Serikali imwangalie Prof. Assad isimwache ateseke hivi. Huyu jamaa hayupo sawa

Serikali imwangalie Prof. Assad isimwache ateseke hivi. Huyu jamaa hayupo sawa

Naona kama kuna mahali unapotosha mtoa maada.Alisema issue inayomuumiza ni kifo cha mke wake kipenzi.Hayo mengine unaongezea wewe.Si dhani kama Prof.Asad ni wa hivyo.angelikuwa ni muoga wa maisha angeendeleza uchawa kama wanavyofanya wengine.binafsi nampenda huyu prof.kwa jinsi anavyoyachukulia maisha na kulinda uhuru wake binafsi na wakitaaluma.Hii inanifanya niaziamini kaguzi zake zaidi kuliko za Ma CAG wengine wote .Inaonekana ni kati ya watu wasiohofia wanadamu ila wanahofu ya Mungu wake.Hata hii interview inaonyesha ni mtu huru.
Unaweza kutupatia ripoti zake kuhusiana na ukaguzi miradi ya NHC na nssf na mwenendo wa mifuko ya hifadhi za jamii
 
Sisi wakristo tunafundishwa kusamehe na kua usipomsamehe mtu hata wewe hutasamehewa na Mungu, angekua ni mkristo anayeisoma bible na kuielewa angeshasamehe

Huwezi samehe kitu kama hiki. Unasemehe individuals siyo mfumo ... mfumo wetu ni mbovu unatakiwa kurekebishwa. Kusamehe mfumo mbovu ni kuhalalaisha dhuluma kwa Taifa zima ... hii ikimaanisha kuwa at some point kila Mwananchi ataathirika.
 
Asante mzee Said kwa Marekebisho hovyo >>ovyo....

Hiyo hoja yako ya kushinda kesi sio ambayo imepostiwa humu...millio yake ndo tunaijadili.

Unajaribu kimsafisha na ushindi wa kesi,haina maana.mwaambie aache kulalama

Ni maprofesa wangapi wamenyang'anywa nafasi?mbona hatuwaskii wakishinda media kujiliza???

Hiyo heshima ya UDsm unayoizungumzia kwa milio yake nafikiri hadhi yake inakuwa sambamba na wale wa majalalani.
Muigai...
Humjui Mussa Assad.
 
MAKAFIRI SIKU ZOTE HAMTAKI WATU WADAI HAKI ZAO,HAKUNA SEHEMU HATA MOJA AMBAPO PROF ASSAD KALALAMIKA.KILICHOFANYIKA NI YEYE KUONDOLEWA KINYUME KWA KATIBA,NA NI HAKI YAKE KUPIGANIA HAKI YAKE...

KAMA KUDAI HAKI NI KULALAMIKA BASI WACHA NA IWE HIVYO.
 
Siyo issue ya kuwa kama angekuwa mkiristo ndiyo asamehe.Kwanza asamehe amefanywa nini.Ile ofisi haukuwa ya baba yake Mzazi kwamba atakaa nayo milele.Kwanza mnavyosema ana akili kwa kuwa ni Profesa ,mimi naseama Assad hana akili kabisa.Profesa mzima mwenye taaluma tena ya kujiongeza binafsi maisha yakaendelea analialia mbele ya kamera eti anakumbuka alivyoondolewa ofisini.Huu ni ubwege uliopitiliza.Angelia kwa kuwa Magufuli kamnyang'anya degree zake zote hapo ningesema labda.Lakini no matter anashahada ngapi lakini hili analolionyesha sasa linamuweka katika kundi la vilaza.Analialia kama LAST BORN.Hata jina la Asaad halimfai tena. Mana ya Asaad ni Simba.Sasa huyu Simba kweli au Kondoo ?
Hivi ndugu yangu uliisikiliza ile interview yake na Kikeke?
Maandiko ya wachangiaji wengi yanaendeshwa na hisia na chuki walizonazo sijui hata za kitu gani.Sijawahi kumsikia Prof Assad akilalamika ajira au kurudishwa kazini.Kesi ya kikatiba alifungua Zitto Kabwe na hukumu ya mahakama kuu ilitoka kuthibitisha Katiba ilivunjwa kuondolewa kwa CAG Assad.Halafu Prof sio mtu mwepesi kama unavyomfikiria.Yuko vizuri na ana connection na heshima kubwa kimataifa.Yeye kubakia Tanzania na kuamua kufundisha chuo kikuu cha kiislamu, ni moja katika mikakati yake ya kutengeneza wema unaoendelea.
 
Anahitaji ushauri wa kisaikolojia. Mpaka leo bado analia akikumbuka alivyoondolewa ofisini. Akiulizwa tu hilo jambo analia sana. Ananung'unika, anasononeka, anahuzunika, anaghadhibika, anatatajika.

Prof mpaka kufika hapo ni wazi ana akili za darasani. Ila emotional intelligence ndo shida. Prof miaka mitatu bado anaugua sana akiugulia ile nafasi. Sisi wengine tulishaondolewa makazini kwa vyeti fake n.k na maisha yakaendelea tu.

Wengine tuliondolewa sababu ya uwezo ila vyetu tulikuwa navyo tukasema tu aaargh sikuzaliwa niwe Mkurugenzi au Katibu xxxxx.

Soma pia: Prof. Mussa Assad: Taarifa ya utenguzi wangu nilipewa siku moja kabla

Kwa Prof Assad. Imekuwa tofauti. Bado analalamika. Serikali iingilie kati. Imsaidie akae sawa kihisia na kiakili. Ni wazi hili suala lilimuathiri sana. Asiachwe peke yake. Na kama ana madai Samia mlipe Prof apumzike. Pia apewe mtaalamu wa saikolojia amwambie haya ni maisha tu . Kwani

KUKATIKA KWA MPINI SI MWISHO WA KULIMA. asiumie bado ana maisha na anaweza pewa cheo kingine. Kumfariji asiachwe hivi hivi please. Afya ya akili is real.
Jitahidi basi kuwa mkweli basi,huyu mtu amepata msiba wa kufiwa na mkewe na ndilo eneo pekee kwenye mahojiano alishikwa na uchungu alipokuwa akihojiwa kuhusiana na huo msiba.
Hii nchi imekuwa ya kishetani sana, wewe unayeongea huu utumbo huna unachoweza kushindana na Prof. Assad, ni kweli alionewa na mahakama imethibitisha. Hili ni funzo kwetu sote kwani aliyemuonea hayupo,yeye Prof. yupo hatujui kwa nini yeye hayupo japo inawezekana ikawa ni majibu kwa yale aliyowatendea wenzie na wao wakamuachia aliye juu, mhukumu wa haki.
 
Anahitaji ushauri wa kisaikolojia. Mpaka leo bado analia akikumbuka alivyoondolewa ofisini. Akiulizwa tu hilo jambo analia sana. Ananung'unika, anasononeka, anahuzunika, anaghadhibika, anatatajika.

Prof mpaka kufika hapo ni wazi ana akili za darasani. Ila emotional intelligence ndo shida. Prof miaka mitatu bado anaugua sana akiugulia ile nafasi. Sisi wengine tulishaondolewa makazini kwa vyeti fake n.k na maisha yakaendelea tu.

Wengine tuliondolewa sababu ya uwezo ila vyetu tulikuwa navyo tukasema tu aaargh sikuzaliwa niwe Mkurugenzi au Katibu xxxxx.

Soma pia: Prof. Mussa Assad: Taarifa ya utenguzi wangu nilipewa siku moja kabla

Kwa Prof Assad. Imekuwa tofauti. Bado analalamika. Serikali iingilie kati. Imsaidie akae sawa kihisia na kiakili. Ni wazi hili suala lilimuathiri sana. Asiachwe peke yake. Na kama ana madai Samia mlipe Prof apumzike. Pia apewe mtaalamu wa saikolojia amwambie haya ni maisha tu . Kwani

KUKATIKA KWA MPINI SI MWISHO WA KULIMA. asiumie bado ana maisha na anaweza pewa cheo kingine. Kumfariji asiachwe hivi hivi please. Afya ya akili is real.
Prof anateseka?

Au afya ya akili?
 
CAG akistaafu, kuna asilimia fulani anaendelea kiupata hadi kifo. yeye anapata? kama hapati, ana haki ya kulalamika. kama anapata, nitamshangaa sana.
 
Unaweza kutupatia ripoti zake kuhusiana na ukaguzi miradi ya NHC na nssf na mwenendo wa mifuko ya hifadhi za jamii
Nikupatie mimi tena?hizi si ni public reports ambazo hata darasa la kwanza B anaweza kuzi-acess. au ulimaanisha nini?
 
Back
Top Bottom