Serikali imuondoe Paul Makonda haraka kabla mambo hayajaharibika. Tamko lijalo linaweza kuathiri nchi pakubwa

Serikali imuondoe Paul Makonda haraka kabla mambo hayajaharibika. Tamko lijalo linaweza kuathiri nchi pakubwa

.
Ndugu wana JF, kila mmoja amesoma tamko la hasira la Marekani juu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ndugu Paul Makonda.

Kwa desturi za USA, mlengwa mkuu hapo ni Rais Magufuli na serikali yake, walichofanya ni kuipima serikali yetu itamfanya nini Makonda baada ya wao kutangazia Dunia kuwa hawataki akanyage Marekani.

Makonda asipoondolewa, tujiandae kususiwa na Dunia nzima, maana Marekani ndio taifa lenye nguvu za kila aina Duniani.

Hata mataifa yanayojitegemea Kiuchumi yana ufyata kwa Marekani, sembuse sisi tunaojitegemea kwa asilimia 56%? Huku 44% tukitegemea kusaidiwa na Mabeberu?

Kama unajua trend reading, Ubalozi Marekani walikuwa wanatoa taarifa inayofanana na balozi nyingine kama ubalozi wa Ulaya, Uingereza nk.

Usishangae ndani ya siku chache ukawasikia washirika wa Marekani nao wakimpiga marufuku Makonda kukanyaga huko.

Kama serikali ikizembea kumfukuza Kazi Makonda ili kujisafisha, usishangae likatoka tamko la kuzuia misaada kwa Tanzania, halafu tuwekewe na vikwazo ikiwa ni pamoja na kuzuia watalii wasije Tanzania kwakuwa ni nchi hatari kiusalama.

Wazungu wanaweza kutukumia vyovyote, hambo la msingi na haraka ni kumuondoa Makonda ofisini na kuteua mtu mwingine atakaefanya tofauti.

Chonde Chonde washauri wa Rais Magufuli, tunawapenda sana na tunaipenda serikali yetu, Makonda Mmoja asiingize nchi kwenye mgogoro wa Kidiplomasia.

Sent using Jamii Forums mobile app


Jr[emoji769]
 
Doh


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Makonda atazid kupewa nafasi ya juu, chuki zinazotengenezwa juu yake kwa Tanzania hazina mashiko....anayemlaumu Makonda bhas atakuwa ana element za ushoga ndani yake.

Mkuu sisi waTanzania ndio tumemlaumu makonda ? mbona mmejificha kwenye kichaka cha ushoga ? mbona hamtaki kujifikirisha mambo mengine ? Daah hapa ndio huwa nakuja kuamini kwamba kila mtu ana uelewa wake . Bashite alivyo na kiherehere vile ingekuwa ushoga pekeake angeongea tayari, kakaa kimya kaufyata, guilty conscience ndio inayomkalisha kimya saivi, he is stranded, alafu wazungu ni washenz hawana shida na makonda kuna lao wanalitafuta na walijua wakichomekea na ushoga mtakomaa hapo hapo na kweli mmejaa,


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Waendeleze Mipango Yao Ya Kutumia Policcm,vikundi Vya Unyanyasaji Na Uuaji Kutunyanyasa Watu Wa Vyama Vingine Ikibidi Watumalize Kwakuwa Ufahamu Wao Mdogo Wanadhani Watakuwa Wamemaliza Fikra Mbadala,wafanye Uhuni Wao Wa Miaka Yote Kwenye Chaguzi
 
Kimsingi makonda siyo msemaji wa serikali hivyo na wao wameonyesha udhaifu mkubwa Sana ۔makonda Ni mkuu wa mkoa huwezi kutoa tamko Kama hii kisa mkuu wa mkoa but kwa kuwa imetoke Ni vyema akachia ngazi pia pro kabudi apunguze majibu ya haraka haraka hata Dem ukimtongoza anajibu subiri kwanza nifikirie
USA huwa wanadeal na mtu specific ndiyo maana ameguswa yeye
 
Baada ya tangazo la Serikali ya Marekani kumzuia Makonda na familia yake kupata visa ya Marekani Kuna uwezekana mkubwa huo ndiyo ukawa mwisho wa Makonda kisiasa.

Tangazo hilo halijatoa Picha nzuri kwa uongozi wa awamu ya tano na ili kurudisha heshima na mahusiano hayo tena ni Makonda kuondolewa katika nafasi ya Mkuu wa mkoa haraka Sana.

Wamerakani watakawa wametuma makachero wao ndani ya nchi Kama majasusi bila tz kujua na uwezekano wamekuja Kama watalii na kukusanya habari nyingi Sana za ndani ya mifumo ya Serikali.

Ni wakati umefika RC aondoke haraka katika nafasi hiyo.

Ni aibu kubwa sana kwa nchi kwa tangazo hilo.
Kuzuiwa kuingia Marekani ni hatua za awali tuu.... Kuna mambo kadhaa yatafuata
. kuongeza kwa list ya wazuiwa
. makonda kutangazwa kukamatwa kama akitoka nje ya Tanzania ili akashtakiwe the Hague
. mtu mwingine muhimu na mkubwa kabisa kuunganishwa kwenye list
. vikwazo kuongezeka

Jr[emoji769]
 
Bashiru ameshaeleza makonda anaujinga mwingi lkn mgawa vyeo kamng'ang'ania na ili kuonesha anaimudu marekani anaweza kumpandisha cheo kabisa. Ndege wafananao....
 
Baada ya tangazo la Serikali ya Marekani kumzuia Makonda na familia yake kupata visa ya Marekani Kuna uwezekana mkubwa huo ndiyo ukawa mwisho wa Makonda kisiasa.
Makonda hawezi kushuka kisiasa kwa kunyimwa viza,kwani marekani ni peponi?
Hakuna cha wapelelezi wala nini,ni fitna za Zitto na lissu,ambao wanakumbatia ushoga
Hili nalo litapita,sijui watakuja na gia gani
 
Kusikia Kwa Kenge Hadi Atoke Damu Puani Na Masikioni
Mbaazi Ukikosa Maua Husingizia Jua
 
Makonda hawezi kushuka kisiasa kwa kunyimwa viza,kwani marekani ni peponi?
Hakuna cha wapelelezi wala nini,ni fitna za Zitto na lissu,ambao wanakumbatia ushoga
Hili nalo litapita,sijui watakuja na gia gani
Kama huoni tatizo la Makonda na boss wake ni kwa sababu wewe ni kipofu.
 
Back
Top Bottom