Kiukweli katika waziri ambaye ataiweza hii wizara ni Jerry Silaa. Sababu kibwa anafuata sheria na amesoma sheria. Nimeona mfano wa sheli pale mikocheni kwa Rupia, Sayore na Mama Tibaijuka pale kuna suala la rushwa mpaka kibali kikatoka kisheria cha kujenga sheli.
Jerry ilikuwa ni kuionesha mamlaka kwamba rushwa imefanyika mamlaka zingine zichukue hatua kama Takukuru.
Kuna suala la Tarura kukodisha road reserve na wafanyabiashara kuje ga majumba, showroom za magari, baa, majiko ya chips hii imetokea Msikiti road mikocheni maarufu kama kwa Warioba. Jerry amemuambia mkurugenzi ashirikiane na Tarura waondoe wale waru kwenye road reserve ambayo ilipaswa kuwa njia ya waenda kwa miguu kuna mtu kaweka car wash, baa, chips na takataka zinhinie ikiwemo showroom ya magari.
Jerry silaa anapaswa kuungwa mkono atusafishie mipango miji. Kuna barabara ya tegeta inahitajika iwe na service road kuanzia mwenge mpaka bunju lakini pale kwa ndevu watu wamejenga mpaka mbele ya mawe na notice walishapewa na Tanroad miaka 7 iliyopita ni utekelezaji tuu unakwama wa kuvunja na kupata nafasi ya barabara mana inasemekana mwendokasi inakuja na washaanza kujenga ofisi pale vilima vya Lugalo kambini.
Barabara ya kawe inahitajika NHC anapomaliza ujenzi wa magorofa ya mama samia housing projects basi na kawe isafishwe yote iwe na setvice roads waliojenga mbele ya road reserve wavunjiwe wote bila huruma.
Suala la kumpa mwamposa aende kule nyuma ya shule ya msingi kawe B halikubaliki kwani ataenda kuleta kelele kwa wanafunzi wa shule za serikali na feza kwa ujumla. I efika wakati mwamposa anajiweza atafute eneo lake hata lile alilojimilikisha waziri mabula na mwinyi angepewa mwamposa upande wa Kawe club akatoka kanisa moja kama St peterburg cathedral.
Matumizi ya atdhi ni suala inabidi lizingatiwe bila huruma haiwezekani sasa hivi mbezi ya chini mpaka bahari beach kote ni fremu tuu. Huu sio ukuaji wa uchumi ni uharibifu wa mazingira. Hatuwezi kuwa na eneo moja ni maduka ya nguo tuu kila wilaya na sio kila anayejisikia anajenga fremu mbele.