Hivi karibuni ilibainika mtoto huyo amelawitiwa na mmoja wa Walinzi wa Kanisa hilo la Roma lililopo Sinza, baada ya mama mtu kubaini hilo (haikujulikana kama ni mara ngapi mtoto kafanyiwa hivyo na kama ni mlinzi peke yake au kuna mwingine), suala likafikishwa hadi Kituo cha Polisi Mabatini.
Mtuhumiwa akakamatwa na kuwekwa ndani kwa muda, lakini baada ya viongozi wa Kanisa pamoja na Viongozi wa Kwaya kufika kituoni hapo, haijulikani nini kilichoendelea lakini mtuhumiwa akaachiwa kwa dhamana huku kukiwa hakuna taarifa yoyote ya maana inayoendelea.