DOKEZO Serikali ina mpango gani na Afya za Wananchi wanaotumia Soko la Mabibo? Watu wanalishwa uchafu pale

DOKEZO Serikali ina mpango gani na Afya za Wananchi wanaotumia Soko la Mabibo? Watu wanalishwa uchafu pale

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna vitu vinaumiza na kukera sana kwenye jiji la Dar es Salaam. Hali ya Masoko yake ni mbaya mno, ni ajabu sana kuamini Masoko haya yapo Dar es Salaam, sehemu inayoongoza kwa makusanyo nchi nzima.

Hebu angalia uchafu uliotapakaa kwenye masoko haya. Haileweki kipi Chakula kisafi kipi kichafu maana vyote viko kwenye uchafu.

Na mbaya zaidi Mkuu wa Mkoa Chalamila anasikika akiagiza Wanajeshi kufanya usafi kwenye mitaa ambako hata hakuna shida bali ni masuala tu ya kisiasa.

Hebu Mamlaka ziwe serious na afya za Wananchi jamani
IMG_20240119_132922_423.jpg
IMG_20240119_132922_696.jpg
IMG_20240119_132922_597.jpg
IMG_20240119_132922_309.jpg
IMG_20240119_132922_444.jpg
IMG_20240119_132922_714.jpg
IMG_20240119_132934_960.jpg
IMG_20240119_132935_053.jpg
IMG_20240119_132934_619.jpg
IMG_20240119_132935_149.jpg
IMG_20240119_132934_723.jpg
IMG_20240119_132934_320.jpg
IMG_20240119_132934_770.jpg
IMG_20240119_132934_634.jpg

Pia soma:
  1. KERO - Hali ya Soko la Ndizi Mabibo ni mbaya, mamlaka ziwajibike kwa kufumbia macho kero ya Wananchi
  2. Wafanyabiashara Soko la Ndizi Mabibo: Rais Samia tunaomba tusaidie tupate hati ili soko lijengwe
  3. Dar: RC Chalamila amevunja Uongozi wa Soko la Mabibo na kukabidhi kwa Manispaa ya Ubungo
  4. Dar: Milioni 600 zatengwa kukarabati soko la Mabibo
 
Kuna wale wakodisha but wanapiga hela hao na wale Waosha miguu ..mkuu labda hii ni biashara ya watu
 
Nchi hii naishangaa sana, hivi zile V8 wanazonunuliana hadi wilayani wakiacha kununua hata 5 tu si wanapiga sakafu ya maana hapo sokoni ni mitalo ya kutiririsha maji machafu!
 
Mheshimiwa spika serikali inampango wa kupoboresha na masoko na ipo kwenye upembuzi yakinifu na mkandarasi yuku saiti kwaiyo wananchi wakae kwa kutulia serikali yao ni sikivu
 
Hapa ndo napowashangaa chadema, wangekua wanafanya ziara zao kwenye sehemu kama hizi na sehemu zenye matatizo makubwa wakiwa na vyombo vya habari ili kuiweka ccm uchi.... Naamini baada ya mwaka ccm akili zingewakaa sawa
Wao wanataka mambo ya uchaguzi tu
 
Mkuu matatizo ya uchafu si masoko ya dar tu ukifika Arusha jiji la kitalii utashangaa masoko machafu kama zizi la kondoo
Wahuni wapo madarakani usitarajie chochote.
 
Nchi hii naishangaa sana, hivi zile V8 wanazonunuliana hadi wilayani wakiacha kununua hata 5 tu si wanapiga sakafu ya maana hapo sokoni ni mitalo ya kutiririsha maji machafu!

Inawezekana kuna haja ya kusakafia hapo, naiona point yako. Lakini pia, kuna tatizo kubwa zaidi, tatizo la kitabia na kiutamaduni, na hili halibadilishwi kwa kujenga au kutenga bajeti kubwa.

Tuna tatizo kubwa sana la kufikiri kwamba tatizo letu ni pesa na bajeti tu.

Kuna jamaa mmoja anaitwa Mubelwa Bandio alikuwa ana msemo wake anasema "unavyoliangalia tatizo ni tatizo".

Hapa tuna tatizo la tabia, tatizo la utamaduni. Zaidi ya tatizo la pesa.

Ukiwa na utamaduni wa usafi, utakuwa msafi tu hata kama bajeti ndogo unaishi kwenye kibanda. Na ukiwa na utamaduni wa uchafu, hata ukikaa kwenye kasri la marumaru na vitasa vya dhahabu, utakuwa mchafu tu.
 
Inawezekana kuna haja ya kusakafia hapo, naiona point yako. Lakini pia, kuna tatizo kubwa zaidi, tatizo la kitabia na kiutamaduni, na hiki halibadilishwi kwa kujenga au kutenga bajeti kubwa.

Tuna tatizo kubwa sana la kufikiri kwamba tatizo letu ni pesa.

Kuna jamaa mmoja anaitwa Mubelwa Bandio alikuwa ana msemo wake anasema "unavyoliangalia tatizo ni tatizo".

Hapa tuna tatizo la tabia, tatizo la utamaduni. Si tatizo la pesa.

Ukiwa na utamaduni wa usafi, utakuwa msafi tu hata kama bajeti ndogo unaishi kwenye kibanda. Na ukiwa na utamaduni wa uchafu, hata ukikaa kwenye kasri la marumaru na vitasa vya dhahabu, utakuwa mchafu tu.
Sasa tunaibadirisha vipi hii jamii ya kitanzania kuzingatia usafi kwenye hili lindi la umaskini lilowatamalaki kila kona? Yaani wao wanajishughulisha kujikimu na maisha tu!
 
Sasa tunaibadirisha vipi hii jamii ya kitanzania kuzingatia usafi kwenye hili lindi la umaskini lilowatamalaki kila kona? Yaani wao wanajishughulisha kujikimu na maisha tu!
Kwanza inabidi tujenge jamii iliyojikita katika elimu na maisha ya kisayansi yasiyokubali kuishi kwa kudra na miujiza.

Mtu anayeamini kuishi kwa kudra na miujiza hawezi kuogopa uchafu, ataupigia sala tu na kusema Mungu ataninusuru tu. Au atauvalia hirizi ya kumkinga. Au atasema tu mimi niko special siwezi kuathirika.

Na hawa ndio wengi Tanzania.
 
Watu weusi tuna upumbavu wa milele!
 
Yaani wanashindwa hata kumwaga zege hapo, kwenye maeneo ya kuuzia - soko zima? Na ushuru wanakusanya kila siku. Soko liko hapo kwa zaidi ya miaka 20, ushuru waliokusanya tu - ungetosha kumwaga zege.
 
Kama mjini Daslam kuko hivyhuko vijijini kukoje?

Suala la afya ya mtanzania sio kipaumbele Cha serikali ya mh SSH maana hata. Kadi za NHIF hospital nyingi za private haipokelew.
 
Nadhani wanunuzi ndo walaumiwe
Wasiponunua watakula nini?
Hali hii iko hivi masoko yote ya Dar! Hizo picha zinapnesha soko la Ilala lakini ukienda masoko ya Temeke , Kinondoni na Kigamboni hali ni hiyo hiyo!
Na DC na RC wapo
uchafu anaokwenda kukusanya Chalamila na majeshi yetu uko wapi? Aanze kwenye masoko!
 
Aione mkuu wa mkoa. Aachane na chadema. Yeye afanye wajibu wa cheo chake. Asisimamie wilaya na halmashauri zimize wajibu wao kwa wananchi
 
Disgusting. Yani we are very primitive kwenye hii karne ya 21.

Tunaishi kama barbarians.
 
Hapa ndo napowashangaa chadema, wangekua wanafanya ziara zao kwenye sehemu kama hizi na sehemu zenye matatizo makubwa wakiwa na vyombo vya habari ili kuiweka ccm uchi.... Naamini baada ya mwaka ccm akili zingewakaa sawa
Umeandika pointi moja nzito iliyosimama, natamani sio tu chadema bali upinzani kwa ujumla wangeiona

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom