Serikali imetoa Tsh. Bil. 20 kulipa madeni ya wakulima, Wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho

Serikali imetoa Tsh. Bil. 20 kulipa madeni ya wakulima, Wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho

19 Jul 2020
Mtwara, Tanzania



Serikali imetoa shilling bilioni 20 za kulipa madeni ya wakulima, wasafirishaji, wapuliziaji dawa na waendesha maghala ya korosho. "Rais Magufuli ametoa fedha hizi kwa ajili ya Tandahimba, Masasi, Mtwara na Kibiti kwa ajili ya waliokuwa wamelipwa nusu, waliolipwa kiasi na wasiolipwa kabisa.

Fedha hizi zitaanza kulipwa kesho asubuhi," Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametoa kauli hii leo (Jumapili, Julai 19, 2020) wakati akizungumza na wanachama wa Chama cha Msingi (AMCOS) cha Matogoro na wakazi wa Tandahimba mkoani Mtwara alikoenda kuhamasisha maandalizi ya msimu wa ununuzi wa korosho.

Chanzo: Azam TV
 
Asante wa kunyumba Bernard Membe joto la uchaguzi lapanda huko kusini, Waziri Mkuu apiga kambi na serikali ya CCM Mpya inakumbuka shuka dakika za lala salama wakati tayari wananchi wamesema Twende Membe Twende 2020

Muungano wa Upinzani umeleta hofu kubwa CCM Mpya

 
CCM imekufa vipande vipande, mambo yote anafanya Magufuli.

Wabunge wa CCM Mpya mtajibeba, chama siyo muhimu ndiyo falsafa ya wakuja ndani ya CCM iliyo na kina Dr. Bashiru Ally, Humphrey Polepole ndo maana "sifa zote zinakwenda kwa bwana yule asiyetajwa jina" - in Bernard Membe voice na CCM si lolote sasa mtu mmoja ndiyo kila kitu.

Ndiyo maana fedha zote zinaelekezwa ktk Maendeleo ya Vitu kama SGR reli, Stiegler's Gorge, Bombadier , Madaraja ya baharini, Flyovers, Stendi Mpya za Mabasi ukubwa wa Airport ya Dar es Salaam kona nyingi za Tanzania... kwa kifupi miradi ya fahari ya macho...

Lakini Maendeleo ya Watu kama kulipa wakulima haki zao za korosho, mishahara kwa watumishi kama waalimu, kujenga hospitali kubwa kama ile ya Bugando Mwanza kila wilaya za Tanganyika ikiwa imejazwa vifaa-tiba, madaktari, wafamasia, Nuclear-Imaging-Radiology staffs, manesi.... siyo kipaumbele cha CCM hii Mpya.

Polepole : " Wewe Si Kitu Mbele ya Hiki Chama"

 
Homa ya uchaguzi inapanda!!

Nawatahadharisha wananchi hawa wasije wakasahau kuwa kuna miaka mingine mitano baada ya uchaguzi hivyo wasifanye makosa.

Hii ndio faida ya kuwa na upinzani katika nchi vinginevyo haya huenda yasingetokea.

Nina hakika miongoni mwa wataofaidika na malipo hayo, ni pamoja na wafuasi wa CCM ingawa inawezekana baadhi yao ni sehemu ya watanzania wanaobeza upinzani.

Kimbembe kiko kwa wafanyakazi maana licha ya kutelekezwa,hata baadhi ya madeni yao bado hawajalipwa kwa miaka mitano sasa.

Siku tukija kupata Tume huru na tukawa na demkrasia ya kweli katika nchi yetu,basi nina hakika wananchi watakuwa ndio mabosi na sio watawala ila ipo siku.
 
Back
Top Bottom