO''.

Shida kubwa ya mawasiliano ya simu, barabara, shule ya sekondari , zahanati , hakuna maji safi yalito salama kwa wananchi sehemu ya Moma pia Afisa Mtendaji wa Kata athibitisha kero hizo.

Source : HTv Tanzania

Hivi mtwara si ndo kuna gesi na bahari? Kwa nni inazidiwa uchumi na MAENDELEO na jiji la Mwanza lenye ziwa na milima tu? R.I.P wote waliouliwa wakati wa vuguvugu la kuzuia gesi isitoke Mtwara. Ntwara kuchereee
 
Back
Top Bottom