Serikali inaendelea kufanya ubaguzi kwenye ajira. Kama una div 1&2 au bachelor degree jua upo kwenye risk ya kutoajiriwa

mkuu hapa umesema ukweli, tatizo hili yabidi kuwepo mwakilishi wa kuliwasilisha bungeni haraka sana.

Viongozi wengi ktk ngazi za juu ni mbulula na vilaza waliorisiti na kuunga elimu. Elimu zao ni za kuungia/ Kuungaunga. Unakuta kiongozi ana PhD, ila PhD yake ameipata kwa rushwa na kwa kujuana kisa tuu ni mbunge.

Hawahawa viongozi wamezaa mbulula na vilaza kama wao. Watoto wao ni form four failure, watu wa div four na zero. Hii ni kwaajili ya ugumu wa vichwa vyao kama vya baba zao na mama zao, then wanaungishwa certificate na diploma.

Hivyo basi ndo maana ajira na kazi nyingi wanapewa form four failure, div four, certificate na diploma maana wengi wao ni watoto wa viongozi.

Pia viongozi wanawakomoa wenye akili waliosoma moja kwa moja bila kuungia, kisa wao na watoto wao ni vilaza wanasoma kwa kuungia.

Hili swala ni la kusikitisha sana, wanaharakati na wabunge wenye akili timamu, ambao hawakuungia elimu walipeleke bungeni likadiskasiwe.
 
Kazi ya polisi kwa Tz inahitaji mtu ambaye amefeli, sababu ni ya kutumia nguvu na siyo akili, fikiria unatumwa kwenda kumwekea madawa ya kulevya mfukoni raia ambaye hana hatia au kumpiga mpaka afe kisa amegoma kusema unachotaka wewe. sikushauri uwe polisi ni dhambi kubwa sn.
 
Yaani mm na degree yangu nikawe mlinzi bank? acha niendeshe bodaboda asee
 
Hapo inabidi watu waanze kufeli maksudi ili wapate nafasi za upolisi ....

Huwezi kuwa polisi kama hujapata zero form four ..
Labda niseme hivi: Tanzania kumekuwa na obsession ya wanafunzi kusoma ili wafaulu mitihani. Lengo la elimu siyo kufaulu mtihani bali kuelimika. Hivyo basi ajira zinatakiwa kutolewa kwa kuzingatia vigezo vingi na siyo kigezo cha ufaulu tu, kwani kama nilivyosema, kuna watu wengi wamefaulu vizuri sana lakini hawajaelimika. Nini kifanyike? Kama kuna post ya kazi ya kujaza, na sifa yake ni A level secondary, basi ni vizuri kuchagua ma-applicant kutoka kila daraja i.e. 1, 2, 3, na 4; halafu washindanishwe ili kupata watu qualified wa kujaza hizo nafasi.
 
Hiyo ni sahihi kabisa ukienda kwenye ukurasa wa tume ya utumishi unakuta nafasi za ajira kwa cheti na diploma ni nyingi zingine hata ambazo mtu mwenye degree anaweza omba lakini utasikia tunataka cheti na diploma mpaka nacheka na kujiuliza Sasa wanaogopa nini watu wa degree
 
Kuna mtu mwenye busara alishawahi kunambia kuwa ukiweka viongozi wasio na utu wataendeleza kariba yao, ukiweka wenye vyeti feki wataendeleza kariba yao kwa watakaowaleta katika mfumo, ukiweka makahaba katika uongozi watavuta makahaba wenzao kwenye uongozi.

So sijui tunatazama watu tunaowaachia kushika nyadhifa maana sijui huwa tunajisahaulisha kuwa hawa watu wakishafika kule juu hurejea asili zao....

Hivi unategemea mtu ambaye amefoji vyeti hadi kufika juu aje aweke mtendaji mwenye vyeti halali vya hadhi ya juu ili aje wajibishwa?!

Wazee wengi waliopo serikalini wana elimu za kuunga unga so wanaendeleza utamaduni huo sababu they are looking after their own kind......
 
Kwa Askari polisi ninaowafaham Mimi yaan niliotoka nao sehemu moja sikumbuki Kama Kuna mtu alienda polisi angalau akiwa hata na division three form four.

Wote walioenda polisi ni wale waliofeli form four hasa wenye division 29 ,30 ,31,na 32. Baadae nikaja gundua why polisi wanapenda waliofeli ,jibu ni kwamba wanataka kuwatumikisha kwa muda mrefu Sana maana wanajua kabisa mtu mwenye matokeo hayo hata akiamua kujiendeleza kutoboa ni mbinde Sana Zaid wanastafu huku wakiwa na mbavu mbili begani.

Kuna mdada mtaani kwetu alikuwa kilaza wa kutupwa yaan alitoka na 32 form four Leo ni Askari na anavimba balaa akijaga rikizo Ila kichwan ni zero brain na hata akiamua kujiendeleza Sina Iman km anaweza pata hizo credit tatu na kutoboa paper la six maana hamna kitu.

Hivyo ndugu yangu hiyo kaz ukiwa na vyeti Safi huwez zingatiwa maana Kwanza watakuhofia sana wale waliounga unga Sana na kupata walau diploma maana wanajua unakuja kutakeover nafas zao .kazi ya upolisi asilimia kubwa ni ya watu vilaza Sana wale toleo la mwisho kabisa ingawa wapo baadhi wenye elimu Safi kabisa Ila hao walioingia na elimu saf jua kabisa lazima Ana mtu mzito huko huko kitengoni ndio maana akingia bila shida .

Askari kalibia asilimia 90 waliingia huko wakiwa na four mbovu ,asilimia 10 waliingia na elimu Safi na ndio hao wanaowaongoza hao vilaza wengi.
 
Kazi ya upolisi haiitaji ufaulu mkubwa ,nyinyi wenye madigirii mnatakiwa mjiajiri 😂😂
 
You need not regret kazi utapata tena yenye heshima kulingana na taaluma yako. Achana na upolisi kazi ambayo aina heshima mtaani. Ujue polisi wote wakisoma sana nani atalinda Benki na majumba ya ma- DC, RC, Waziri, na waheshimiwa waliofeli pia form four na six
 
Ila wabongo tunalalamika aiseeeeee.

Kwenye kila kitu. Kila kitu.
Wabongo bhana!

Mafanikio kidogo tu tayari unajiona umepatia maisha na kuanza kudharau wengine!

Hata hivyo Heri yako usiyelalamika leo maana ipo siku yaja nawe utalia na kusaga meno!
 
Kwahiyo walipata four wasiajiriwe au hawastahili kupata ajira acha ujinga nawao ni binadam na wanahaki kama wewe kama umesoma sana umefaulu vizuri pambana elimu yako ikusaidie utoke kimaisha sio uone wengine wanafaa wengine hawafai
 
Haiwezi kukulipa kwa degree yako walimu mpo wengi sana
 
Hapo inabidi watu waanze kufeli maksudi ili wapate nafasi za upolisi ....

Huwezi kuwa polisi kama hujapata zero form four ..
Ukisema hivyo unakosea, semea connection mkuu.... Kama huna connection kwa maisha ya sasa mafanikio utayapata kwa kutoka jasho la meno na damu kila kona ya mwili wako! Utateseka mno ili kufanikiwa iwe kupata kazi ama michongo tu ya kukutoa kimaisha.
 
Upuuzi wao ni kutaka Advanced dipoloma ambayo kwa sie wa NTA level 6 inakuwa ni diploma ila sio ile advanced ya ki old school wanayotaka serikali!

Yani Diploma za vyuo vya sikuhizi ukiombea kazi ajira portal zinagoma inataka advanced diploma ya kizamani ile ambayo ni equivalent na degree sasa sijui serikali ina mawazo gani? Ifikie mahali Diploma zote ziwe acceptable sio ile tu wanayoita wao “Advanced diploma”
 
Mimi binafsi Naona suala la ajira ni mtambuka na Lina sekta yake ya ajira chakufanya shauri serikali ifanye nini ili kuboresha .LENGO LA SERIKALI NI KUCHUKUA USHAURI MZURI NA KUUFANYIA KAZI KUPITIA VYOMBO HUSIKA.NA PIA USILALAMIKE NDUGU SERIKALI NI SIKIVU MNO TENA CHINI YA SSH 💥💥 MAMBO NI FIRE JAMANI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…