Serikali imwangalie Prof. Assad isimwache ateseke hivi. Huyu jamaa hayupo sawa

Unaweza kutupatia ripoti zake kuhusiana na ukaguzi miradi ya NHC na nssf na mwenendo wa mifuko ya hifadhi za jamii
 
Sisi wakristo tunafundishwa kusamehe na kua usipomsamehe mtu hata wewe hutasamehewa na Mungu, angekua ni mkristo anayeisoma bible na kuielewa angeshasamehe

Huwezi samehe kitu kama hiki. Unasemehe individuals siyo mfumo ... mfumo wetu ni mbovu unatakiwa kurekebishwa. Kusamehe mfumo mbovu ni kuhalalaisha dhuluma kwa Taifa zima ... hii ikimaanisha kuwa at some point kila Mwananchi ataathirika.
 
Muigai...
Humjui Mussa Assad.
 
MAKAFIRI SIKU ZOTE HAMTAKI WATU WADAI HAKI ZAO,HAKUNA SEHEMU HATA MOJA AMBAPO PROF ASSAD KALALAMIKA.KILICHOFANYIKA NI YEYE KUONDOLEWA KINYUME KWA KATIBA,NA NI HAKI YAKE KUPIGANIA HAKI YAKE...

KAMA KUDAI HAKI NI KULALAMIKA BASI WACHA NA IWE HIVYO.
 
Na

Naona una hasira sana baada ya babako Asad kuzodolewa kwa kulialia kama mtoto
NI SEHEMU GANI AMBAPO ASSAD KALALAMIKA KUHUSU KUONDOLEWA KWENYE HIKO CHEO ZAIDI YA KUDAI HAKI ZAKE??
 
Hivi ndugu yangu uliisikiliza ile interview yake na Kikeke?
Maandiko ya wachangiaji wengi yanaendeshwa na hisia na chuki walizonazo sijui hata za kitu gani.Sijawahi kumsikia Prof Assad akilalamika ajira au kurudishwa kazini.Kesi ya kikatiba alifungua Zitto Kabwe na hukumu ya mahakama kuu ilitoka kuthibitisha Katiba ilivunjwa kuondolewa kwa CAG Assad.Halafu Prof sio mtu mwepesi kama unavyomfikiria.Yuko vizuri na ana connection na heshima kubwa kimataifa.Yeye kubakia Tanzania na kuamua kufundisha chuo kikuu cha kiislamu, ni moja katika mikakati yake ya kutengeneza wema unaoendelea.
 
Jitahidi basi kuwa mkweli basi,huyu mtu amepata msiba wa kufiwa na mkewe na ndilo eneo pekee kwenye mahojiano alishikwa na uchungu alipokuwa akihojiwa kuhusiana na huo msiba.
Hii nchi imekuwa ya kishetani sana, wewe unayeongea huu utumbo huna unachoweza kushindana na Prof. Assad, ni kweli alionewa na mahakama imethibitisha. Hili ni funzo kwetu sote kwani aliyemuonea hayupo,yeye Prof. yupo hatujui kwa nini yeye hayupo japo inawezekana ikawa ni majibu kwa yale aliyowatendea wenzie na wao wakamuachia aliye juu, mhukumu wa haki.
 
Prof anateseka?

Au afya ya akili?
 
CAG akistaafu, kuna asilimia fulani anaendelea kiupata hadi kifo. yeye anapata? kama hapati, ana haki ya kulalamika. kama anapata, nitamshangaa sana.
 
Unaweza kutupatia ripoti zake kuhusiana na ukaguzi miradi ya NHC na nssf na mwenendo wa mifuko ya hifadhi za jamii
Nikupatie mimi tena?hizi si ni public reports ambazo hata darasa la kwanza B anaweza kuzi-acess. au ulimaanisha nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…