Serikali imuondoe Paul Makonda haraka kabla mambo hayajaharibika. Tamko lijalo linaweza kuathiri nchi pakubwa

Serikali imuondoe Paul Makonda haraka kabla mambo hayajaharibika. Tamko lijalo linaweza kuathiri nchi pakubwa

Yaani mnataka kutuaminisha kuwa Makonda ni One man army?? Hao wenzake ni kina nani?? Tulieni tu jamani mambo haya yatakwisha ni upepo wa kisulisuli tu utapita
 
Chadema mnauwana
Screenshot_20200201-212750.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya tangazo la Serikali ya Marekani kumzuia Makonda na familia yake kupata visa ya Marekani Kuna uwezekana mkubwa huo ndiyo ukawa mwisho wa Makonda kisiasa.

Tangazo hilo halijatoa Picha nzuri kwa uongozi wa awamu ya tano na ili kurudisha heshima na mahusiano hayo tena ni Makonda kuondolewa katika nafasi ya Mkuu wa mkoa haraka Sana.

Wamerakani watakawa wametuma makachero wao ndani ya nchi Kama majasusi bila tz kujua na uwezekano wamekuja Kama watalii na kukusanya habari nyingi Sana za ndani ya mifumo ya Serikali.

Ni wakati umefika RC aondoke haraka katika nafasi hiyo.

Ni aibu kubwa Sana kwa nchi kwa Tangazo Hilo.
Hakuna kitu kama hicho, hata nafasi yako inakusuta kwa unafiki! Toka lini ukawa mpinzani wa hii awamu? Au unataka watu waanze kuongea muwakamate?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya tangazo la Serikali ya Marekani kumzuia Makonda na familia yake kupata visa ya Marekani Kuna uwezekana mkubwa huo ndiyo ukawa mwisho wa Makonda kisiasa.

Tangazo hilo halijatoa Picha nzuri kwa uongozi wa awamu ya tano na ili kurudisha heshima na mahusiano hayo tena ni Makonda kuondolewa katika nafasi ya Mkuu wa mkoa haraka Sana.

Wamerakani watakawa wametuma makachero wao ndani ya nchi Kama majasusi bila tz kujua na uwezekano wamekuja Kama watalii na kukusanya habari nyingi Sana za ndani ya mifumo ya Serikali.

Ni wakati umefika RC aondoke haraka katika nafasi hiyo.

Ni aibu kubwa Sana kwa nchi kwa Tangazo Hilo.
Hakuna makachero wowote! Akitangaza kuwasaka mashoga, au kupima tezi dume kila mtaa, kupakazia watu wauza madawa hadharani, wakipimwa mkojo, nchi nzima inatangaziwa, alikuwa akifanya kifichoni? Na haya yote ndio uvunjaji wenyewe wa haki ya binadamu, kila mtu awe na tatizo lolote au la, ana haki ya kujisitiri (privacy). Sisi tunashangilia kudhalilishana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimsingi makonda siyo msemaji wa serikali hivyo na wao wameonyesha udhaifu mkubwa Sana ۔makonda Ni mkuu wa mkoa huwezi kutoa tamko Kama hii kisa mkuu wa mkoa but kwa kuwa imetoke Ni vyema akachia ngazi pia pro kabudi apunguze majibu ya haraka haraka hata Dem ukimtongoza anajibu subiri kwanza nifikirie
 
Iwapo human rights ni kutetea 'mapunga' . Tutasimama naye....acha wampige ban.... .. Marekani kitu gani?
Acha upotoshaji!! Kuna viongozi walishatoa kauli kali juu ya mashoga, na wengine kupelekea kuuawa, lakini hawakuzuiliwa kuingia USA, ije iwe yeye tena kwa kauli zile za kitoto?!! Wafuatiliaji wa mambi wanajua kuna mengi juu ya hii ban!! Acha kuja na hoja dhaifu hizo!!
 
Makonda atazid kupewa nafasi ya juu, chuki zinazotengenezwa juu yake kwa Tanzania hazina mashiko....anayemlaumu Makonda bhas atakuwa ana element za ushoga ndani yake.
 
Hatuwezi geuza mgogoro wa MaKonda na Marekani kuwa mgogoro wa kitaifa. Yeye makonda aumalize yeye mwenyewe
 
Imebaki Makonda Makonda, tuelezane ukwel mkuu wa mkoa gan anapiga kaz kama Makonda? Masuala ya sijui mauaji, sijui kitu gani, nani ana evidence aweke hapa? Na nani kakuambia nchi inaweza tu kwensa bila baadhi ya vichwa kukatwa? Watu wanataka kutetea Marekani.....wanalifaham vzur kwel taifa la Marekan au wanaongea emotionally.....vurugu zote dunian Marekan ndo anazozianzisha sasa kama mtu hajui....leo watu ohh Makonda....jitahidin kujifunza kuendana na wakat...Marekan watabaki kuwa wao...kwa nafasi yao.....Spiritually the stage is known.
 
Wampe ubalozi hata wa malawi akakae huko, kitaa hapa wengi wanamsubiri atoke hiyo nafasi aone dunia tambara bovu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana.

Kumpa ubalozi mtu mwenye madoa hivi ya haki za binadamu ni kuushusha hadhi ubalozi wa Tanzania.

Nawaheshimu mabalozi wa Tanzania kama watu wenye weledi. Hata kama wana mapungufu, si kama haya ya kusababisha diplomatic war na Marekani.

Nazungumzia mabalozi kama balozi Benjamin William Mkapa, balozi Ali Hassan Mwinyi, balozi Salim Ahmed Salim, balozi Augustine Philip Mahiga, balozi Ami Mpungwe, balozi Jaka Mwambi, balozi Mustapha Nyang'anyi, balozi John Samuel Malecela, balozi Nsilo Swai, balozi Paul Milyango Rupia, balozi Abbas Kleist Sykes, balozi Crispin Mbapila, balozi George Magombe, balozi Wilbert Kumalija Chagula, balozi Juma Volter Mwapachu, balozi Juma Maharage na mabalozi wengine wengi wa kada hiyo.

Sasa unataka kumuweka Makonda kwenye kada hiyo baada ya uchafuzi alioufanya, hawa wazee wote wenye heshima zao duniani nao wawe kundi moja na Makonda?

Utaushusha hadhi sana ubalozi wa Tanzania.

Najua ubalozi wa Tanzania ushahuka hadhi, lakini usitake kuushusha zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom