Tuache ushaabiki maandazi, mimi siyo muumini wa kuonewa au kuona mtu anamuonea mwenzie. Huyu Slaa sidhani km ni kichaa hadi asimamie zoezi Hilo bila kibali cha mahakama. Tangu wanaanza kubomoa ni nani alimskia yule mama akisema alishinda kesi mahakamani.
Tunaambiwa kesi imedumu mahakani kwa miaka 20, unadhani ni kitu gani kilichelewesha hukumu hadi ije iwe leo. Watu wenye vijisent wawe na tabia ya kuheshimu watu masikini kwani "haki ya mtu huwa haipotei bali hucheleweshwa tu". Zoezi liliosimamiwa na askari police tena wengine wa vyeo vya juuu mtu anakuja kusema ni mambo ya family friends eti kwamba huyo mama kaonewa. Guys "kitanda usichokilalia huwezi kujua kunguni wake", vipi huyo mama mjane aliekuwa amedhulumiwa kiwanja ndo angekuwa MAMA yako huku mkiishi upangajini kwa tabu.
Mimi ninaamini kilichofanyika ni matokeo ya maamuzi ya mahakama na siyo blaa blaa za mleta mada, km kaonewa bado nafasi anayo ya kwenda mahakamani.
Said: BANDOKITITA