Serikali inaendelea kufanya ubaguzi kwenye ajira. Kama una div 1&2 au bachelor degree jua upo kwenye risk ya kutoajiriwa

Jiajiri kaka kwenye BIASHARA ndogo ndogo intrepreneurship ili KUPATA fedha kubwa hata humu unaweza kuonana na WATAALAMU wa ujasiriamali na KUFANIKISHA kukuza UWEZO wako kiuchumi.Fursa ni nyingi mnoo
 
Serikali mara kwa mara imekuwa ikiwahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kufaulu lakini jambo la kusikitisha unapofika wakati wa ajira serikali hiyo hiyo inawabagua tena.

Tumeona kwenye ajira za polisi wanaotakiwa ni wale ambao hawakufanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne. Yaani waliopata divisheni Four ila waliofaulu vizuri kwa kupata divisheni one na Two hawatakiwi.

Sanjari na hilo, kuna ubaguzi mkubwa unafanywa na serikali kwenye utoaji wa ajira hasa kwa wahitimu wenye elimu ya juu i.e bachelor degree holders kulinganisha na level zingine za kielimu kama vile diploma na certificate.

Mfano mimi nimehitimu kidato cha nne mwaka 2011. Kwakuwa nilikuwa na ndoto ya kufika mbali kielimu kama serikali inavyosisitiza, nilisoma kwa bidii na kufanikiwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita.

Sikuishia hapo, niliendelea kukazana kwa nguvu zote na maarifa yote na hatimaye nikafanikiwa kuendelea na elimu ya juu na sasa ni mhitimu wa moja ya chuo kikubwa hapa nchini

Lakini katika yote, wenzangu niliomaliza nao kidato cha nne wakapata ufaulu wa divisheni Four kisha kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti leo hii ni waajiriwa wa serikali wanakula keki ya Taifa.

Niliomaliza nao kidato cha sita wakakosa sifa (qualifications) za kujiunga chuo kikuu wakaenda kusomea ualimu ngazi ya diploma tayari wote wameajiriwa serikalini

Lakini mimi niliyefuata ushauri wa serikali wa kusoma kwa bidii na kufaulu kwa kufikia kiwango cha elimu ya juu leo naonekana sina thamani kwani serikali ile ile iliyonihamasisha kusoma kwa bidii ndio ile ile imeniweka mtaani kwa takribani miaka minne sasa. Kwa maana nyingine kiherehere changu cha kusoma kwa bidii na kufaulu leo hii ndio kinaniponza kwa sababu kama ningefeli kidato cha nne au sita leo ningekuwa ni miongoni mwa wanaofaidi keki ya Taifa.

Mwisho wa yote kama serikali haina mpango wa kuajiri wahitimu wenye bachelor degree tunaomba itamke hadharani ilikusudi vijana tujue moja kwani hata ajira zinapotangazwa wenye bachelor degree wanaoajiriwa ni wachache sana tena nafikiri ni katika jitihada za serikali kuficha dhambi ya ubaguzi wanayoifanya isijulikane kirahisi.
BACHELOR DEGREE??? 🤣🤣😃😃😁😁

POLE SANA
 
Vumilia mkuu naamini mambo yako yataenda sawa, hii serikali inachofanya inabana wage bill kwa kuajiri watu wengi wenye certificate na diploma na kama ulivyosema polisi wenye div. 4 kwa kuwa inajua itawalipa mshahara mdogo kulinganisha na ukiajiri wenye shahada. Ni serikali ya ajabu tu inayoweza ku compromise na sifa ya kiwango cha elimu kufikia maendeleo ya haraka. Na ukiona kwa haraka haraka pesa wanazobana wanazitumia kwenye madili yao ya ufisadi pamoja na zile tozo wanazopora wanyonge.
 
by the way wewe pia si uliimba wataisoma nambae Ccm mbere kwa mbere??
Serikali mara kwa mara imekuwa ikiwahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kufaulu lakini jambo la kusikitisha unapofika wakati wa ajira serikali hiyo hiyo inawabagua tena.

Tumeona kwenye ajira za polisi wanaotakiwa ni wale ambao hawakufanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne. Yaani waliopata divisheni Four ila waliofaulu vizuri kwa kupata divisheni one na Two hawatakiwi.

Sanjari na hilo, kuna ubaguzi mkubwa unafanywa na serikali kwenye utoaji wa ajira hasa kwa wahitimu wenye elimu ya juu i.e bachelor degree holders kulinganisha na level zingine za kielimu kama vile diploma na certificate.

Mfano mimi nimehitimu kidato cha nne mwaka 2011. Kwakuwa nilikuwa na ndoto ya kufika mbali kielimu kama serikali inavyosisitiza, nilisoma kwa bidii na kufanikiwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita.

Sikuishia hapo, niliendelea kukazana kwa nguvu zote na maarifa yote na hatimaye nikafanikiwa kuendelea na elimu ya juu na sasa ni mhitimu wa moja ya chuo kikubwa hapa nchini

Lakini katika yote, wenzangu niliomaliza nao kidato cha nne wakapata ufaulu wa divisheni Four kisha kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti leo hii ni waajiriwa wa serikali wanakula keki ya Taifa.

Niliomaliza nao kidato cha sita wakakosa sifa (qualifications) za kujiunga chuo kikuu wakaenda kusomea ualimu ngazi ya diploma tayari wote wameajiriwa serikalini

Lakini mimi niliyefuata ushauri wa serikali wa kusoma kwa bidii na kufaulu kwa kufikia kiwango cha elimu ya juu leo naonekana sina thamani kwani serikali ile ile iliyonihamasisha kusoma kwa bidii ndio ile ile imeniweka mtaani kwa takribani miaka minne sasa. Kwa maana nyingine kiherehere changu cha kusoma kwa bidii na kufaulu leo hii ndio kinaniponza kwa sababu kama ningefeli kidato cha nne au sita leo ningekuwa ni miongoni mwa wanaofaidi keki ya Taifa.

Mwisho wa yote kama serikali haina mpango wa kuajiri wahitimu wenye bachelor degree tunaomba itamke hadharani ilikusudi vijana tujue moja kwani hata ajira zinapotangazwa wenye bachelor degree wanaoajiriwa ni wachache sana tena nafikiri ni katika jitihada za serikali kuficha dhambi ya ubaguzi wanayoifanya isijulikane kirahisi.
 
Serikali mara kwa mara imekuwa ikiwahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kufaulu lakini jambo la kusikitisha unapofika wakati wa ajira serikali hiyo hiyo inawabagua tena.

Tumeona kwenye ajira za polisi wanaotakiwa ni wale ambao hawakufanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne. Yaani waliopata divisheni Four ila waliofaulu vizuri kwa kupata divisheni one na Two hawatakiwi.

Sanjari na hilo, kuna ubaguzi mkubwa unafanywa na serikali kwenye utoaji wa ajira hasa kwa wahitimu wenye elimu ya juu i.e bachelor degree holders kulinganisha na level zingine za kielimu kama vile diploma na certificate.

Mfano mimi nimehitimu kidato cha nne mwaka 2011. Kwakuwa nilikuwa na ndoto ya kufika mbali kielimu kama serikali inavyosisitiza, nilisoma kwa bidii na kufanikiwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita.

Sikuishia hapo, niliendelea kukazana kwa nguvu zote na maarifa yote na hatimaye nikafanikiwa kuendelea na elimu ya juu na sasa ni mhitimu wa moja ya chuo kikubwa hapa nchini

Lakini katika yote, wenzangu niliomaliza nao kidato cha nne wakapata ufaulu wa divisheni Four kisha kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti leo hii ni waajiriwa wa serikali wanakula keki ya Taifa.

Niliomaliza nao kidato cha sita wakakosa sifa (qualifications) za kujiunga chuo kikuu wakaenda kusomea ualimu ngazi ya diploma tayari wote wameajiriwa serikalini

Lakini mimi niliyefuata ushauri wa serikali wa kusoma kwa bidii na kufaulu kwa kufikia kiwango cha elimu ya juu leo naonekana sina thamani kwani serikali ile ile iliyonihamasisha kusoma kwa bidii ndio ile ile imeniweka mtaani kwa takribani miaka minne sasa. Kwa maana nyingine kiherehere changu cha kusoma kwa bidii na kufaulu leo hii ndio kinaniponza kwa sababu kama ningefeli kidato cha nne au sita leo ningekuwa ni miongoni mwa wanaofaidi keki ya Taifa.

Mwisho wa yote kama serikali haina mpango wa kuajiri wahitimu wenye bachelor degree tunaomba itamke hadharani ilikusudi vijana tujue moja kwani hata ajira zinapotangazwa wenye bachelor degree wanaoajiriwa ni wachache sana tena nafikiri ni katika jitihada za serikali kuficha dhambi ya ubaguzi wanayoifanya isijulikane kirahisi.
Si sawa kusema kwamba Divisheni 1 na 2 hawatakiwi Polisi. Nafasi ya kazi inapotangazwa, sifa zinazotajwa ni kiwango cha chini kabisa kinachohitajika kwa kazi hiyo ili kwamba kama uko chini ya hapo ujue hutachukuliwa. Hata kuendelea na masomo ukiambiwa lazima uwe na 'C' kwenye somo fulani haimaanishi mwenye 'B' au 'A' hatachukuliwa. Polisi wanapotaja Divisheni 3 au 4 maana yake ni kwamba kama wewe ulimaliza Darasa la 7 tu au ulipata Divisheni '0' Kidato cha 4, usiotee kupewa kazi hiyo. Najua kwamba polisi siyo kwamba hawataki waliofuzu vizuri. Ingekuwa hivyo, wasingekuwa wanachukua watu wenye shahada ya Chuo Kikuu. Shughuli inayokuwa wazi hivi sasa ni ile inayomuhitaji mtu aliyepata si chini ya Divisheni 3 au 4 Kidato cha 4. Kesho na kesho kutwa kutakuwepo na nafasi zinazohitaji shahada ya Chuo Kikuu ngazi ya 3rd Class. Mwenye 1st Class hakatazwi kutuma maombi; lakini asishangae kuajiriwa pamoja na mtu wa 3rd class kwa kuwa kiwango hicho cha elimu kimepimwa kuwa kinatosha kwa kazi iliyopo.
 
Lakini katika yote, wenzangu niliomaliza nao kidato cha nne wakapata ufaulu wa divisheni Four kisha kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti leo hii ni waajiriwa wa serikali wanakula keki ya Taifa.
Hapa umedanganya jukwaa. Nakushauri uache mara moja.
 
Hata, kama ndio ajira hizo ndio niwe polisi wa kukimbizana na were??! Bora nijiajiri mwenyewe. Kwani hao certificate unaowazungumzia wanalipwa shilingi ngapi kwa mwezi???
 
Mimi nina maswali ya msingi ya kukuuliza wewe mtoa mada

1.) Kabla ya kuanza kusomea degree ya ualimu, ulikuwa unafahamu hii trend ya serikali kufanya ubaguzi kwenye ajira?

2.) Shule private hasa hizi za English medium , kama Tusiime, na zenye ada kubwa na mishahara mikubwa, huwa zinaajiri wenye degree tu, wenye certificate huwa hawasogezi pua zao huko, mbona hulalamiki kwamba zinabagua wenye certificate?
 
Hapo inabidi watu waanze kufeli maksudi ili wapate nafasi za upolisi ....

Huwezi kuwa polisi kama hujapata zero form four ..
Hawa polisi ndio maana wanakuwa na tabia za ajabu sana , jitu limepata Zero huko basi linataka kukomoa kila mtu, as if sisi ndio tulikwambia afeli, hata huyo aijiipiii sina imani na elimu yake.
 
Suluhisho ni kupunguza muda kustaafu kutoka 60 hadi 50 serikalini.

Pia serikali kuweka mazingira rafiki ili makampuni binafsi yawe mengi, maana ndio wazalishaji wa ajira.

Bila kusahau mazingira rafiki kwa wafanyabiashara ili raia wajiajiri kupitia biashara.
Dawa ni kupiga kodi kubwa bidhaa zinazoagizwa toka nje ambazo pia zinazalishwa hapa nchini, mfano kama cement, sukari, mafuta ya kula nk; vitu ambavyo hatuna uwezo navyo ndio vipewe nafuu
 
Division one na two toka zamani walikuwa hawapewi direct employment hasa kipindi cha Nyerere na Mwinyi hao walikuwa wananyimwa ajira ili waende chuo kikuu nchi ipate viongozi wa juu

Nyerere aliwahi ajiri mameneja vijjiji wenye digrii akawapa mishahara ya digrii hayo matusi waliyomporomoshea baada ya kwenda kuripoti maeneo ya kazi kuwa mabaya hayafai kwa mtu mwenye digrii ikabidi serikali ifute huo mpango wote kuna paper nilisoma mahali

Serikali iko sahihi mtu mwenye digrii huwezi mpanga patrol polisi mwenye digrii ukamuamrisha akimbizane na kibaka au panya road hiyo kazi waweza hao division zero,four na three yeye abakie kamanda tu
 
Una ufaulu mzuri Kwenye makaratasi ila Kichwani huoneshi kama una kitu ume lack Exposure Na Flexibility nasema wacha uteseke
 
Serikali mara kwa mara imekuwa ikiwahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kufaulu lakini jambo la kusikitisha unapofika wakati wa ajira serikali hiyo hiyo inawabagua tena.

Tumeona kwenye ajira za polisi wanaotakiwa ni wale ambao hawakufanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha nne. Yaani waliopata divisheni Four ila waliofaulu vizuri kwa kupata divisheni one na Two hawatakiwi.

Sanjari na hilo, kuna ubaguzi mkubwa unafanywa na serikali kwenye utoaji wa ajira hasa kwa wahitimu wenye elimu ya juu i.e bachelor degree holders kulinganisha na level zingine za kielimu kama vile diploma na certificate.

Mfano mimi nimehitimu kidato cha nne mwaka 2011. Kwakuwa nilikuwa na ndoto ya kufika mbali kielimu kama serikali inavyosisitiza, nilisoma kwa bidii na kufanikiwa kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita.

Sikuishia hapo, niliendelea kukazana kwa nguvu zote na maarifa yote na hatimaye nikafanikiwa kuendelea na elimu ya juu na sasa ni mhitimu wa moja ya chuo kikubwa hapa nchini

Lakini katika yote, wenzangu niliomaliza nao kidato cha nne wakapata ufaulu wa divisheni Four kisha kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti leo hii ni waajiriwa wa serikali wanakula keki ya Taifa.

Niliomaliza nao kidato cha sita wakakosa sifa (qualifications) za kujiunga chuo kikuu wakaenda kusomea ualimu ngazi ya diploma tayari wote wameajiriwa serikalini

Lakini mimi niliyefuata ushauri wa serikali wa kusoma kwa bidii na kufaulu kwa kufikia kiwango cha elimu ya juu leo naonekana sina thamani kwani serikali ile ile iliyonihamasisha kusoma kwa bidii ndio ile ile imeniweka mtaani kwa takribani miaka minne sasa. Kwa maana nyingine kiherehere changu cha kusoma kwa bidii na kufaulu leo hii ndio kinaniponza kwa sababu kama ningefeli kidato cha nne au sita leo ningekuwa ni miongoni mwa wanaofaidi keki ya Taifa.

Mwisho wa yote kama serikali haina mpango wa kuajiri wahitimu wenye bachelor degree tunaomba itamke hadharani ilikusudi vijana tujue moja kwani hata ajira zinapotangazwa wenye bachelor degree wanaoajiriwa ni wachache sana tena nafikiri ni katika jitihada za serikali kuficha dhambi ya ubaguzi wanayoifanya isijulikane kirahisi.

uhitaji wa watumishi ktk level za chini na kati ni kuliko degree holders ndo maana unaona wanachukuliwa wengi.mfano ukiajiri degree holders wengi mfano upande wa majeshi hao wanaenda kuwa watawala na si wapiganaji.uhitaji wa watenda wa elimu ya cheti na diploma ni mkubwa kuliko wa degree holders na huo ndo ukweli hata hvyo fikra ya kuwa unasoma ili uajiriwe serikalini ni potofu mnatakiwa kujiajiri.hakuna sehemu yoyote duniani ambayo imeweza kuajiri kila graduate.maarifa tunayopewa vyuoni yanatusaidia kupambana na changamoto za maisha na cha kufanya ni kuunganisha nguvu zenu pamoja ili serikali iwape mitaji mfanye biashara na maisha yaendelee.kubaki mjini ili kusaka ajira za serikali si dili tena.Nchi ni tajiri na kuna rasilmali nyingi tuchangamkie mitaji tukamate hizo fursa.ukianzisha tu kilimo cha tangawizi unapata pesa na sasa hivi watu wanapiga pesa kwa kilimo cha maparachichi tu.huku kwetu Bukoba kila kukicha masemi yakishusha mzigo pale sudan kusini na uganda yakipita hapa Bukoba yanabeba maparachichi kibao tu yanapelekwa mikoani (viwandani).kazi zipo nyingi tu msilalamike tu njoeni huku shamba tupige kazi.
 
Siku utapojua kwanini ulizaliwa ndipo utaacha kulalamika na kufanya mambo ya msingi. Dunia haina huruma mdogo wangu usisubiri serikali utazeeka bado unatafuta ajira.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kuna vijana wa jkt wenye degree huwa hawabagui hali wanacheza na mavumbi muda wote na wanatii amri , wana nidhamu Na wavumilivu ndo wakashindwe kufanya patrol ? Akati tunawaona huku mitaani wakiwa wanajitolea kufanya usafi.
Naeleza kutokana na uzoefu mfano mdogo shule za private walimu wengi ni wa certificate na diploma ukitaka kuajiri mwenye digrii umlipe mshahara wa Diploma sababu uwezo huna anaanza fujo kukukushtaki Kila Kona kazi atakubali lakini baada ya miezi mitatu anaanza fujo ooh mwalimu mkuu ana ki certificate au kidiploma analipwa vizuri ana gari ya shule self drive na nyumba Mimi na digrii nasota sikubali ila walimu wakenya na waganda hawana shida ana digrii analala bwenini Yuko tayari kulipwa mshahara wa certificate bila shida ndio maana private schools wengi wanawapenda walimu wenye digrii toka Uganda na kenya
 
Kuna vijana wa jkt wenye degree huwa hawabagui hali wanacheza na mavumbi muda wote na wanatii amri , wana nidhamu Na wavumilivu ndo wakashindwe kufanya patrol ? Akati tunawaona huku mitaani wakiwa wanajitolea kufanya usafi.
Hiyo kitaalaamu inait towa over qualification mfano huwezi ajiri mtu mwenye digrii ya transport and motor vehicle engineering Kama dereva wa daladala!!! Ni kweli magari anayajua vizuri lakini Post ya udereva ka over qualify mtasumbuana mbele ya safari ukimwajiri Kama dereva
 
Baada ya kumaliza BA , Bsc na MSc, mambo bado yalitatiza kwenye hilo suala la ajira bongo. Vijana kama hamna mtu wa kuwashika mkono hapo bongo na hela ya kuhonga hamna mtasubiri mpaka Yesu arudi.
Timkeni mwende ughaibuni, maisha popote.
Vijana hamkuzielewa methali hizi kule mashuleni?
(1) Mguu utokao mtume (SAW) kauombea.
(2) Mgaa gaa na upwa hali wali mkavu.
(3) Mwenda bure si mkaa bure.
(4) Nabii hakubaliki kwao.
Canada🇨🇦, Australia 🇦🇺, New Zealand 🇳🇿, UK 🇬🇧, Rwanda 🇷🇼, Botswana 🇧🇼 .
 
Back
Top Bottom