ThnkingAloud
JF-Expert Member
- Sep 13, 2017
- 546
- 564
Wanyonge ni watu gani katika nchi hii? Nani aliwafanya wawe wanyonge? Magufuli alifanya nini kuondoa unyonge wao? Hizo ni kauli za ALIYE JUU MNGOJE CHINI badala ya kumfuata huko huko juu.Huyu Assad hayupo sawa.Ikiwezekana serikali impeleke Mirembe akatulizwe.Amekosa subra ambayo inasisitizwa sana kwenye imani yake.Mimi nilianza kumuona wa ovyo siku moja alipokuwa anaongea sehemu fulani akawa anasema tuwe makini tusije tukapata Rais mwingine DUBWANA.Mwingine !! maana yake kuna mwingine aliyepita ni DUBWANA.Asijue kwamba Magufuli alikuwa kwenye mioyo ya wanyonge wengi.Waliomchukia ni yale majizi, vibaraka wa magharibi na wahujumu wa uchumi kwa ujumla wao. Neno DUBWANA halikuwa la kiungwana litoke kwenye kinywa cha Prof. wa hadhi yake.Lakini pia ajiulize ana umri gani wa kuanza kulilialilia cheo.Kilishapita hicho.Ajutie mdomo wake kwa kauli aliyoitoa kule nje kuhusu bunge. Kama nia ilikuwa kuwafurahisha mabeberu basi awalilie haohao.
Kauli tu za kubeza matajiri na kuwaita MASHETANI ndiyo zilikuwa zinawafurahisha unaoita wanyonge. Maisha ya unaouta wanyonge yamebaki vile vile wanacheza bao vibarazani wanamsubiri Magufuli mwingine wamshagilie.