rafikiwamwananchi
New Member
- Apr 16, 2026
- 1
- 1
Kuna jambo ambalo nimekuwa nikijiuliza kuhusu safari yetu ya digital transformation Tanzania. Serikali ina mifumo mingi yenye taarifa muhimu, na tayari ina miundombinu ya data sharing na interoperability kupitia GovESB. Miongozo ya e-GA yenyewe inaeleza kuhusu application integration, data exchange, APIs na hata ushirikiano na third parties.
Lakini swali langu ni hili: nini hasa kimezuia serikali kuweka APIs za baadhi ya huduma na data zisizo nyeti ziweze kupatikana kwa developers na startups kupitia utaratibu rasmi? Sizungumzii kufungua data zote za wananchi. Taarifa binafsi na nyeti lazima zilindwe chini ya sheria za ulinzi wa data. Ninachozungumzia ni kuwa na Developer Portal, documentation, sandbox na controlled API access kwa wale wanaokidhi vigezo.
Kwa mfano, kijana anayetengeneza School Management System anaweza kuhitaji kuunganisha mfumo wake na huduma fulani za serikali. Badala ya kila developer kuanza mchakato mrefu wa kutafuta taasisi, kuandika barua na kusubiri approvals zisizo na timeline, kwa nini isiwe register → apply → security review → API key → sandbox → production? Serikali yenyewe ina guidelines zinazotaka data sharing iwe na security assessment, permissions na data-sharing agreements; kwa hiyo controlled access inawezekana bila kuathiri usalama.
Zaidi ya hapo, Tanzania e-Government Strategy tayari inaweka msisitizo kwenye system integration, interoperability na data sharing, pamoja na lengo la mifumo ya serikali kushirikishana data. Kwa hiyo, labda mjadala haupaswi kuwa “je APIs zinahitajika?” bali “kwa nini tusipanue interoperability kutoka ndani ya serikali kwenda kwenye ecosystem ya innovators, startups na private sector pale ambapo ni salama na kuna manufaa kwa umma?”
Swali langu kwa serikali, developers na wadau wa teknolojia ni moja: Kama API inaweza kutolewa kwa usalama, ikiwa na authentication, permissions, rate limits, audit trails na data-sharing agreements, ni kikwazo gani hasa kinachofanya APIs za huduma za serikali zisiwe na njia rasmi na rahisi ya kuombwa na kutumiwa na wabunifu wa Tanzania? Je, ni sheria, usalama, ownership ya data, technical capacity, bureaucracy, au ni suala la policy?