Serikali imlipe Tundu Lissu gharama zake za matibabu

Humu ndani tupunguze roho mbaya hazina maana yoyote ile,mtu kapigwa risasi na wasiojulikana kaambiwa ukienda tu Muhimbili wanakumalizia sana mlitaka wakaombe kibali kwa nani?wakati mtu alikuwa anakimbiza roho yake
 
mtu kapigwa risasi na wasiojulikana kaambiwa ukienda tu Muhimbili wanakumalizia sana mlitaka wakaombe kibali kwa nani?wakati mtu alikuwa anakimbiza roho yake
Aliyemwambia hilo ni nani? Anayechafua jina la Muhimbili nani huyo?

Kazi ya madaktari Muhimbili ni kuua watu?

Kutishia kukamata ndege zilizonunuliwa kwa pesa za walipa kodi ndio roho.nzuri?
 
PTSD therqpy sii mchezo. Ni gharama kubwa sana. Na itaja kuwa gharama kubwa zaidi pale atakapopewa nyadhifa.

Masikini zile pyu pyu pyu, 😭Usimuombee hata adui wako.🙌🏾
 
Kwa hiyo anatakahe watu wafumbe macho wasijali taratibu zinavyotaka za malipo walipe tu bila kujali taratibu za kulipa?
Nimekuuliza swali ili utuambie hizo taratibu ambazo unadhani hajazifuata....

Na Je, unaweza kuonesha ushahidi wa serikali iwapo ilishawahi kumjibu Tundu Lissu kuwa hutalipwa madai yako kwa sababu hayana uhalali wa kisheria kwa sababu 1, 2, 3....?

Halafu jiulize maswali mengine rahisi tu kama;

√. Hivi kweli tunadhani Tundu Lissu mwanasheria mbobezi mpenda haki hajui sheria na taratibu zinamtaka afanye nini kwenye hili....?

√. Hivi kweli kwa ufahamu na akili zenu nyie kina Shotocan mnadhani Tundu Lissu mwanasheria anayeelewa sheria na taratibu anaweza kudai na kung'ang'ania haki yake iliyo nje ya sheria? Really...?

SIKILIZA BWANA Shotocan:

Acha ubishi usio na kichwa wala miguu ambao obviously umeujenga ktk msingi wa ujinga, chuki na ubinafsi tu....

Kila mtu anajua kuwa kinachofanyika si ishu ya kuwa HAKI zake "haziko kisheria" au "iko nje ya utaratibu"...

Bali anachofanyiwa Tundu Lissu na wengine wote wanaodai haki zao serikalini, ni chuki ileile waliyotaka kumuulia na ambayo wanatamani afe hata leo...

Wanaogopa kuwa wakimlipa, kila dai lake litapata uhalali wa kisheria ikiwepo kudai uchunguzi wa tukio lote la jaribio la kuuwawa kwake, madai kuwa Paul Makonda ndiye Kiongozi wa mauji yake nk nk...

Tumia kichwa na akili zako vizuri kufikiria. Usifugie nywele tu...
 
Naona umejaza uadhani nyingiiiiii
Jibu fupi tu ni je kilikuweko kibali cha wizsra ya afya yeye kwenda kutibiwa nje?

Hilo analijua mwenyewe kama kilikuwepo au la
 
Anaupiga mwingi kumbe ni changa la macho.
 
Naona umejaza uadhani nyingiiiiii
Jibu fupi tu ni je kilikuweko kibali cha wizsra ya afya yeye kwenda kutibiwa nje?

Hilo analijua mwenyewe kama kilikuwepo au la
Kwani rafiki ndugu Shotocan hiki unachokiita "kibali cha wizara ya afya" ni nini, kinakuwaje na kinatolewaje unadhani kwa uelewa wako....?

Mwisho, waambie wahusika wanaopaswa kutoa haki ya mtu huyu wamwandikie barua kujibu madai yake kuwa hayatalipwa kwa sababu ya hiki unachosema "kibali cha wizara ya afya" cha kwenda kutibiwa nje ya nchi....

Ni hivyo tu na ni rahisi kabisa.....

Au wewe Shotocan unaonaje kwenye hili..?
 
Madai yake ni ya 2017 ,serikali ya 2015 -2020 ndiyo iliyomdhulumu...Wewe unaitambua serikali ya 2020-2025?
 
Mwisho, waambie wahusika wanaopaswa kutoa haki ya mtu huyu wamwandikie barua kujibu madai yake kuwa hayatalipwa kwa sababu ya hiki unachosema "kibali cha wizara ya afya" cha kwenda kutibiwa nje ya nchi....
Madai kama yako kinyume taratibu hayana haja hata ya kujibiwa ni kuyatupa tu kwenye dustbin

Ndio maana maombi ya kazi wakiomba wengi huambiwa tu usippoata majibu jua hukufanikiwa

Huwa hawajibu kila bi ambalo ni rejected na kueleza sababu
 
na tulizochanga zilienda wapi?
 
Serikali ipo tayari kulipa goli la yanga au simba on the spot kwa cash siyo mkopo uwanjani lakini siyo raia wake aliyeumizwa na wahuni
 
Ni kwa sababu tu hujui lakini hujui kuwa hujui...

Taratibu zipi ambazo unadhani zinamzuia Tundu Lissu kupata haki zake...?

Au unakariri tu uliyokaririshwa na hao bwana zako bila wewe mwenyewe kutetea unachodhani unajua...?
hana haki na wala hawezi kulipwa hata sent moja ikiwa alikiuka sheria na taratibu za mbunge kwenda kutibiwa. Na kama hakukiuka, basi awasilishe stakabadhi na vielelezo vya ruhusa kulingana na utarabu wa idara za bunge na ikiwezekana aviweke wazi kwa uma ikiwa anaonewa🐒
 
Kwani Hospitali wanamdai?
 
Kaka yake alifuatilia taratibu zote alipokuwa kwenye matibabu, ila kwakuwa suala ilikuwa ni kumkomoa kwa kumtaja Magufuli kuwa ndio muhusika wa shambulio lake, wakawa wanamzungusha.

Ukweli ni kuwa Magufuli alijipa jukumu la kutoa kibali cha mtu kwenda nje ya nchi, lakini halikuwa jukumu lake kisheria, na aliitumia nafasi hiyo aliyojipa kinyume cha utaratibu kwa utashi wake binafsi. Usitake kuzungusha maneno sijui utaratibu, wakati tunajua kinachoendelea sio utaratibu bali ni kumkomoa Lisu maana hajinyenyekezi kwa viongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…