Serikali imetoa Tsh. Bil. 20 kulipa madeni ya wakulima, Wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho

Serikali imetoa Tsh. Bil. 20 kulipa madeni ya wakulima, Wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho

Hivi mtwara si ndo kuna gesi na bahari? Kwa nni inazidiwa uchumi na MAENDELEO na jiji la Mwanza lenye ziwa na milima tu? R.I.P wote waliouliwa wakati wa vuguvugu la kuzuia gesi isitoke Mtwara. Ntwara kuchereee

Ni wakati sasa wananchi kufanya maamuzi magumu kutuma ujumbe kwa wanasiasa Oktoba 2020 kuwa wamechoka ahadi hewa.
 
Yaan Haki ya mtu inakuja kutolewa kama rushwa tena.
Watz amken'
CCM INATTAKIWA KUWA CHAMA PINZAN.
 
19 Jul 2020
Mtwara, Tanzania

Serikali imetoa shilling bilioni 20 za kulipa madeni ya wakulima, wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho. "Rais Magufuli ametoa fedha hizi kwa ajili ya Tandahimba, Masasi, Mtwara na Kibiti kwa ajili ya waliokuwa wamelipwa nusu, waliolipwa kiasi na wasiolipwa kabisa. Fedha hizi zitaanza kulipwa kesho asubuhi," Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametoa kauli hii leo (Jumapili, Julai 19, 2020) wakati akizungumza na wanachama wa Chama cha Msingi (AMCOS) cha Matogoro na wakazi wa Tandahimba mkoani Mtwara alikoenda kuhamasisha maandalizi ya msimu wa ununuzi wa korosho.

Source : Azam TV

Kama RAIS ndiye katoa hizo bilion 20,

Hakika hiyo ni RUSHWA kwa Wakulima na Wadau wa KOROSHO.

Kwa nini iwe kipindi hiki cha kuelekea UCHAGUZI?

TAKUKURU, POLISI, TUME YA UCHAGUZI NA MSAJIL WA VYAMA VYA SIASA MKO WAPI?
 
TAKUKURU hapa kuna aina ya kutafuta ushawishi wa kisiasa kwa njia zinazotia shaka hasa kwa vile nchi inaelekea ktk kufanya uchaguzi mkuu Oktoba 2020
 
Kuna watu humu wanasema ccm itashinda kwakuwa imetekeleza ilani yake yote na kupitiliza. Tunawaambia bila tume hii mbovu ccm haiwezi kushinda, na hata ikishinda itakuwa ni kwa asilimia chache mno. Saa hii wanaendelea na siasa za ghiliba. Wanajifanya kuwalipa wakulima wa korosho kwa ajili huko kusini kuna upinzani. Lakini hata wakulima wengi wa pamba hawajalipwa. Hapa ndio tunasema ni maendeleo ya vitu na sio watu.
 
Ina maana zile habari kwamba hawa jamaa bado walikuwa wanadaiwa pesa za korosho kumbe zilikuwa za kweli!!!
 
Kama RAIS ndiye katoa hizo bilion 20,

Hakika hiyo ni RUSHWA kwa Wakulima na Wadau wa KOROSHO.

Kwa nini iwe kipindi hiki cha kuelekea UCHAGUZI?

TAKUKURU, POLISI, TUME YA UCHAGUZI NA MSAJIL WA VYAMA VYA SIASA MKO WAPI?

Magufuli ndio zake, nakumbuka wakati fulani wa chaguzi za marudio akiwa waziri huko Tabora, muda mfupi kabla ya uchaguzi alienda kuahidi daraja, na akawa anawaambia wananchi waichague ccm ili daraja lijengwe. Hali ile ilileta shida sana kwani vyombo vya habari vilikuwa huru. Leo hii rushwa ya wazi itanyamaziwa maana yeye ndio rais, na hakuna wa kumfanya lolote.
 
19 Jul 2020
Mtwara, Tanzania

Serikali imetoa shilling bilioni 20 za kulipa madeni ya wakulima, wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho. "Rais Magufuli ametoa fedha hizi kwa ajili ya Tandahimba, Masasi, Mtwara na Kibiti kwa ajili ya waliokuwa wamelipwa nusu, waliolipwa kiasi na wasiolipwa kabisa. Fedha hizi zitaanza kulipwa kesho asubuhi," Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametoa kauli hii leo (Jumapili, Julai 19, 2020) wakati akizungumza na wanachama wa Chama cha Msingi (AMCOS) cha Matogoro na wakazi wa Tandahimba mkoani Mtwara alikoenda kuhamasisha maandalizi ya msimu wa ununuzi wa korosho.

Source : Azam TV

Hiyo tunaiita MEMBE impact.

Na bado.
 
Ina maana zile habari kwamba hawa jamaa bado walikuwa wanadaiwa pesa za korosho kumbe zilikuwa za kweli!!!

Zilikuwa ni za kweli tupu, na waandishi wa habari waliokuwa wanaandika hayo mambo walikuwa wanatishiwa vibaya sana.
 
Asante wa kunyumba Bernard Membe joto la uchaguzi lapanda huko kusini, Waziri Mkuu apiga kambi na serikali ya CCM Mpya inakumbuka shuka dakika za lala salama wakati tayari wananchi wamesema Twende Membe Twende 2020

Muungano wa Upinzani umeleta hofu kubwa CCM Mpya

Kama si Membe, Majaaliwa asingerudi bungeni kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 manake jamaa alikaliwa vibaya ile mbaya! Kwenye jimbo la Ruangwa, kuna kata inaitwa Mandawa; nadhani ndio au moja ya kata kubwa kabisa kwenye jimbo la Ruangwa!

Kabla CUF hawajavurugana, pale Mandawa ilikuwa ni mwendo wa CUF tu, na ndipo hapo Kassim alikaliwa kohoni ikabidi Ben afungashe virago kwenda kuokoa jahazi ingawaje alishindwa kuokoa jahazi la Jimbo la Mchinga ambao ni majirani zake!!
 
Zilikuwa ni za kweli tupu, na waandishi wa habari waliokuwa wanaandika hayo mambo walikuwa wanatishiwa vibaya sana.
Seriously, mimi nilikuwa naamini was just a political game, na ndipo hapa nakumbuka yale ambayo tuliongea sana hapa JF siku Magufuli anatangaza serikali kununua korosho!!!

Na kuna uwezekano mkubwa serikali iliuza kwa hasara zile korosho, na tena kama waliuza zote basi manake hawa jamaa kwa mbwembwe, angekuwa amepatikana potential buyer, kungewekwa hadi kipindi maalumu pale TBC!!
 
Ile biashara iliharibika kabisa, na korosho nyingi ziliooza. Siku Magufuli anatoka madarakani mambo mengi yatakuwa wazi.
 
Ile biashara iliharibika kabisa, na korosho nyingi ziliooza. Siku Magufuli anatoka madarakani mambo mengi yatakuwa wazi.
Hilo la kusema nyingi zilioza, nakubaliana na wewe kwa sababu hata wakati ule tulisema hapa kwamba, msimu wa korosho kwa nchi za Asia, umekaribia sana, huku Afrika Magharibi wakiwa njiani kufika kipindi cha mavuno, kwahiyo za kwetu lazima zikutie msimu!! Tena hawa jamaa wasiwe wamegawa jeshini wakazitafune huko!!!!
 
Mpwa itakua fitna tu za kumchafua Mwenyekiti wetu, taarifa zipo wazi kabisa kuwa walishalipwa na kwamba ambaye hajalipwa ni wale waliokua na madeni feki
Labda wale walioshindwa kuonyesha mashamba waliyolimia korosho nw wasio na account bank
 
Yaani mtu namdai ananizungusha kunilipa miezi na miezi leo anakulipa anaamua akunadi na kuanza kujisifia.
Pawepo na utaratibu wa kulipana na fidia pindi unapochelewesha deni la mtu.
Hii sio fadhila, nyau nyie
 
Kama RAIS ndiye katoa hizo bilion 20,

Hakika hiyo ni RUSHWA kwa Wakulima na Wadau wa KOROSHO.

Kwa nini iwe kipindi hiki cha kuelekea UCHAGUZI?

TAKUKURU, POLISI, TUME YA UCHAGUZI NA MSAJIL WA VYAMA VYA SIASA MKO WAPI?
Tukukuru na polisi ni jumuia za CCM
 
Hilo la kusema nyingi zilioza, nakubaliana na wewe kwa sababu hata wakati ule tulisema hapa kwamba, msimu wa korosho kwa nchi za Asia, umekaribia sana, huku Afrika Magharibi wakiwa njiani kufika kipindi cha mavuno, kwahiyo za kwetu lazima zikutie msimu!! Tena hawa jamaa wasiwe wamegawa jeshini wakazitafune huko!!!!

Na ole wake muandishi yoyote wa habari atangaze hayo mambo, yatamkuta ya Azory Gwanda.
 
Back
Top Bottom