DOKEZO Serikali imsaidie Mtoto huyu anayedaiwa kulawitiwa na Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza

DOKEZO Serikali imsaidie Mtoto huyu anayedaiwa kulawitiwa na Mlinzi wa Kanisa Katoliki Sinza

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
katika moja ya Shule zilizopo Sinza kama sijakosea inaweza kuwa ni pale Mapambano (sija uhakika na jina la shule)
Mkuu Rudi upya ukakusanye data hapo kuna ukakasi kidogo there's doubt in your story, you have to disclose everything kuanzia Shule anayosoma na kila kitu ili iwe wazi sasa unaposema sijui au Sina uhakika hapo unaonekana hauna uhakika na taarifa yako, aidha umesimuliwa na mtu haumjui huyo mtoto ndio ukaamua kuibeba story na kuileta huku kaongee nao vizuri wahusika alafu uje ufanye updates kwenye huu uzi
 
Duh! Mzee wa makasiriko. Adhabu ulopendekeza itatekelezeka kivipi? Yani kosa linalipwa kwa kutenda kosa hilo hilo tena mara saba? Je mtoa/mtekelezaji wa adhabu (Yule atakayelawiti mara saba) akifariki baada ya miezi mitatu hiyo adhabu mwisho wake itakuwaje? 😠 😠 😠
Kwani makosa mengine mfungwa akifariki adhabu huendelea au hufa?
Ukipata jibu pigia mstari.

Hakuna makasiriko tunataka kuondoa ubakaji na ulawiti kwenye jamii za kitanzania kwa adhabu kali na zenye kudhalilisha pia wahusika.

Haiwezekani mtu kalawiti halafu yeye abaki na sealed nyuma,haiwezekani aisee..
 
Huyo mlinzi ashukuru Mungu katenda ukatili kwa mtu mnyonge....

Yaani umlawiti mtoto wangu na nikujue halafu uendelee kutembea, kuona, kusikia, kula, kuwa na uume...nooo!
Kwa ubabe wako huo una msaada gani kwa mwathirika maana mleta mada kasema ni mtoto yatima mama yake hana uwezo wa kupambana na hao maparoko wa sinza.
 
Nikiwa kama raia mwema na mtumishi wa Kanisa Katoliki lililopo Sinza nimeona sio vema nami nikae kimya wakati kila wiki naenda Kanisani kumuomba Mungu kisha niache familia iteseke wakati nina nafasi ya kupaza sauti na haki ikatendeka.

Kuna mtoto ambaye nafikiri anasoma darasa la 5 au la 6 katika moja ya Shule zilizopo Sinza kama sijakosea inaweza kuwa ni pale Mapambano (sija uhakika na jina la shule).

Nilianza kumjua mtoto huyo kwa kuwa amekuwa akifika mara nyingi kwenye kwaya ya Kanisa hilo (Dar es Salaam).

Huyu mtoto ni wa kiume, alianza kuwa muumini mzuri wa Kanisa bada ya kuletwa na mzazi wake, mama mtu alifanya hivyo baada ya kufiwa na mumewe ambaye alikuwa ni Mwandishi wa Habari.

Mara baada ya msiba huo, kwa kuwa kiuchumi mama mtu hakuwa vizuri, akaamua kusogeza familia yake karibu na Kanisa ili angalau apate msaada.

Hivi karibuni ilibainika mtoto huyo amelawitiwa na mmoja wa Walinzi wa Kanisa hilo la Roma lililopo Sinza, baada ya mama mtu kubaini hilo (haikujulikana kama ni mara ngapi mtoto kafanyiwa hivyo na kama ni mlinzi peke yake au kuna mwingine), suala likafikishwa hadi Kituo cha Polisi Mabatini.

Mtuhumiwa akakamatwa na kuwekwa ndani kwa muda, lakini baada ya viongozi wa Kanisa pamoja na Viongozi wa Kwaya kufika kituoni hapo, haijulikani nini kilichoendelea lakini mtuhumiwa akaachiwa kwa dhamana huku kukiwa hakuna taarifa yoyote ya maana inayoendelea.

Licha ya kwanza vipimo vya Kitabibu kutoka kwa Daktari kuonesha wazi kuwa ni kweli Mtoto alifanyiwa ukatili huo wa kulawitiwa, hakuna kinachoendelea na dalili zilizopo ni kuwa viongozi wa Kanisa, Askari wa Kituo cha Polisi Mabatini wanataka kulizima suala hilo kinyemela.

Mtoto yupo tu nyumbani na mama yake, ameathirika kisaikolojia, mama mtu naye hajui cha kufanya kwa kuwa hana uwezo wa kupambana na watu wanaomzunguka mtuhumiwa.

Ushahidi wa tukio hili wanaujua watu wa karibu na kanisa hilo hasa Watumishi kuanzia wafanyausafi na hata baadhi ya mjirani pia wanajua.

Naomba ujumbe huu uzifikie Mamlaka husika kwa kuwa tukio tunalijua mwanzo mwisho lakini tuna hofu ya kujitokeza na kukemea kwa kuwa kama Kituo cha Polisi Mabatini, Daktari wa Hospitali ya Palestina (Sinza), Kanisa wote hawataki lijulikane kuna nini nyuma ya pazia na kwa nini?
Mleta mada waziri keshajibu na kaomba umpe namba za simu anasubiri msaada wako. Tafadhari mkuu kamilisha kazi njema uliyoianza. Ubarikiwe na Bwana.
 
Mtoto wa darasa la sita muda wa kwenda kanisani kila siku kuimba kwaya anaupata wapi na kwa nini anaruhusiwa kushinda mazingira ya nje ya nyumbani bila uangalizi wa mzazi, ifike mahali wazazi tuwe walinzi wa hawa watoto sio kuwaachia tu dunia imeharibika

Chanzo cha ukatili ni sisi wazazi kutokua responsible kwa watoto wetu

Nampa pole huyo mama.
Kwani shule wanashinda huko??? Kwahiyo unataka asiende kanisani wew inaelekea hujui kanisa wala msikiti
Kwani akitoka shuleni saa tisa hawezi kwenda kanisani??
Kwani kwenda kanisani nikosa kwa mzazi???
Mimi nafikiri ungemsifu kuwa amechagua fungus jema maana elimu bila Mungu haina maana
 
Kanisa Katoliki linaficha sana waovu mapadri wanalawiti watoto lakini hawachukuliwi hatua zaidi ya kuhamishwa vituo vya Kazi, ata like sakata la paroko kumbaka mtoto kule Moshi limezimwa kinyemela
 
Kwani shule wanashinda huko??? Kwahiyo unataka asiende kanisani wew inaelekea hujui kanisa wala msikiti
Kwani akitoka shuleni saa tisa hawezi kwenda kanisani??
Kwani kwenda kanisani nikosa kwa mzazi???
Mimi nafikiri ungemsifu kuwa amechagua fungus jema maana elimu bila Mungu haina maana
Najua kanisa, na huwa naenda kanisani siku za jumapili na watoto. Ibada ikiisha tunarufi nyumbani, jumamosi mmoja anaenda mafundisho kanisani nampelaka nasubiri masaa mawili akitoka ananikuta mlangoni namsubiri tunarudi nyumbani

Unaponiambia mtoto anaenda aknisani kila siku najiuliza akitoka shule hana muda wa kufanya homework, kusaidia vikazi vichache vya nyumbani na kupumzika?

Kama anataka kuimba kwaya asubiri umri sahihi ukifika ataimba kwaya akiwa anajitambua na anaweza kujilinda
 
Ila sisi watanzania aisee ni watu wa ajabu mno. Huyo mama anasingizia fedha, hili jambo linahitaji fedha kupaza sauti? Siku hizi njia za mawasiliano zipo nyingi na wala hawatozi fedha kwa mambo kama haya.
Mkuu usimlaumu sana tonatoufationa uelewa. Na watanzania wengi hawana elimu ya uraia kiasi hata haki zao za msingi hawazijui na hata wakizijua hawajui wazapate wapi na kwa kupitia njia gani. Kwa sasa hivi asaidiwe tu hayo mambo mengine yaje baadae.
 
Mkuu usimlaumu sana tonatoufationa uelewa. Na watanzania wengi hawana elimu ya uraia kiasi hata haki zao za msingi hawazijui na hata wakizijua hawajui wazapate wapi na kwa kupitia njia gani. Kwa sasa hivi asaidiwe tu hayo mambo mengine yaje baadae.
Ni kweli. Dunia ina watu wa kila aina hivyo nisihukumu sana. Nimekumbuka kile kisa cha wanawake kupewa dawa ya kupunguza unene, na dawa yenye inabidi ipakwe kwenye uume, ndiyo iingizwe kwa njia ya uke wake. Na walikuwa wanaenda wengi! Nimefanya utafiti nimegundua kumbe hii njia waganga wa kienyeji wanaitumia sana ''kutibu'' dada zetu.
 
Hongera sana mama, upo active sana kushughulikia matatizo ya jamii.
Wenzako akina Nape Nnauye wanatumia JF kwa kujificha kama bange.
Si vibaya wakaiga mema yako.
Hata swala la ushoga ni kama vile Rais kaamua kulibariki ksbu hakuna katazo wala Sheria Kali iliyotungwa kudhibiti hii tabia, huyu mama Yuko poa lakini viongozi wenzake hawana time kabisa, wanakomaa na ufisadi tuu, haya mambo yanakera sana!
 
Huyo mlinzi ashukuru Mungu katenda ukatili kwa mtu mnyonge....

Yaani umlawiti mtoto wangu na nikujue halafu uendelee kutembea, kuona, kusikia, kula, kuwa na uume...nooo!
sio tatizo je saikolojia yako itafuta tukio ukikumbuka ndio mtoto wako kashafanyiwa
 
Kanisa lihangaike kuficha uovu wa mlinzi? Waandishi mpo nendeni mkalete facts. Kama ni kweli wahusika wote wawajibike
 
Ujumbe umetufikia. Ahsante Sana kwa moyo wako wa kutoa taarifa.

Haya, huyo mzazi mpe namba yangu ya 0765345777 anitumie ujumbe hata Sasa hivi aseme tu "mimi ni mama wa sinza ambapo mtoto wangu amekatiliwa". Nitamtambua.

Shukrani 🙏🏾
Heshima yako Muheshimiwa,kama hutojali naomba baada ya hili tukio kukufikia mezani kwako urudi kwenye huu uzi utueleze limefika wapi.

Haya mambo yamekuwa mengi sana kwenye jamii ni kama watu hawajali tena em ninyi kama wizara jitahidini kuwahimiza polisi kuharakisha uchunguzi na mahakama zitoe hukumu mapema ili watakaojisikia kujaribu watishike waache huu unyama.
 
Ujumbe umetufikia. Ahsante Sana kwa moyo wako wa kutoa taarifa.

Haya, huyo mzazi mpe namba yangu ya 0765345777 anitumie ujumbe hata Sasa hivi aseme tu "mimi ni mama wa sinza ambapo mtoto wangu amekatiliwa". Nitamtambua.

Shukrani [emoji1488]
Mungu akubariki sana Dkt Gwajima.
Nakuombea upate nafasi kubwa zaidi ututumikie Watanzania kwa mapana zaidi.
Unaweza hakika.
 
Huyo mlinzi ashukuru Mungu katenda ukatili kwa mtu mnyonge....

Yaani umlawiti mtoto wangu na nikujue halafu uendelee kutembea, kuona, kusikia, kula, kuwa na uume...nooo!
Mi ningemchiinja mwenyewe walah
 
Makonda yupo sahihi sana kuhusu si mahakama tu bali mchakato mzima wa upatikanaji haki kwa wasionacho nchini umeoza.

Kama siyo kupitia kwa huyu Mama Waziri anayejitolea basi hakuna kitu kitafanyika hapo!

BTW:Ni aibu sana kanisa kushiriki dhulma hii tena kwa mtoto.
 
Back
Top Bottom