Serikali impe angalizo Jerry Silaa, namuona anaiingiza Serikali katika mgogoro mkubwa wa kulipa fidia!

Wazir bishoo anatafta sifa , Hana lolote Zaid ya makamera na Kiki .... Hii nchi mpak huko misenyi ina shida kubwa ya ardhi, badala ya kushawishi Bunge kutunga Sheria kupitia udhaifu wa mahakama na maafisa ardhi , mtu anaamua kufanya one man show na kuita makamera na machawa, haya mpak aje afike kwetu ikunguilipu lini
 
Uongozi wa awamu hii, mtu akipata kacheo tayari anajiona kamaliza, awe na cheo huko ccm kama mtu flani ndo kbs. Hawàjali katiba wala sheria inasemaje. Kiburi mtindo 1 kwa kwenda mbele. Inaitwa kuupiga mwingi ...tutafika tukiwa Trabant...dah!
 
WEWE PIA NI MIONGONI MWA WAVAMIZI WA VIWANJA
 
Ni law gani aliyoisoma huyu, basi mmupigishe hata introduction ya "Administrative Law"
 
Hiyo wizara ,ilianza kutulia kipindi cha Lukuvi wengine chenga
 
Kama sikosei, hii kesi huyo aliyevunjiwa alishinda kesi na eneo lipo kilonga wima Mbezi Beach.
Jambo la busara ni serikali kukataa rufaa na sio kutumia mabavu.
Hadi kufikia hatua za kuvunja lazima rufaa zilishakatwa na kufika mwisho.
 
Mmmh ndugu yangu hakuna haki mahakamani si ya chin si ya juu ya kulia wala kushoto.... inshu hizi za ardhi mabaraza ya kata yapewe nguvu yanaujua ukweli sana mana physical wanajua location na wanaifikia kabisa mahakama inapelekewa stor tu
Mabaraza ya Kata hawajui kitu , wale ndio wala rushwa wakubwa na chanzo cha migogoro ya Ardhi .
 
sheria ya ardhi iko wazi. mwenye hati ya kwanza halali ndie mmiliki.

maafisa ardhi wahuni huwa wanatoa hati halali hata kwa watu kumi tofauti.

hapo yule wa kwanza ndie anakuwa mmiliki

Hivi Mfano unejenga nyumba umekuwa nayo Miaka 20 halafu anakuja Mtu anakuambia hiki ni Kiwanja changu tangu Miaka 20 iliopita!
Anataka kubomoa utafanyaje?
Unamuonyesha hati sababu Uliuziwa yeye anakuonyesha Offer au hata Pia Hati nae!
Na Ukute Offer yake ndio imetangulia ila kujenga Umejenga wewe utafanyaje?
Na Kwa Miaka yote 20 Hajawahi Kuja kulalamika!
 

hapo utapeleka kesi kwenye baraza la ardhi kata, kisha mtaenda baraza la ardhi wilaya.

huko wilayani ofisi ya afisa ardhi itaitwa na mahakama ije ithibitishe uhalali wa documents zenu, kama hakuna feki.

zikionekana zote halali. ndipo watatazama nani alikuwa wa kwanza kupewa ofa na kulipia kiwanja hicho.

ikionekana wewe uliejenga hukuwa wa kwanza. nyumba yako itavunjwa

KUJENGA WA KWANZA HAKUKUPI USHINDI WA KIWANJA MAHAKAMANI
 
Kubomoa hawajafanya vizuri maana ni kurudisha uchumi nyuma.

Hapo hata kama aliyejenga kiwanja siyo chake ,wangekaa chini na mwenyewe wakacompasate na kumrudishia atleast gharama za ujenzi 50% na wakaliacha ghorofa kutumika na mwenyewe(Original).
 
As long siyo kiwanja chako halali,hata ukikaa nacho miaka mia bila kufuata utaratibu wa kisheria, mwenye kiwanja halali akijitokeza imekula kwako!!
 
Mwache hivyo hivyo tu Mkuu mwisho wa haya sio mbali ngoja mmoja wa wahanga ende Mahakamani kupinga agizo lake ndio zitamkaa sawa.

Nilimueleza mtu mmoja mahala hili jambo akaniulza ila Jerry si ni wakili mwenzenu kwani haya hayajui?, nilitoa jibu moja tu.

''Ukilewa unaweza ukasahau hata jina lko''

Kifupi ni kuwa hana hayo mamlaka na mamlaka zinamuangalia tu.

Dawa ni kumshtaki kwenye nafasi mbili, kama waziri na kama mtu binafsi, na sababu zipo pia. Maana kwanza mtu yoyote mwenye mamlaka akifanya jambo nje au kinyume na mamlaka au taratibu zinazomhusu anaweza kuwqjibishwa yeye binafsi na sio kama mwenye mamlaka.
 
Huyu ni showoff Minister very soon Madame President atanpiga chini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…